Shule za serikali kidato 5 wachache waripoti baada kucheleweshwa mwezi mzima, wengi walishaanza shule binafsi. Mabweni na madarasa yamekamilika?

TRAT

Member
Nov 29, 2022
41
117
Waziri mhusika ulikuwa ni mpango wako wa kujaza shule za binafsi kidato Cha 5? Ulichelewesha wanafunzi kuanza shule mwezi mzima kwa sababu ya ujenzi wa mabweni na madarasa.

Tunaomba utujibu ni shule ngapi madarasa na mabweni yamekamilika ndani ya mwezi mmoja na tayari yamepokea wanafunzi.
 
Mama Samia Kila Siku anajenga mabweni,Shule mpya,madarasa,zahanati,vituo vya afya na hospitali mpya..

Sasa hivi mafundi hawapatikani mitaani. Kila ukimgusa anakwambia nina tenda ya serikali
 
Kuchelewa kwako na kuteseka kwako kusiwe SI Unit ya maisha ya wengine. Ushanfahamu?
Acha kudeka, mwezi ni topic ngapi a level!?..hata logic haiishi,ungesoma Azania mid 2000s si ungelia,mwalimu darasani haingii miezi miwili mitatu ya mwanzo,we si kichwa,umetoka na one o level,vitabu vipo,Anza msuli...msimu a level unalia kuchelewa mwezi mmoja!?..hii nchi inaenda wapi!?
 
Acha hoja za kiuwanafunzi Dogo. Kusifia matatizo uliyopitia usifikiri ndio ujanja. Kuna watoto wamezaliwa matawi ya juu. Wamesomea Mzizima na Shaaban Robert za enzi hizo na leo Feza Boys and Girls. Na mpaka leo Wana elimu nzuri na kazi nzuri kukuzidi wewe unayejisifia shida na tabu ulizopitia.

Binafsi nimepitia maisha hayo unayoyazungumzia nikiwa Dakawa High School Miaka ya Tisini. Nini wewe wa Miaka ya Elfu Mbili?
 
Acha kudekeza wasomi,a level siyo ya spoon feeding
 
Halafu wazazi/walezi walipotafuta uhamisho wa wanafunzi kwa sababu mbalimbali waliwakatalia katukatu.

Eti mpaka muongozo utoke baada ya miezi 2-3 baada ya Shule kufunguliwa

Fikiria kwanza Shule wamechelewa kuanza wanaaanza katikati ya mwezi wa 8,

Unawezakuta masomo yataanza labda baada ya wiki 2-3 yaani September huko,

Halafu Eti mzazi unayetaka mwanao uhamisho usubiri baada ya miezi 2-3 yaani October Au November ambako pia itategemea nafasi kuwepo

Yaani kuna mambo ya ajabu huko sijapata kusikia.

Halafu kama hujawahi kukutana na jambo Kama hilo huwezi kujua mambo wanavyofanya.

Kuna jamaa amekasirika kaamua kupeleka mwanae Shule kubwa kwa hasira za urasimu uliopo.
 
Kule Shule binafsi wanaanza mapema,

Wanamaliza mapema ,

Wanapata muda wa revision wa kutosha,

Wanafanya majaribio na mitihani ya kutosha kuwapa stamina ya mitihani ya Taifa.

Na hata wakifika Chuo wanakuwa na msuli mnene sababu ya ushindani mkubwa.

Shule nyingine mwanao anawezakuta anaongoza vilaza.!
 
Back
Top Bottom