Derspiegel
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 285
- 242
Lengo si kukosoa ubora wa elimu inayotolewa kwa shule za sekondari za kata na nikiri kuwa shule hizo zimeongeza chachu kubwa kwa wananchi kuimarisha elimu na huduma nyingine za jamii katika maeneo yao ya vijijini.
Tofauti na nchi nyingine za kiafrika ambazo zimekuwa zikikabiliwa na matatizo ya udini na ukabila, Tanzania tulifanikia kwa kiwango kikubwa kukwepa changamoto hiyo. Mojawapo ya sababi kubwa ya utaifa ni wanafunzi kuchaguliwa kusoma shule za nje ya mikoa yao huku wengo wao wakipangiwa ajira zao nje ya mikoa yao.
Hata hivyo kwa sasa, hali hiyo inabadilika kutokana na kupanuka kwa elimu ya sekondari ambapo wanafunzi wengi wanachaguliwa kuendelea na masomo hayo. Tatizo hapa ni kuwa wanafunzi hao hawapati fursa ya kutembea na kujifunza utamaduni na maendeleo ya sehemu nyingine za nchi na kuwafanya wanafunzi kuwa na identity fulani kwenye fikra zao.
Yote tisa, tatizo linakuja kwenye namna ya kutoa elimu ambayo inadumisha utamaduni wa kitanzania wa moyo wa kupendana na kujaliana miongoni mwa watanzania licha ya nchi yetu kuwa heterogeneous society.
Kuna jamii ambazo zimekuwa zikifanya vyema kielimu nchini lakini nyingine zimekuwa hazifanyi vyema. Hivyo, katika mazingira haya, shule za kata zimepelekea kuongezeka kwa gap kati ya jamii zilizozoeleka kuwa za kielimu na zisizo vizuri kielimu.
Mbaya zaidi ni kuwa, kuna chance kubwa ya mtumishi aliyeajiriwa eneo asilolipenda kuhama eneo hilo kwenda analopenda na hiyo inazidisha jamii nyingine kuwa nyuma still.