SHULE ZA SEKONDARI ZA KATA NA MITIHANI YA TAIFA Vs UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

london

JF-Expert Member
Sep 12, 2010
221
143
Majuzi nilitembelea shule moja ya sekondari ya kata huko kijijini. Nikakuta ina walimu wanne-historia, Jiografia, biology, katika idadi hiyo yumo mkuu wa shule. Nikaelezwa kuwa darasa lilomaliza kidato cha nne hawakuwahi kufundishwa masomo ya sayansi pamoja na hesabu hadi wanafanya mtihani wa taifa 2011. Kibaya zaidi pamoja na kuwa mkuu wa shule ni mwalimu wa hesabu yeye huwa hafundishi kabisa na hakuna anayemlalamikia-wanakijiji au mratibu wa elimu wa kata.Sasa najiuliza hivi kuwafanyisha wanafunzi mitihani kwa masomo ambayo hawakufundishwa kabisa au kumaliza silabasi sio ukiukwaji wa haki za binadamu? Mimi nataka wana JF mnisaidie nini kifanyike ili kuondoa hali hii vinginevyo wanafunzi wa kijijini watabaki nyuma kielimu miaka nendarudi.
 
Back
Top Bottom