Shule za msingi Tanzania hali bado tete, fedha zinazopelekwa shuleni hazitoshi

bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,657
1,992
Ile sera ya elimu bure sasa imedhihirika kuwa ni kaa la moto ktk elimu ya Tanzania kiasi ya kwamba ni dhahiri kabisa itaathili utowaji wa elimu Tanzania.

Hayo yamethihirika wazi ktk kikao cha wazazi kilichofanyika leo ktk shule ya msingi ya Gongolamboto JICA ambapo wazazi wametoa shutuma kali dhidi ya serikali kwamba imekua ikinadi kutoa elimu bure wakati inapeleka fedha kiasi kidogo ambacho hakikidhi mahitaji kabisa.

Akiongea ktk kikao hicho mwalimu mkuu wa shule hiyo ambae hana muda mrefu shuleni hapo, ndg Job Ndugusa alisema kwamba kiasi kinachotolewa ni kidogo sana kiasi kwamba hakitoshi kabisa ktk kuiendesha shule.

Akitoa mchanganuo wa fedha wanazoletewa kila mwezi alisema kwamba,shule inawanafuzi zaidi ya 800 lkn kila mwezi wanaletewa kiasi cha tsh. 490,000 ambacho huwa kimetengewa kabisa matumizi yake. Alisema katika hizo fedha,mitihani ni asilimia 20 na uendeshaji ni asilimia 30. Hivyo ktk mitihani na majaribio ni kiasi kisichozidi 97000 ambazo hazitoshi kabisa kwa wanafunzi kufanya majariobio yao darasani, kununua karatasi, uchapishaji n.k. hali ambayo imepelekea wawe wanaandika mitihani ubaoni ambayo huwa chini ya kiwango.

Mwalimu wa taaluma wa sule hiyo akitoa majumuisho ya kitaaluma alisema kuwahali hiyo imesababisha kushuka kwa viwango vya ufaulu shuleni hapo kwani watoto hawapewi mazoezi ya kutosha. Akitolea mf, alisema mwaka huu walikua na watoto 115 wa darasala saba kati ya hao waliofeli ni 25 tu, hivyo wameshinda kwa kiasi cha asilimia 85. Lkn akasema ushindi huo umekua wa chini sana kwani watoto wameshinda kwa viwango vya chini vya D,C,B na kiasi kidogo sana cha A hali itakayopelekea watoto wengi kukosa kwenda sekondari tofauti na miaka na nyuma
Kutokana na hali hiyo wazazi kwa kauri moja walimuomba mwenyekiti wa bodi ndg Mkama na msaidizi wake ndg Keneth Mfinyu kuwaondoa walimu wote ili wao walijadili swala hilo kama wazazi bila kuwashilikisha walimu.

Katika maamuzi yao wameamua kwa pamoja kuchangia elimu hasa masomo ya ziada pamoja na tuisheni. Mzazi mmoja Juliasi isaya alitoa angalizo kwa wazazi wenzake kuwa wasiwasikilize wana siasa wanaosema elimu bure wakati watoto wao hawasomi shule hizo,wanawapeleka watoto wao kwenye shule za kimataifa

Wameitaka serikali isiwaingilie ktk maamuzi yao kwani wanao halibikiwa ni watoto wao wala si watoto wa Raisi, waziri,RC au DC,. Mzazi mmoja Faraja Mwitaa lisema inaonekana wazi kuwa sera hii ya elimu bure imeisha washinda serikali hivyo ni jukumu la wazazi kuingilia kati la watajikuta wamechelewa.

Tangu aingie madarakani raisi John Pombe Magufuri amekuwa anapambana kuitekeleza sera hii ambayo haikuwa sera ya chama,jambo ambalo linampa shida kubwa kuilikamilisha kwani halikua na maandalizi yoyote wala mfumo maalumu wajinsi ya kulitekeleza kiasi ambacho huumfanya wakati mwingine alalamike kuwa amepewa mzigo mzito unaomuelemea.

HAKIKA HALI NI MBAYA MASHULENI JE HUKO WENZETU WANAJOPOMNAONAJE? NA JE MNATOA USHAURI GANI? TANZANIA NI YETU SOTE TUKIHALIBIKIWA TUNAHALIBIKIWA WOTE'
 
Mmmh, huku kwetu Matepwende - Lusewa, hali ni tofauti , hadi hela inabaki.

Hili suala ni case by case, na ni shule kwa shule, JICA Gongolamboto isihitimishe na tuamini kuwa ni Tanzania yote.
 
Msituletee fyoko fyoko zenu hapa... elimu! elimu! Unaweza kukaa juu ya madaftari au juu ya vitabu au hata juu ya madawati ukaweza kusafari japo kutoka Kibaha hadi Dar es salaam?!

Acheni tununue ndege sisi na ikiwa wewe ndo unajali sana elimu; chukua mshahara wako uwapelekee; ebo!
 
Mmmh, huku kwetu Matepwende - Lusewa, hali ni tofauti , hadi hela inabaki.

Hili suala ni case by case, na ni shule kwa shule, JICA Gongolamboto isihitimishe na tuamini kuwa ni Tanzania yote.
Umesema wa kunyuamba
 
Niliwahi kushauri humu juu ya kufanya jambo bila utafiti. Hili la Elimu bure kwa zama hizi ni gumu kutekekelezeka. Na hakuna rejea yoyote juu hill kuwa kuna nchi duniani zinazopractice hili kwa asilimia mia.
Hata mmem na Mmes hayakuenda moja kwa moja nchi nzima bali kuna baadhi ya maeneo yaliyoteuliwa kwa majaribio ili kuona na kupima mafanikio na mapungufu. Hili LA sasa halikupewa nafasi wala maandalizi na matokeo take ni mabaya kuliko ilivyotarajiwa.
Sh.200/= kwa mwezi kwa kila mwanafunzi ni utani kwa watoto wetu. Yabidi wazazi watafakari hatima ya watoto wao Kama kweli wanawapenda. Kuisubiri serikali hii kuinua taaluma ya mwanao ni sawa na kulisubiri dodo chini ya mwarobaini.
 
  • Thanks
Reactions: bne
Waacheni watoto wasome hivyo hivyo tu, wakimaliza kidato cha sita inakuwa rahisi kupata mikopo kwa hao waliosoma shule za Kata, mikopo yenyewe inatolewa kwa ubaguzi, aisee nchi hii ina vituko vingi sana
 
Mmmh, huku kwetu Matepwende - Lusewa, hali ni tofauti , hadi hela inabaki.

Hili suala ni case by case, na ni shule kwa shule, JICA Gongolamboto isihitimishe na tuamini kuwa ni Tanzania yote.
Kama shule ya wanafunzi 800 inapewa almost laki 4 je uko maporini kwenye wanafunzi 150 hali ikoje? Ukweli ni kuwa Sera hii imeshindikana Tanzania inalazimishwa na wanasiasa, madhara ni kwa watoto wetu
 
  • Thanks
Reactions: bne
Nazidi kusisitiza ishu ya elimu bure CCM walikurupuka bila kuwa na mipango.Walikurupuka baada ya kusikia CHADEMA wanaongelea elimu bure na wao wakaanza kuongelea kwenye kampeni bila kuwa na mipango wata finance vipi hiyo sera. Mkulu alivyoingia tu madarakani akaagiza kuanzia january elimu bure huku serikali ikiwa haina bajeti hiyo. Kilochofwata sote tunakijua. Kiukweli elimu inazidi kushuka,primary schools na secondary schools. Serikali ina hali mbaya ndo maana hata vocha wanachukua kodi. Hell this country.
 
  • Thanks
Reactions: bne
Mtoto wangu atasoma private mwanzo mwisho. Kwan mkopo kitu gani?
Watoto wa viongozi wanasoma shule za private. Ndiyo maana hawajali.
ELIMU IKIINGILIWA NA WANASIASA, INAPOTEZA UBORA WAKE.
 
  • Thanks
Reactions: bne
Ile sera ya elimu bure sasa imedhihirika kuwa ni kaa la moto ktk elimu ya Tanzania kiasi ya kwamba ni dhahiri kabisa itaathili utowaji wa elimu Tanzania.

Hayo yamethihirika wazi ktk kikao cha wazazi kilichofanyika leo ktk shule ya msingi ya Gongolamboto JICA ambapo wazazi wametoa shutuma kali dhidi ya serikali kwamba imekua ikinadi kutoa elimu bure wakati inapeleka fedha kiasi kidogo ambacho hakikidhi mahitaji kabisa.

Akiongea ktk kikao hicho mwalimu mkuu wa shule hiyo ambae hana muda mrefu shuleni hapo, ndg Job Ndugusa alisema kwamba kiasi kinachotolewa ni kidogo sana kiasi kwamba hakitoshi kabisa ktk kuiendesha shule.

Akitoa mchanganuo wa fedha wanazoletewa kila mwezi alisema kwamba,shule inawanafuzi zaidi ya 800 lkn kila mwezi wanaletewa kiasi cha tsh. 490,000 ambacho huwa kimetengewa kabisa matumizi yake. Alisema katika hizo fedha,mitihani ni asilimia 20 na uendeshaji ni asilimia 30. Hivyo ktk mitihani na majaribio ni kiasi kisichozidi 97000 ambazo hazitoshi kabisa kwa wanafunzi kufanya majariobio yao darasani, kununua karatasi, uchapishaji n.k. hali ambayo imepelekea wawe wanaandika mitihani ubaoni ambayo huwa chini ya kiwango.

Mwalimu wa taaluma wa sule hiyo akitoa majumuisho ya kitaaluma alisema kuwahali hiyo imesababisha kushuka kwa viwango vya ufaulu shuleni hapo kwani watoto hawapewi mazoezi ya kutosha. Akitolea mf, alisema mwaka huu walikua na watoto 115 wa darasala saba kati ya hao waliofeli ni 25 tu, hivyo wameshinda kwa kiasi cha asilimia 85. Lkn akasema ushindi huo umekua wa chini sana kwani watoto wameshinda kwa viwango vya chini vya D,C,B na kiasi kidogo sana cha A hali itakayopelekea watoto wengi kukosa kwenda sekondari tofauti na miaka na nyuma
Kutokana na hali hiyo wazazi kwa kauri moja walimuomba mwenyekiti wa bodi ndg Mkama na msaidizi wake ndg Keneth Mfinyu kuwaondoa walimu wote ili wao walijadili swala hilo kama wazazi bila kuwashilikisha walimu.

Katika maamuzi yao wameamua kwa pamoja kuchangia elimu hasa masomo ya ziada pamoja na tuisheni. Mzazi mmoja Juliasi isaya alitoa angalizo kwa wazazi wenzake kuwa wasiwasikilize wana siasa wanaosema elimu bure wakati watoto wao hawasomi shule hizo,wanawapeleka watoto wao kwenye shule za kimataifa

Wameitaka serikali isiwaingilie ktk maamuzi yao kwani wanao halibikiwa ni watoto wao wala si watoto wa Raisi, waziri,RC au DC,. Mzazi mmoja Faraja Mwitaa lisema inaonekana wazi kuwa sera hii ya elimu bure imeisha washinda serikali hivyo ni jukumu la wazazi kuingilia kati la watajikuta wamechelewa.

Tangu aingie madarakani raisi John Pombe Magufuri amekuwa anapambana kuitekeleza sera hii ambayo haikuwa sera ya chama,jambo ambalo linampa shida kubwa kuilikamilisha kwani halikua na maandalizi yoyote wala mfumo maalumu wajinsi ya kulitekeleza kiasi ambacho huumfanya wakati mwingine alalamike kuwa amepewa mzigo mzito unaomuelemea.

HAKIKA HALI NI MBAYA MASHULENI JE HUKO WENZETU WANAJOPOMNAONAJE? NA JE MNATOA USHAURI GANI? TANZANIA NI YETU SOTE TUKIHALIBIKIWA TUNAHALIBIKIWA WOTE'
Tuachage kulaumulaumu wakati Serikali haijaanza huu utaratibu tulikua tunalalamika ,sasa hivi Serikali inajitahidi bado watu wanalalamika.
 
Ndg utaratibu lazima uendane na mafanikio. Huwezi kuua elimu ya mtoto wangu halafu useme me nilikua na Nia njema il uwezo sikua nao. Hilo neno linamsaidiaje yule ambae tayari amekwisha athirika? MAJI UKIYAVULIA NGUO.....
 
Back
Top Bottom