Shule za English medium za serikali

PRINCEd

JF-Expert Member
Dec 14, 2015
850
586
Kwa wenye kumbukumbu nzuri, mtakumbuka kipindi Rais akitanganza azimio la kuondoa ada kwa shule za msingi za umma. Rais alitaja shule sita kuwa shule hizi zitaendelea na utaratibu wa ada na kati ya shule zilizotajwa ni Bunge(Dar), Mlimani (Dar) na Olimpio (Dar).

Kwa utafiti wangu mdogo niligundua kuwa shule hizi wanafunzi wake wanajifunza (medium of instruction) kwa kutumia lugha ya Kingereza, yaani English medium.

Hoja yangu...

Kwanini serikali isianzishe shule za namna hii atleast shule 50 kila mkoa?

Mchakato wa kupata wanafunzi wa shule hizi ukoje, kwani niligundua kuna watoto wanatoka Madale kwenda Upanga, je mchakato ni wa wazi?

Ni watoto wa Watanzania wenye hadhi hudailiwaa pale na kiwango cha ada kikoje?

Naomba kuwasilisha.
 
acheni kupenda vya bure ndugu zangu elimu nigharama...sana...ukiifanyia masikhara na yenyewe inakuletea umasikhara...hizo nishule za bure tusipende vya bure
 
Back
Top Bottom