Shule yaridhia mwalimu aache kazi kwa kudaiwa shoga

Pepombili

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
439
58
Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Majengo, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi umeridhia kuacha kazi kwa mwalimu wa kiume wa shule hiyo anayedaiwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.Kufuatia hatua hiyo, Bodi ya shule imemlipa mwalimu huyo Endrew Katto, Sh. 2,409,924 kama kiinua mgongo baada ya kuitumikia shule hiyo kwa miaka sita.Mwalimu Katto aliajiriwa katika shule hiyo Februari Mosi, 2006 hadi Februari Mosi mwaka huu, alipoamua kuandika barua hiyo na kumfungulia kesi Mkuu wa shule hiyo, Bruda Peter Lyimo, kwa madai ya kumtukana kwa maandishi katika kituo kikuu cha polisi Mjini Moshi na kufungua jalada Na.MOS/RB/11709/2012

Alipotakiwa na NIPASHE kueleza sababu za kuandikiwa barua hiyo alisema hawezi kuzungumzia kwa undani kwa kuwa alishamuelekeza wakili wake kuchukua hatua za kisheria
Aidha, mwalimu huyo amewasilisha barua ya kutaka aombwe radhi na kulipwa fidia ya Sh milioni 800 kupitia wakili wake Kipoko & Advocate, akidai kuwa Bodi ya shule imemdhalilisha na kuchafulia jalada la taaluma yake hali inayomsababishia asiajiriwe sehemu yoyote.Hata hivyo, wakili huyo aliiambia NIPASHE kwa njia ya simu kuwa endapo watamuomba radhi mteja wake na kumlipa gharama na kuridhika hawataenda mahakamaniKwa mujibu wa barua ya Mkuu wa shule hiyo, Bruda Peter Lyimo ya 18/04/2012 yenye kumbukumbu Na. MSS/PP/AK/189/30 imeeleza kuwa uongozi wa shule umeridhia mwalimu huyo kuacha kazi baada ya kubainika kuwa alikuwa akijihusisha na masuala ya kujamiiana kinyume cha maumbile.

"The school administration received your letter dated 12.04.2012 in which you clearly stated that you will not keep on working at this shool as a teacher after a homosexual scandal was revealed on you" (Utawala wa shule umepokea barua yako ya tarehe 12. 04. 2012 ambayo umeeleza wazi kuwa huwezi kufanyakazi katika shule hii kama mwalimu baada ya kubainika kwa kashfa dhidi yako ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja),"
ilisomeka sehemu ya barua hiyo ikimaanisha kuwa kuacha kazi kwa mwalimu huyo kulitokana na kubainika kushiriki suala la ushoga.

Akizungumza na NIPASHE ofisini kwake, Bruda Lyimo alikiri kuandika barua hiyo kwa maelezo kuwa aliiandika akiwa makini kwa kuwa ushahidi upo nakuongeza kuwa Majengo Sekondari ni shule inayoheshimika nchini kwa elimu na malezi bora kwa hiyo sio busara kuendelea kuwa na mwalimu aliyekiri kuwa ni shoga.
Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Elimu Jimbo Katoliki la Moshi, Padre Wiliamu Ruaichi, zimeeleza kuwa uongozi wa kanisa hilo bado unatafakari hatua iliyochukuliwa na bodi.
 
Bruda Lyimo anaposema ana ushahidi nashindwa kuelewa kuwa utakuwa ushahidi wa namna gani?!

1. Atakuwa na vijana walioshiriki nae tendo la ushoga?!

2. Ana vielelezo zinavyo onyesha kuwa mwalimu wake anafanya ushoga na wanafunzi shuleni au majumbani?

Hili sakata linaweza kuwa gharimu sana manajement ya Majengo.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums
 
Mungu ni mwema bora ameondolewa mapema na kwa shule nyinginezo tafadhali asiajiriwe huyu mwalimu atamaliza watoto na vijukuu vyetu. Ahamie kwa OBAMA na CAMEROON!!!
 
Majengooooooooooooo. Nakumbuka mlishawahi kuwa na Denti shoga hapo, mkamtimua akahamia Singe babati
 
Bruda Lyimo anaposema ana ushahidi nashindwa kuelewa kuwa utakuwa ushahidi wa namna gani?!

1. Atakuwa na vijana walioshiriki nae tendo la ushoga?!

2. Ana vielelezo zinavyo onyesha kuwa mwalimu wake anafanya ushoga na wanafunzi shuleni au majumbani?

Hili sakata linaweza kuwa gharimu sana manajement ya Majengo.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums
Ukweli uyo mwalimu ni shoga..ISITOSHE alishafumaniwa na mkewe akiriwa tigo,kuna vijana aliwapangishia chumba kwa ajiri ya kumunanii alafu tabia zake zinajulikana majengo nzima..Ebu waulize PCB wakupe habari zake kwa urefu na mapana mkuu
 
aah !! TICHA WA PCB huyo ticha alikuwa na mbwembwe balaaah nikikumbuka jinsi alivyokuwa akiongea hahahahahah kwanza hakuwa deep bioz ka ticha NELIGWA
 
Kivipi mkuu, alikuwa akitembea anakatikakatika nini!!??

kwanza alikuwa anatembea kidada mwanaume gani unabinua sehemu za nyuma? Pili anarembuwa tatu mapozi ya kishost duu na marafiki zake waliomaliza nawasiwasi nao kwa sababu walikuwa nao hawaeleweki hongera broda Lymo kwa kulitamuwa hilo KISS THE GROUND
 
afu kuna kipindi huyu ticha alichezea kichapo kwa kufumaniwa na Mke wa mtu !! Akasimamishwa kufundisha nadhani mwaka huu karudishwa tena hahahahahah ticha wa pcb
 
kwanza alikuwa anatembea kidada mwanaume gani unabinua sehemu za nyuma? Pili anarembuwa tatu mapozi ya kishost duu na marafiki zake waliomaliza nawasiwasi nao kwa sababu walikuwa nao hawaeleweki hongera broda Lymo kwa kulitamuwa hilo KISS THE GRAUND

when i just see you roaming around hakuna lugha nyingine nitakayo zungumuza bt i will just say kiss the ground
 
Bruda Lyimo anaposema ana ushahidi nashindwa kuelewa kuwa utakuwa ushahidi wa namna gani?!

1. Atakuwa na vijana walioshiriki nae tendo la ushoga?!

2. Ana vielelezo zinavyo onyesha kuwa mwalimu wake anafanya ushoga na wanafunzi shuleni au majumbani?

Hili sakata linaweza kuwa gharimu sana manajement ya Majengo.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums

Litawagharimu sio kidogo,kuna hizi taasisi zinapigania haki za binadamu soon wakilinasa imekula kwao.Huyu Bruda ni mtu wa kukurupuka sana .Ila kanisa Katoliki linawalea sana hawa kina Bruda ,sioni logit ya kuandika barua yenye maneno makali kiasi hicho kwa mtumishi aliyefanya kazi chini yake miaka 6. Barua inaonyesha wazi kuna chuki na ugomvi uliozuka kati ya huyo mwl. Na Bruda,hata kama tuhuma hizo ni za kweli.

Nakumbuka miaka ya 2001/02 kulikuwa na kesi ya mwanafunzi kufukuzwa shule kutokana na kuwa na wastani wa chini kulingana na viwango vyao.Alimropokea mzazi wa yule mwanafunzi ila mwisho wa siku mambo yalipokwenda mahakamani ikabidi aombe yaondolewe mahakamani na mwanafunzi arudishwe shule pamoja na fidia.
 
Back
Top Bottom