Shule ya Sekondari Mbeya DAY!!

Shule ya Sekondari Mbeya DAY!!

Matukuta Jr

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
207
Reaction score
27
Hii ni moja ya Shule za Serikali hapa Mkoani Mbeya inayoongoza kwa Ufaulu na kuupa Mkoa Heshima.
Ni kwa Matokeo yote Form 4 na 6

Mlioko Mbeya na Mliosoma hapa na kuhifahamu hii Shule nadhani sijakosea.

#Hakika wana Mbeya tunajivunia Shule hii ambayo Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba Ndg. Peter Mchechu,Mbunge wetu Mhe. Joseph Mbilinyi pamoja na Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Philipo Mulugo wamesoma hapa na watu wengine kibao tu!
 
Attachments

  • Photo0074.jpg
    Photo0074.jpg
    253 KB · Views: 411
Mulugo...!? huyo ndo kaharibu...!
 
Huyu Mulugo anatuharibia sifa ya shule yetu, pambafy !! Mliosoma hapo tukumbushane waalimu: Mbawala, Mwakamele (duh kabla ya kuokoka jamaa huyu alikuwa anapiga bakora kama mwehu...sura yake na wasirra sijui nani zaidi ), Mpesya (duh huyu kalamba sana wanafunzi ofisini, vyooni ect), Mama Sombrero, duh yule mwalimu wa hesabu alikuwa na mzuzu, na yule mwingine kamwili kadogo lkn namba zinashuka sana na ana kiburi nimesahau jina, ....duh tumetoka mbali jamani. Yule headmaster gwiji, chain smoker na asiyeongea na mtu hata mwezi mzima... ha ha
 
lakini Sugu aliishia Kidato cha Pili hapa.
Unamkumbuka Mwl. Malanyingi pande Cooker and Nutrition?
 
Mwampale, mwanyingili, magelewanya, msuku.
Namiss sana those tymz.

Ila kuna watu km kina M23 wanaidharirisha sana shule.
 
Last edited by a moderator:
M 23 ndiyo nani tena ?

Kuna kijana mmoja humu jf. Alikuwa mgombea ubunge jimbo flan mbeya huko kupitia cdm. Akasaliti chama, akafukuzwa na sasa anafanya kazi lumumba chini ya payrol ya "nepi" na "n'chemba".
 
Duh...ngoja nitamfuatilia....basi noma sana huyo kuendekeza njaa...
Kuna kijana mmoja humu jf. Alikuwa mgombea ubunge jimbo flan mbeya huko kupitia cdm. Akasaliti chama, akafukuzwa na sasa anafanya kazi lumumba chini ya payrol ya "nepi" na "n'chemba".
 
Vijana acheni kuleta Propaganda kwenye thread zisizo na Usiasa.
 
Ha ha ha ha nimesoma pale Head Master akiwa S.P Shauri. Sijajuta kusoma pale
 
Wakuu mbona naskia Swilla sec ndiyo the best school in Mbeya? Au mi ndo nimechanganya mafile kichwani.
 
Huyu Mulugo anatuharibia sifa ya shule yetu, pambafy !! Mliosoma hapo tukumbushane waalimu: Mbawala, Mwakamele (duh kabla ya kuokoka jamaa huyu alikuwa anapiga bakora kama mwehu...sura yake na wasirra sijui nani zaidi ), Mpesya (duh huyu kalamba sana wanafunzi ofisini, vyooni ect), Mama Sombrero, duh yule mwalimu wa hesabu alikuwa na mzuzu, na yule mwingine kamwili kadogo lkn namba zinashuka sana na ana kiburi nimesahau jina, ....duh tumetoka mbali jamani. Yule headmaster gwiji, chain smoker na asiyeongea na mtu hata mwezi mzima... ha ha
Mkuu naona ulikuwepo hapo miaka ambayo na mimi nilisoma, hao waalimu uliowataja duu. Yule headmaster unamaanisha Nisajile nini? Aliyekuwa anashusha sana namba wakati huo na mwenye mzuzu alikuwa anaitwa Gwasa, Mama Sombrero - Manyama, Mbawala - second master Mwalimu wa English alikuwa anatumia sana ndizi choma na maparachichi ya pale Mbogoso sijui kama bado ipo Mbogoso! Mwl. wa nidhamu Mwakamele kwa miaka minne niliyokuwepo Mbeya Day nilimuona mara moja tu akiwa hajavaa koti la suti na wanafunzi wengi sana walitoka madarasani kumuangalia alivyokuwa anaonekana. Angekuwa ni Mtu wa Musoma lazima angekuwa ni ndugu na Wasira haah haaa!!
 
Marehemu swakasonda, hastings, mwampale, second master mwakasala mzee wa viboko vyote chake na miti

ahaahaa hastings na rafikiye Kiduduye. Kwenye chipsi na mihogo tulikuwa na Mama one. Kulikuwa na wali mpk wa tsh. 150 by then. That waz life.
 
Last edited by a moderator:
Acheni kujisifia ujinga, kama we unaesema eti.... Na ukascore 0 au unataka nikutaje? Utaibika coz nakujua frm A-Z. In life circle tunaangalia specific reference sio generic reference ok.
 
Dah kweli umenikumbusha mbali sana. Gwasa bwana na mbwembwe zake na kale kamwili kamekomaa utafikiri Remires wa Chelsea..ha ha ha. Mama Manyama nae alikuwa anachukia sana wasichana wazuri au tudume tulitwoonekana mbegu, na shoto lake lahaula..!!
Kweli kabisa inaelekea ni miaka hiyo hiyo mkuu. Mimi nilikuwa Maiko Jodan wa enzi hizo 🙂 piga sana ball pale ktk uwanja ule uliokuwa katikati wa zege !! Pia yale mambo ya disko na yule DJ Bulushi (maiko jackson wa Mbeya, na push back lake la nguvu na don't touch dah...ama kweli vya kale dhahabu (demu wa DJ alikuwa anasoma pale mbele yetu, Hellen ? Enzi za mtemi wa mujini Biso na trupu zima la Sangu sec... !! Sisi tulikuwa pia tunakipiga sana kiputa pale na mara kadhaa tulizichapa sana na Iyunga na Meta !!

Nisajile alikuwa balaa, moto wa kuotea mbali na fegi zake 24/7

Hawa akina mulugo ndo walikuwa hawalali usiku, wanasomea miguu ikiwa ktk mabeseni na kwenda kuiba chapati kwa wamama wa jirani, nyumba za FFU ??

Back
Top Bottom