Shule ya Nganza Girls ya jijini Mwanza katika kashfa nzito.

Shule ya Nganza Girls ya jijini Mwanza katika kashfa nzito.

Huu uongo hata housegirl ataugundua..

Hivi mnapata nini kwa kupost uahetani?
 
hiki nacho kipaji maalumu mwanafunzi kuwa JF wakati wa masomo!
 
Shule kongwe ya wasichana wenye vipaji maalum Almaarufu kama Nganza High School iliyopo jijini Mwanza imeingia katika mgogoro mkubwa unaofukuta chini kwa chini kati ya wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo na Uongozi wa shule hiyo ikihusisha walimu na wanafunzi wa shule hiyo, baada ya viongozi wa shule hiyo kuanza kuwabebesha wanafunzi wa kidato cha Tano na cha Sita jukumu la kujenga madarasa ya shule hiyo kama sehemu ya Adhabu kwa makosa mbali mbali katika mfumo ufuatao.

Imeelezwa kua pale inapotokea mwanafunzi amefanya kosa lolote adhabu zinazotolewa hapo shuleni ni mwanafunzi kutakiwa kununua matofali ya block yasiyopungua kati ya matofali 1000 mpaka 2000 kulingana na aina ya kosa ndio na idadi ya matofali inavyoongezeka ama kupungua.

Aidha pia imeelezwa kua moja ya ukiritimba unaofanyika shuleni hapo ni pamoja na Viranja wa shule hiyo ambao nao pia ni wanafunzi kupewa mamlaka na walimu ya kumuadhibisha mwanafunzi mwenzake kwa kumcharaza viboko mbele ya wanafunzi wenzake.

Wana JF mnalizungumziaje hili..Je ni sahihi kwa aina ya adhabu hizi zinazotolewa ama si sahihi na je nini kifanyike????

Jamani mimi nimesoma hiyo shule, nimemaliza form six hapo 2010! Jamani hiyo shule kwa adhabu hawajambo. Jamani enzi zetu ilikuwa ni kuponda kokoto ndoo kumi na tano peke yako au kubeba Moram kuroka huko misituni, kuchimba mitaro nk! Jamani wale watu wana adhabu zilizoenda shule to yje extent kwamba hautamani hata ifike wewk end maana lazima wakutafutie kosa lolote ili tu ufanye adhabu! Makosa yao ni madogo madogo tu kama kuongea kiswahili ambayo hayaendani na adhabu mtu anayofanya! Unaweza ukajikuta hata una adhabu karibia tano kwa siku moja na Yule headmistress Madam Shimo alivyo na roho mbaya wanafunzi wanakoma! That is the sad truth, wahusika waliangalie hili its not fair kabisa!
 
UJAMAA NA KUJITEGEMA HUO NA MADhara yake
 
Haiwezekani...though nakumbuka miaka hiiyoo tulikuwa tunabebeshwa moram ndoo kedekede kutoka ile milima ya mawe km adhabu. Zilikuwa adhabu ngumuuu.
Ila hii ya matofali zidhanii
 
Ada elfu 70.. alafu matofali ya milion 1.. kweli ni shule ya vipaji maalumu
 
Usibishe kitu kama hujafanya Research ya kutosha...waulizeni form six waliomaliza hiyo shule juzi..ijumaa na wengine wa kombi za Sayansi ambao bado wanaendelea na mitihani wawape habari vizuri...dhabu zinatofautiana...kuna wengine matofali 600 wengine 800 wengine 1000..kutegemea na kosa....Shule hiyo saiv inatoa adhabu za aina hiyo kwa kile kinachoitwa adhabu za kimaendeleo....coz wapo katika kuongeza madarasa...na juzi tuu kwenye graduatiom inaelezwa kua mgeni rasmi aliwaahid mifuko kibao ya Saruji...kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya kwa sasa ambao upo on progress
 
Jamani mimi nimesoma hiyo shule, nimemaliza form six hapo 2010! Jamani hiyo shule kwa adhabu hawajambo. Jamani enzi zetu ilikuwa ni kuponda kokoto ndoo kumi na tano peke yako au kubeba Moram kuroka huko misituni, kuchimba mitaro nk! Jamani wale watu wana adhabu zilizoenda shule to yje extent kwamba hautamani hata ifike wewk end maana lazima wakutafutie kosa lolote ili tu ufanye adhabu! Makosa yao ni madogo madogo tu kama kuongea kiswahili ambayo hayaendani na adhabu mtu anayofanya! Unaweza ukajikuta hata una adhabu karibia tano kwa siku moja na Yule headmistress Madam Shimo alivyo na roho mbaya wanafunzi wanakoma! That is the sad truth, wahusika waliangalie hili its not fair kabisa!

Umenikumbusha mbali sana. Nimebeba moram mm Nganza sitaki kukumbuka.
 
Hukutwanga kokoto? Hukwenda lake kuchota maji? Mwaka gani huo??

Enzi za marehemu mama SEIF, LAKE kuchita nami nimeenda saana, ila kokoto namshukuru Mungu sikuwahi, ila nakumbuka siku yakwanza nimeripoti tu km saa 1 usiku, kesho yakoe ahsubuh nasubiri kujisajili nasikia jina langu linatajwa swahili speakers, sitaisahau hiyo siku kwa kweli, day 1 nilibeba bucket 10 za moram. Kulikuwa na kawalimu kamoja kembambaa keusi kasukuma ndo kalikuwa kwenye english speaking programme hata jina nimekasahau, kana roho mbaya sijapataa kuonaa
 
Naomba ninukuu chanzo kimojawapo cha habari

""Kuna mengine yalojitokeza. Walokamatwa na cm ijumaa wameambiwa wapeleke Lori 2 ya mawe Kila m1."""
Mwisho wa kunukuu

Baada ya mda ntawaletea ushahidi wa barua ambazo wanafunzi hao wamepewa toka shuleni zikiwapa amri ya kutekeleza hizo adhabu..
 
mkuu wake ni yule mama mrefuuu sijui anaitwa nani ila ni mzuri kweli! chadema hoyeeeee!ukawa hoyee!
 
Ndugu JF S.E.Memeber, Jambo usilolijua usilivalie njuga litakuumiza kichwa bureeee. KUMBUKA la KUAMBIWA siku zote CHANGANYA NA FIKRA ZAKO.

Kumbuka na waalimu wanawapenda WATOTO hawa pengine KULIKO wewe mzazi. Wewe unakaa na mwanao kwa muda gani kwa mwaka.Hayo ni malezi usiingilie wazazi wenzako.Kosa la kufukuzwa na tofali za kuchoma 600 ziko sawa. Usilipuke wazazi walio ona uzito wametekeleza.Adhabu lengo ni kuzuia uhalifu zaidi kumbuka kulea wanafunzi mia saba si
mchezo.WEWE WAWILI WANAKUTOA JASHO.wenzio wana kikosi unafanya mchezo.
 
Yaani mwanafunzi unachapwa na kiranja?...

Hiyo kitu ndio ilinifanya nimng'oe meno mawili kaka mkuu wa shule yangu, tena bila ganzi, kiti ndio kifaa kilichotumika, sintosahau, sijui huko alipo huwa ananikumbuka! Kama yumo humu JF Naomba anisamehe bure.
 
Walimu wetu hutenda bila sheria.Huo ni uvunjaji wa Haki za Binadamu.
 
Back
Top Bottom