Mugabe wa Bongo
Senior Member
- Apr 14, 2012
- 145
- 73
Shule kongwe ya wasichana wenye vipaji maalum Almaarufu kama Nganza High School iliyopo jijini Mwanza imeingia katika mgogoro mkubwa unaofukuta chini kwa chini kati ya wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo na Uongozi wa shule hiyo ikihusisha walimu na wanafunzi wa shule hiyo, baada ya viongozi wa shule hiyo kuanza kuwabebesha wanafunzi wa kidato cha Tano na cha Sita jukumu la kujenga madarasa ya shule hiyo kama sehemu ya Adhabu kwa makosa mbali mbali katika mfumo ufuatao.
Imeelezwa kua pale inapotokea mwanafunzi amefanya kosa lolote adhabu zinazotolewa hapo shuleni ni mwanafunzi kutakiwa kununua matofali ya block yasiyopungua kati ya matofali 1000 mpaka 2000 kulingana na aina ya kosa ndio na idadi ya matofali inavyoongezeka ama kupungua.
Aidha pia imeelezwa kua moja ya ukiritimba unaofanyika shuleni hapo ni pamoja na Viranja wa shule hiyo ambao nao pia ni wanafunzi kupewa mamlaka na walimu ya kumuadhibisha mwanafunzi mwenzake kwa kumcharaza viboko mbele ya wanafunzi wenzake.
Wana JF mnalizungumziaje hili..Je ni sahihi kwa aina ya adhabu hizi zinazotolewa ama si sahihi na je nini kifanyike????