born to win
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 561
- 168
by ngoko la 1 - form iv chuo ndo mimepanda gar
Asubuhi had kumi na nusu shule ya msingi mlikua mnasoma nini mkuu,sisi darasa la kwanza na la pili tulikua tunatoka saa 5 tu, la tatu na la nne tunaingia saa 4 tunatoka saa9, darasa la tano hadi la saba tunaingia saa 1 na nusu tunatoka saa 8 mchana.
Kusema kweli utaratibu huu ulibadilisha mimi nikiwa shule ya msingi. Nilidhani wamebadilisha nchi nzima wa kuingis asubuhi na kutoka mchana bila kurudi shule. kwa maajabu nadhani mpaka leo wa vijijini wanarudia kwa kweli sijaelewa vizuri logic ukizingatia vijijini shule ziko mbali zaidi ya mjini, wanawasumbua watoto kurudi majumbani ambapo wakati mwingine hamna chakula hivyo watoto wanaenda na kurudi bila hata kula. Watunga sera wa elimu hebu mtufafanulie, je bado vijijini watoto wanarudia? je kuna tija yoyote? kama la iwe kama ya mjini ili watoto wapate kupimzika na muda mwingine wawasaidie wazazi wao!Huku mjini ndio walikuwa wanatoka saa nane na nusu....ila nilipohamishiwa huko Geita mzee..shule ni hadi saa kumi na nusu jioni...tena madarasa yalikuwa ni ya kugeukiana...yani sisi darasa la tatu na la tano tulikuwa class moja...mnapeana migongo tu..na la nne wanakaa na la sita..alaf la saba ndo wanakaa pekeyao...
ratiba ilikuwa saa mbili kamili asbui mnaingia class hadi saa nne break fupi..mnarudi class...kutoka tena ni saa sita kamili mchana mnarudi nyumbani kula hadi saa nane kamili.mnaingia class tena hadi saa tisa na nusu..hapo sasa mnaanza stadi za maisha...kama ni kulima shamba la shule, kwenda kwa mwalimu mkuu kujenga nyumba yake ya udongo, au kutafuta kuni kwa mwalimu wa zamu..u name it...hadi kumi unusu tunarejesha majeshi nyumbani
Mkuu Ndo mlikuwa mnalolitumia nn ? 😀😀😀
Kumbe chekechea umesomea Chuo Cha Ushirika...sasa nimeelewa why you're very knowledgeable about mambo ya mapolisi.
By the way nimepitia Old Moshi Sec pale...those good years!