Shule ya msingi ulienda kwa style ipi?

Shule ya msingi ulienda kwa style ipi?

Huku mjini ndio walikuwa wanatoka saa nane na nusu....ila nilipohamishiwa huko Geita mzee..shule ni hadi saa kumi na nusu jioni...tena madarasa yalikuwa ni ya kugeukiana...yani sisi darasa la tatu na la tano tulikuwa class moja...mnapeana migongo tu..na la nne wanakaa na la sita..alaf la saba ndo wanakaa pekeyao...

ratiba ilikuwa saa mbili kamili asbui mnaingia class hadi saa nne break fupi..mnarudi class...kutoka tena ni saa sita kamili mchana mnarudi nyumbani kula hadi saa nane kamili.mnaingia class tena hadi saa tisa na nusu..hapo sasa mnaanza stadi za maisha...kama ni kulima shamba la shule, kwenda kwa mwalimu mkuu kujenga nyumba yake ya udongo, au kutafuta kuni kwa mwalimu wa zamu..u name it...hadi kumi unusu tunarejesha majeshi nyumbani
Duh, pole mkuu, ungewaomba wazee wakurudishe mjini,ila hiyo ya kurudi kula nyumbani nayo ilichangia mngeweza kupumzika nusu saa then class hadi saa nane mnatimka kimoja, stadi za maisha sisi zilikua na siku maalum na zinzchukua muda wa vipindi vingine, sio kukaa hadi jioni, vilevile asubuhi kuna nusu saa ya kushughulika na bustani, basi hiyo ilikua inatosha. ila changamoto za vijijini utakuta mwalimu hana maji inabidi mkamchotee, la sivyo anahamia shule za mjini. Ila nazo zinakomaza
 
namba inne ilikuwa inahusika sana enzi zangu ila dei wani wani nilikuwa nakwea UDA kama nikiwa nimechelewa sana
 
Nilienda kwa lift ya basi la jeshi toka tazara-g/mboto kurudi ndio kwa daladala.
 
Back
Top Bottom