Shule ya msingi Kisambi iliyopo Bagamoyo inatia aibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule ya msingi Kisambi iliyopo Bagamoyo inatia aibu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mgelukila, Jun 11, 2012.

 1. M

  Mgelukila JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shule ya msingi Kisambi ipo bagamoyo inawalimu 2 tu shule haina nyumba ya mwl, mwl mkuu anatembea males 16 kufika shule, darasa moja wanasoma wanafunzi wa madarasa matatu kwa pamoja yani la 1, la 2,la 3 shule ya miti ipo wazi mifugo inaingia darasani na kunya hovyo, kijiji kimezungukwa na wakulima na wafugaji inatokea siku walimu wote wawili hawapo hawasomi hivi wizara ya elimi ipo?

  Waziri husika yupo? Bagamoyo si ndipo alipotoka mkuu wa nchi? Wanasubili M4C iwakomboe? Mwanafunzi photocopy haijui, sayansi na tekinolojia itamkomboa vipi tuliambiwa Ardhi,Siasa safi na uongozi bora nchi itaendelea sasa miaka 50 ya uhuru tupo wapi? Nawasilisha

  SOURCE: Taarifa ya habari ITV
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hao ndio wakina magufuli wanasema wameleta maendeleo kwenye ile operation jaza uwanja
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Hayo ndio maisha bora kwa kila mtanzania! Ndio kukua kwa uchumi! Ndio fahari ya ccm! Ndio everything! Period...!
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Habari hizi zinahusu SIASA? UNAHARIBU JAMII FORUM MPANGILIO WAKE... Nadhani unajua Jinsi ya kuposti Habari

  Hii ya Mwanafunzi kutokujua PHOTOCOPY kweli ni SIASA?
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Mfanyabiashara maarufu amejenga darasa moja kwa tenda ya halmashauri sh 56milion huko bagamoyo.ufisadi uliokubuhu ccm na serikali yake
   
 6. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Jamani inasikitisha sana wakati mikutano ya siasa masaa 2 wanatumia 200m kuandaa ........na ndio wilaya ya Mh Rais JK!hatari sana kuna haja ya kuitisha harambee kuwasaidia hao wahanga kwa kweli!madarasa yote na nyumba za walimu hata 5 hivi walimu watakuja tu na kukaa pale!!!!
   
 7. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Nimeona hiyo habari,inatisha,ila hao ndio wapiga kura wa magamba waache wataisoma namba.rais na waziri wa elimu ndio kwao
   
 8. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Kama hali ya shule ile ipo vile na ni hapo bagamoyo maili 30 toka dar, jiulize wale walioko kibondo, muleba na songea shule zao zikoje? Then Makufuri na yule Wa-hasira wanatamba kuwa wamefanya makubwa. Yani karne ya 21 mtu anashea jengo na mbuzi? Lile darasa kiukweli hata mbuzi wangu hawakai kwenye jengo la miti kama lile, jamani mie ningekuwa chama tawala nisingejaribu kufanya mkutano wa hadhara na kubwatuka kama mzee bingwa wa-hasira! That is a shame, leo unaongea kujenga fly overs wakati wanafunzi wanakaa jengo la miti? Mbavu za mbwa? Hebu kahawa-mbwa jaribu kufanya mageuzi hiyo wizara yako, tena kule ni kwako bagamoyo! Naona aibu kujiita Mtanzania. Sijui lini nitatembea kifua mbele kujisifia utanzania wangu.
   
 9. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwenye "red" Duh, hivi hakuna neno la kiswahili linalomanisha "miles"
   
 10. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Bwana mkubwa, katika yote hapo umekiona hicho tu? anyway 'miles' kwa kiswahili ni 'maili'. Happy now? Karibu tena.
   
 11. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hiyo ndiyo Tanzania imara ya chama cha mapinduzi.Kelele nyingi lakini kwenye utekelezaji sifuri.Hawa jamaa wananiudhi na kunikera kila niwaonapo.MWALIMU NYERERE alitaka angalau usawa katika huduma za jamii,na alijaribu japokuwa hakuuza rasilimali nyingi kama hawa waliojivika MAGAMBA.Na huyo kijana mwenye kuropoka hata mbele ya wazee bila kupima ukweli awajibike.NAPE UNAPIGA KELELE SANA,SASA UZA GARI LAKO KISHA UKAJENGE SHULE.We si ndo unajifanya kidume wa kukoroma eti CCM ITATAWALA MILELE.Je hivyo ndo vigezo vya kutawala? Mnaboa sana wanaccm.Taarifa hii imenisikitisha sana.Kesho tukiongea ukweli:Ooh CHADEMA kinachochea chuki kwa wananchi dhidi ya serikali.SASA dawa yenu imechemka M4C itaingia kwa J.K hadi kwa MWANDOSYA nitaifikisha.
   
 12. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Hii kiru haikubaliki kabisa, na inasikitisha sana.
   
 13. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ....namshauri na muanzisha uzi arekebishe hapo, ila sema hata zito naye aliwahi chapia badala ya "kambi" akaandika "kamba"
   
 14. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2012
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bagamoyo iko Mkoa wa Pwani, Pwani ni moja ya mikoa iliyoko kwenye mwambao wa bahari ya Hindi. Mikoa hii wakazi wake wengi ni wa imani ya UAMSHO. Kama Karne hii ya 21 shule iko hivyo tena Bagamoyo anakotoka Bwana Mkubwa, Je miaka 30-50 iliyopita hali ilikuwaje.

  Hapo bado UAMSHO wanatafuta ushahidi ya kwanini hawajashika nyazifa nyingi serikalini? Bado watadai kuwa wanabaguliwa kwa imani yao? Bado wanataka kila kitu kiwe 50/50!

  UAMSHO ni sawa na BOKO HARAMU! Wazalendo TUJIPANGE SAWA SAWA!
   
 15. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Ktk mkutano wao wa juzi(jaza uwanja)hiyo gharama walitumia si bora wangeitumia kujenga hiyo shule?Sababu hakuna cha msingi kilichofanyika ktk ule mkutano zaidi ya posho na blah blah za kutosha pmj na kuwaita uamsho ni majambazi pia hawana tofauti na boko haram.
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  hatua gani tuchukue kama watanzania?maana kuna chama tangu kimetawala tangu uhuru mpaka leo hata darasa la shule tabu!maoni yako mkuu
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu tatizo ni kwamba uzi kama huu ukiwekwa kwenye education hamtakwenda kuuchangia!!

  Hiki ni kipindi cha siasa kwa watanzania.... Hapa ndo penyewe!!
   
 18. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huko hata M4C haiwezi kuwakomboa...huko wenyewe ngoma na ngoma wenyewe...
   
 19. F

  Froida JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ungewaona walivyokuwa wakitamba Jumamosi ungedhani darasa kama lile huwezi kuliona kamwe,wakajenge basi hiyo shule
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,333
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nimeiona habari hii ITV kiukweli hali ya shule hiyo sio inatia aibu bali ni ya kuhuzunisha na kusikitisha!.

  Mjue hali kama hiyo ipo maeneo mengi tena hapo unaweza ukakuta ndio afadhali maana japo darasa la miti lipo na walimu 2!. Kuna maeneo hakuna mwalimu kabisa, na watoto wanasomea chini ya mti!.

  Hii ndio Tanzania yetu na mafanikio ya miaka 50 ya uhuru wetu tena ujinga ni moja ya maadui wetu watatu pamoja na umasikini na maradhi!.

  Tukiendelea hivi hivi, watoto wetu na watoto wa watoto wetu, watasherehekea miaka 100 ya taifa hili kwa hali hiyo hiyo!.
   
Loading...