Shule sita nchini kufundisha Kichina

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeteua shule sita za sekondari nchini kuingia katika mpango maalumu wa wanafunzi wake kufundishwa somo la lugha ya Kichina kuanzia mwaka huu.

Kutokana na uamuzi huo, walimu 12 kutoka China wamekamilisha utaratibu wa mpango kazi wa namna ya ufundishaji wa somo hilo kwa shule zilizoteuliwa mara zitakapofunguliwa rasmi mwezi huu.

Ofisa Elimu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Salum Salum, alitaja shule zilizoingizwa kwenye mpango huo katika awamu ya kwanza ni Benjamin Mkapa na Chang’ombe (Dar es Salaam), Msalato na Dodoma (Dodoma), Morogoro na Kilakala za mkoani Morogoro.

Salum alitoa taarifa hiyo juzi wakati akifungua mafunzo ya kazi na mipango mikakati iliyoandaliwa na Taasisi ya China inayojihusisha na lugha ya Kichina kwa walimu wake walioteuliwa kufundisha somo la lugha ya kichina katika shule hizo.

Alisema kabla ya kufunguliwa kwa shule, viongozi wa China wamekutana kwa siku mbili mjini Morogoro kufanya mafunzo ya kazi ya kujiandaa kuingia darasani baada ya shule kufunguliwa.

“Mafunzo kazini ni ya kujiandaa na kupeana mikakati na nini kifanyike kabla ya shule kufunguliwa ili kuingia madarasani kufundisha wanafunzi wa kitanzania lugha ya kichina,” alisema Ofisa Elimu Mkuu.

Alisema wanafunzi watatahiniwa somo hilo la lugha ya kichina katika mitihani yao na watakapohitimu watahesabiwa alama za ufaulu sawa na yalivyo masomo mengine yanayofundishwa katika shule za sekondari kama ilivyo kwa Kifaransa na Kijerumani.

Alisema wizara inaona ni njia nzuri kwa vijana wa Kitanzania kuwa na lugha ya mawasiliano katika kuwasaidia kujifunza zaidi na kutumia fursa zitakazopatikana China ikiwemo kujiendeleza na elimu ya juu zaidi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya China ya lugha ya kichina, Ambar Zheng, kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alisema walimu 12 wa China wameshapatiwa mafunzo ya namna ya kufundisha somo hilo kwenye shule husika.

Alisema kila shule ya sekondari iliyoteuliwa katika mikoa hiyo ya Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro, zitapangiwa walimu wawili kila moja kwa ajili ya kufundisha somo hilo kuanzia mwaka wa masomo unaoanza mwezi huu.

Alipongeza ushirikiano mzuri uliooneshwa kati ya Serikali ya Tanzania na China na wizara husika kuwezesha kuanzishwa kwa somo hilo katika baadhi ya shule za sekondari nchini. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro, Profesa Hamza Njozi alipongeza Serikali ya China kwa kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali, ikiwemo elimu ya vyuo vikuu.
 
Dah! Tanzania sijui tuna laan gani! kiingereza chenyewe hatujui, kiswalihi ndio usisema watu badala ya kuandika 'kura' wanasema 'kula'. Kifaransa sijui kilifia wapi, then leo tunakuja na kichina! then what?......................!!! kweli hapa kazi tu
 
Hivi itakuwa kwa tija ya nani???watoto wa hawa waChina wanaokuja kufanya kazi tunazoweza kuzifanya hapa Tz au waTz wanaotaka kwenda kufanya uchuuzi China au ????
 
Nchi haiishi vituko hii,hili si hitaji la waTZ kwa sasa,mbona viongozi wanakuwa malimbukeni hivi.
Kiswahili&kiingereza vitiliwe mkazo, si vinginevyo!
 
Ukiitwa mtanzania anza kujilaumu kwa maana English hatujui kiswahili mpaka tunawekewa penati Sasa kichina tutakiweza kweli. Serikali fikirieni Mara ya pili mnaweza kuwa mlikosea kufikiri kwa Mara ya kwanza. Tusidanganyike na ubia tukasahau uwezo wetu WA kielimu
 
Bora wangefundisha KIKWERE ili kumuenzi rais wetu msitaafu kwa kuliingiza Taifa kwenye mkenge...
 
Ukiitwa mtanzania anza kujilaumu kwa maana English hatujui kiswahili mpaka tunawekewa penati Sasa kichina tutakiweza kweli. Serikali fikirieni Mara ya pili mnaweza kuwa mlikosea kufikiri kwa Mara ya kwanza. Tusidanganyike na ubia tukasahau uwezo wetu WA kielimu

Tatizo kuna watanzania wamelala!!! Wawekezaji wakubwa sasa hivi wanaoibukia duniani ni wachina.Ukiwa na ujuzi na ukawa unajua kichina ni rahisi kuajiriwa na wawekezaji wa kichina popote duniani.Nakumbuka kuna kipindi kampuni moja ya mafuta ilikuwa ikitaka marketing manager mtanzania awe na digrii moja ya marketing lakini awe anajua kifaransa.Hakupatikana walipatikana watanzania wana hadi PHD za marketing lakini hawajui kifaransa hadi wakaomba kibali kuajiri raia wa nje na raia waliyempata ni mkenya ambaye alikuwa na digrii ya marketing na alijisomea mwenyewe kwa kujilipia kusoma kifaransa hadi akakimudu barabara.Walipoulizwa kwa nini wanataka mtu ajuaye kifaransa wakasema wanataka asimamie soko lao la mafuta lililoko kongo na burundi ambako wanatumia kifaransa.

Taabu ya baadhi ya watanzania hasa UKAWA huwa ni kubeza tu kila kinachofanywa na serikali!

Watoto wanatakiwa waandaliwe kimataifa ili washindane ajira kimataifa ziwe za kichina,kifaransa,kiingereza n.k Naipongeza serikali ya Magufuli.

Kichina muda si mrefu kitakuwa moja kati ya lugha kubwa mno duniani kutokana na influence yake kwa dunia.
 
Watu kama wewe ndio mnafanya uchumi wa nchi hii uzidi kudidimia, unakaa unamshawishi mtu aendelee kujifunza lugha bila mpangilio eti ili akaajiriwe huo ni ugonjwa wa upungufu wa kufikiri kichwani.

Kuna mambo mangapi mazuri China wanayafanya kwanini tusijifunze kwanza hayo kisha lugha iwe ya mwisho? Kwanini serikali isiende kuchukua walimu wa ufundi china waje kufundisha vijana jinsi ya kutengeza simu, radio nk

Huo mchezo unazidi kuwafanya vijana wafikirie kuajiriwa kama wewe, hawa vijana wajengewe mentality ya kuajiajiri nasio kuajiriwa halafu mwajiri mwenyewe mchina. Unawafaham wachina wewe??? Ni waonezi wakubwa kwa wafanyakazi wa kitanzania

BADILIKA
 
" Najiuliza hili swali,
Sipati jibu kamili,
Wanachoongea wabongo,
Kimombo kiswahili,
Tuongeze basi kichina,
Tuzidi pata jina,,,,,,,,,,"
Yametimia ya ule wimbo wa bongo fleva
^^
 
Kiingereza kimetushinda sasa tunaleta kichina...?

Hivi hii Elimu yetu mbona kila warizi akija anakuja na lake?
 
Kwanini serikali isiende kuchukua walimu wa ufundi china waje kufundisha vijana jinsi ya kutengeza simu, radio nk
Walimu wa ufundi china wamesomea ufundi kwa lugha ya kichina na wanafundisha vyuoni kwa lugha ya kichina.Ukiwaleta hao walimu hapa hawataweza kufundisha sababu hawatumii kiingereza ndio maana serikali inaleta walimu wa kichina kwanza waje wafundishe watoto wengi kichina kwanza kisha ukiwaleta hao walimu wa ufundi wa kichina inakuwa rahisi kufundisha vyuo VETA .

Vyuo vingi ukienda china lazima usome lugha kwanza ndio uanze kozi.Mkakati wa serikali uko sahihi unawarahisishia wanafunzi hata wakiamua kwenda zao kusoma china hawahitaji kukaa mwaka kusoma kichina na kulipia pesa kibao watakuwa tayari wamepata kujua hapa hapa Tanzania tena kwa gharama nafuu ya kusomeshwa bure na serikali.China kuna watanzania wengi wanasoma kule
 
hili kuwa dhaifu hiliyopita sasa hii ni yakukurupuka. magu acha kutuangusha kwakifupi kichina atukitaki
 
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeteua shule sita za sekondari nchini kuingia katika mpango maalumu wa wanafunzi wake kufundishwa somo la lugha ya Kichina kuanzia mwaka huu.

Kutokana na uamuzi huo, walimu 12 kutoka China wamekamilisha utaratibu wa mpango kazi wa namna ya ufundishaji wa somo hilo kwa shule zilizoteuliwa mara zitakapofunguliwa rasmi mwezi huu.

Ofisa Elimu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Salum Salum, alitaja shule zilizoingizwa kwenye mpango huo katika awamu ya kwanza ni Benjamin Mkapa na Chang’ombe (Dar es Salaam), Msalato na Dodoma (Dodoma), Morogoro na Kilakala za mkoani Morogoro.

Salum alitoa taarifa hiyo juzi wakati akifungua mafunzo ya kazi na mipango mikakati iliyoandaliwa na Taasisi ya China inayojihusisha na lugha ya Kichina kwa walimu wake walioteuliwa kufundisha somo la lugha ya kichina katika shule hizo.

Alisema kabla ya kufunguliwa kwa shule, viongozi wa China wamekutana kwa siku mbili mjini Morogoro kufanya mafunzo ya kazi ya kujiandaa kuingia darasani baada ya shule kufunguliwa.

“Mafunzo kazini ni ya kujiandaa na kupeana mikakati na nini kifanyike kabla ya shule kufunguliwa ili kuingia madarasani kufundisha wanafunzi wa kitanzania lugha ya kichina,” alisema Ofisa Elimu Mkuu.

Alisema wanafunzi watatahiniwa somo hilo la lugha ya kichina katika mitihani yao na watakapohitimu watahesabiwa alama za ufaulu sawa na yalivyo masomo mengine yanayofundishwa katika shule za sekondari kama ilivyo kwa Kifaransa na Kijerumani.

Alisema wizara inaona ni njia nzuri kwa vijana wa Kitanzania kuwa na lugha ya mawasiliano katika kuwasaidia kujifunza zaidi na kutumia fursa zitakazopatikana China ikiwemo kujiendeleza na elimu ya juu zaidi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya China ya lugha ya kichina, Ambar Zheng, kutoka katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), alisema walimu 12 wa China wameshapatiwa mafunzo ya namna ya kufundisha somo hilo kwenye shule husika.

Alisema kila shule ya sekondari iliyoteuliwa katika mikoa hiyo ya Dodoma, Dar es Salaam na Morogoro, zitapangiwa walimu wawili kila moja kwa ajili ya kufundisha somo hilo kuanzia mwaka wa masomo unaoanza mwezi huu.

Alipongeza ushirikiano mzuri uliooneshwa kati ya Serikali ya Tanzania na China na wizara husika kuwezesha kuanzishwa kwa somo hilo katika baadhi ya shule za sekondari nchini. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro, Profesa Hamza Njozi alipongeza Serikali ya China kwa kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali, ikiwemo elimu ya vyuo vikuu.
Ningekuwa mimi ningeimarisha zaidi somo la kiingereza. Huwezi kupinga kwamba lugha namba moja duniani ni English. Hata ukienda huko China kwenyewe wanagombania madarasa ya kiingereza. Ukikutana na mfaransa, mGerman, Mreno, MuItaliano wanajua sana lugha zao lakini utashangaa hata English wanajua. English ni lugha ya dunia ambayo ukiijua ina fursa nyingi mno. Leo hii Mtanzania ukitaka uombe scholarship Marekani na UK bila cheti cha lugha (TOEFL) hupokelewi wakati nchi za Africa magharibi wao cheti cha form four yao tu kinatosha. Tunakosa scholarship mamia wanabaki kwenda watoto wa vigogo tu waliosoma English Mediu. Leo mnatuletea kichina sisi wana wa maskini inauma.
 
KINGEREZA NI JANGA,KICHINA JE ?
JANGA JIPYA.
Kwanza kabisa niisifu serikali kwa
kuona umuhimu wa lugha ya kichina
ambayo itaweza kusaidia kuongeza
upinzani na ushindani ktk biashara ya
kiuchumi na taifa hilo.
lugha ya kingereza ni tatizi kubwa ktk
shule zetu na ajabu ni kwamba
mwanafunzi anaweza kukaa darasani
miaka minne na kumaliza bila ya
kuifahamu lugha hiyo na hilo nalo ni
tatizo la kitaifa.
na sijui ni kwanini mpaja sasa tatizo
halitatuliwi.
inawezekana basi hata walimu
wakawa na tatizo la ufundishaji wa
lugha hii ana mtaala siyo mzuri na
walimu hawana mbinu ya kuutumia.
kingereza kinachangia kwa asilimia
kubwa wanafunzi kushindwa ktk
kufaulu kwa kuwa hawakiekewi
vyema
leo lugha ya kichina nayo imeingizwa
ktk baadhi ya shule chache,je
kingereza kinafahamika ?
wanafunzi wanakielewa ?
ni vyema serikali iboreshe kingereza
kwanza na kianzie ktk shule za
msingi tena kiboreshwe.
mbona kuna walimu wazuri
wanafahamu lugha hii na wapo mtaani
tu bila ya kupewa nafasi serikalini.
serikali watazameni watu hao wenye
uwezo wa kufundisha japokuwa
hawajapata kusomea ualimu lakini
uwezo wao ni zaidi ya hao walimu.
ni vyema kutazama uwezo kwanza
kabla ya vyeti ili kuliokoa taifa.
tunahitaji mabadiliko hata kama ni
tofauti na mwendo wa dunia, ilimradu
nchi ipate kuendelea.
lazima tuwe na njia tofauti ili kufikia
maendeleo tunayoyataka.
TUWEKE KICHINA KANDO NA
TUBORESHE KINGEREZA.
ila serikalu ilete walimu wa lugha ya
kichina kwa ajili ya kuifundisha ktk
vyuo vidogo,vya kati na vikuu.
TULIOKOE TAIFA.
 
Ningekuwa mimi ningeimarisha zaidi somo la kiingereza. Huwezi kupinga kwamba lugha namba moja duniani ni English .
Swala si kwamba hiyo lugha ni namba moja au ngapi swala ni kuwa hiyo lugha ina manufaa kiuchumi kwa watu wengi au la.KWA SASA FURSA NYINGI ZA ELIMU NA KIUCHUMI kwa watanzania zinapatikana zaidi china kuliko kwenye nchi zingine zinazoongea kwa ufasaha lugha ya kiingereza.Ni rahisi watanzania wengi kwenda kufanya biashara China kuliko Uingereza au marekani.Vijana wengi na wazazi wengi wanaweza somesha watoto wao na kuweza kulipia kule ada kuliko nchi hizo za kiingereza.
 
The black person's stupidity must be liberated from the mind.
Hivi hamjui kama kuna watu nchini china hawana ajira?,mara ngapi mmewaona wachina hapa kwetu wakijishughulisha na kazi ndogondogo ambazo kwa kawaida ni za mtu wa maisha ya chini?hapo mijitu kutokana na uvivu wa kutafakari imeshindwa kubaini hapo mchina kawatengenezea ajira watu wake.
Hilo somo naomba liwe la hiari,maana itakuwa ajabu kama unasoma lugha ya kwako tu na haikusaidii halafu unataka ikakusaidie lugha ngeni tena eti ukiwa ugenini.
 
Hapo ni kama wanabeza elimu, mtoto anatakiwa afundishwe akiwa shule ya msingi tena sio lugha moja bali wapangiwe wa kusomea lugha tofauti kwani duniani kuna ushindani.

Mataifa mengine wanafundisha lugha ili kupeleka watu wao kupeleleza halafu wengine wanabeza humu.

Uingereza watoto wadogo wanaongea kichina wengine kijapan na hata kiarabu,kijerumani na kifaransa na ni lazima kila mtoto ajue lugha moja zaidi ya kingereza
 
Back
Top Bottom