YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,900
- 52,036
Nenda china kuna watanzania wengi kuliko hao wachina unawaona Tanzania wako kule wakifanya biashara ndogo ndogo za wachina wa hali ya chini pia.Huku Tanzania wamekosa cha kufanya lakini wakaenda china wakapata cha kufanya na kuna wachina hawaoni cha kufanya kule wakija huku wanaona cha kufanya ambacho yule aliyeenda china hakukiona!mara ngapi mmewaona wachina hapa kwetu wakijishughulisha na kazi ndogondogo ambazo kwa kawaida ni za mtu wa maisha ya chini?i.
Wewe ukipanda ndege kwenda marekani au uingereza kutafuta maisha usishangae angani kupishana na ndege zimejaa wamarekani na waingereza wanakuja kutafuta maisha Tanzania!!! Hilo sio ajabu