Shule Nzuri ya Boarding kwa mtoto wa miaka 3 - 4

Mtoto wa miaka 3....kweli kuna watu hawana mapenzi na watoto wao...ulizaa ili nani akulelee..m sure huyo mtoto akitoka huko atakua ni nunda balaa na wala hatokujali km mzazi
 
Jamani msimlaumu mleta mada nafikiri yamemkuta kama mm, mfano mzuri ni mimi mwenyewe nina mtoto wa miaka 4 na kazi zangu ni za kusafiri kwenye ships ninaweza kukaa hata mwaka ndio nirudi Tz, mwaka jana nilimuachia mdogo wangu mtoto amlee ikiwemo ampeleke shule na pesa za matumizi ya mtoto nilimuachia 3million na kadi ya health insurance juu kwa matumizi ya mwaka mmoja
Sasa mdogo wangu huyu alichokifanya ni madudu pesa niliyomuachia kaenda kununulia kiwanja na mtoto hajampeleka shule, kula mtoto akila asubuhi mpk jioni kuumwa kila siku kwa ukosefu wa lishe, can u imagine vile mzazi ninavyojisikia inauma sana, baada ya kupata taarifa ya mazingira ya mwanangu ilinibidi nirudi bongo kumchukua na nilipomuona nililia kama nimefiwa na ss niko nae hapa but hasomi kutwa mama yake niko kwenye meli
Nafikiria hata mimi nimpeleke boarding school, kwa hiyo tusitoe maneno ya kumlaumu mleta mada hujui nini kimemsibu.
 
Nimetambua kwa nini wanafunzi wengi hurudia mtihani. Mleta mada anaomba kufahamishwa shule nzuri ya boarding na wala hajaomba ushauri ampeleke binti yake boarding au la. Tumtajia shule kwanza na ushauri ufuate chini ya jibu sahihi.

jaribu: Angelico Lipan School, hii ni ya masista wa Franciscan Sisters of the Lord (Osterbay kuelekea Mbauda). Ila sidhani kama wanapokea boarding kwa wanafunzi wa shule ya awali

we mwenyewe bado uko op 2 yeye kakwambia zilizoko
Kilimanjaro au Arusha alafu wewe unamtajia za Dar.!?
 
Sasa na wewe umemsaidia nini? Mwenzio anataka shule ya bweni afu unamtajia shule ambayo huna uhakika kama ni ya bweni kwa wanafunzi wa chekechea. Hata wewe pia unahitaji kurudia mtihani.

Watanzania ndivyo tulivyo.
 
Mkuu ulieleta hii thread unahitaji msaada wa kiroho, inabid uwekewe mikono maana najua hilo wazo sio wazo lako bali ni pepo mkuu wa anga.´

Uponywe kwa jina la yesu.
 
we mwenyewe bado uko op 2 yeye kakwambia zilizoko
Kilimanjaro au Arusha alafu wewe unamtajia za Dar.!?

Mkuu, Mbauda haiko Dsm. Hilo neno Oysterbay hata kwetu Kiomboi tunalitumia sana.
 
Miaka minne ni mdogo sana yaani bora mtoto aende boarding akiwa form one ila primary school na chekechea ni ngumu sana katika malezi ya mtoto hatalelewa unavyotaka wewe na ni rahisi sana mtoto ku adopt tabia za watoto wengine.

Ila kuna shule ipo moshi mjini ni ya. Walokole inaitwa foundation of hope wanapokea kuanzia umri huo.
Ila bora utafute. Nanny mtu mzima akae na mwanao atlist kuliko boarding school

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Na vimchezo vya kugusagusana visichana vinaanzia huko huko hakuna wa kumuonya as mzazi jaribu uone
 
Mkuu,
Watu wengi tumeangalia implication ya mchakato mzima, sio swali lake, maana tunaishi katika jamii na tunajua kitakachofuata!...cha msingi hapa ni kudiscourage kabisa suala la kumpeleka mtoto kwenye shule za hivyo, na pia hatuko kwenye mtihani hapa!

Pili, suggestion yako kuhusu shule ya Fransiscan Sisters/Angelico Lipani, inaonyesha hujui kabisa kuhusu shule hiyo na wala hujaitembelea lkatika siku za karibuni!
Wanangu nilikuwa nimewapeleka shule hiyo lakini nilienda kuwahamisha wote baada ya sababu zifuatazo:

1. Darasa moja linakuwa na watoto 50, na ukitaka mwanao afuatiliwe ni lazima uongeze kitu kwa kila mwalimu wa somo, apart from ada!

2. Kama wewe kabila lako si MMBULU imekula kwako, maana asilimia 68 ya walimu wa pale ni Wambulu kutokana na fact kwamba Mwalimu Mkuu alikuwa Sista wa kabila hilo, na aliajiri walimu almost wote wa kabila lake!. Ukitaka mtoto wako afuatiliwe vema darasani lazima uongee kilugha na Mwalimu wake, tofauti utaishia kupoteza hela.

3. Huyo Sista wa Kimbulu aliivuruga shule kabisa mwaka jana baada ya kukomba 70m kwenye account ya shule na kutoroka na kijana mdogo wa kiume na kuelekea kusikojulikana!
Shule ilikosa mwelekea na harakaharaka Wajanja tukaondoa watoto wetu!

Narudia tena, Mleta mada tafadhali usithubutu kupeleka mtoto wako boarding kwa sababu yoyote ile!

Usemayo kuhusu Angelico Lipan kuisiana na ukabila kwa mwaka jana rudi nyuma ilikuwa kwelie. Kwa mwaka huu mambo yamebadilika na shule ina kamati ya shule na mimi ni makamu mwenyekiti; itembelee sasa hivi kujiridhisha
 
we mwenyewe bado uko op 2 yeye kakwambia zilizoko
Kilimanjaro au Arusha alafu wewe unamtajia za Dar.!?

Angelico Lipan school iko Arusha, eneo la mbele ya Oysterbay kama unaelekea Mbauda. Al-shabaab Oysterbay is Dar tu kama ilivyo "majengo"

Sasa na wewe umemsaidia nini? Mwenzio anataka shule ya bweni afu unamtajia shule ambayo huna uhakika kama ni ya bweni kwa wanafunzi wa chekechea. Hata wewe pia unahitaji kurudia mtihani.

Watanzania ndivyo tulivyo.
Asprin pole, shule niliyomtajia ina bweni kwa wasichana wa shule ya msingi. Bweni linawalenga zaidi watoto wa mitaani
 
Last edited by a moderator:
Acheni uvivu na ubize usiokuwa na kichwa wala miguu, mtoto uzae kwa starehe zako uende ukawatese waalimu kwa malezi, mtoto anapaswa awe kwenye uangalizi na malezi ya wazazi mpaka atakapoweza kumudu kupambana na changamoto za maisha. Maadili ya vijana wetu yanaporomoka kwa kuendekeza wazazi wa aina hii, mimi nilisoma katika hizo boarding school nikiwa Advanced level na kwa kweli watoto wadogo wanaharibika sana, wanajifunza kuvuta bangi, ulevi, uhuni kwa kujiunga na makundi hatarishi wawapo mashuleni ambako ni mbali na hao wazazi, nyinyi mnaona raha tuu kuhamisha majukumu yenu ya ulezi kwa waalimu ila utakapogundua na kujua kuwa toto lako limekuwa changu, teja, jambazi nadhani ndio utajua athari ya hiki unachotaka kukifanya.
 
Usemayo kuhusu Angelico Lipan kuisiana na ukabila kwa mwaka jana rudi nyuma ilikuwa kwelie. Kwa mwaka huu mambo yamebadilika na shule ina kamati ya shule na mimi ni makamu mwenyekiti; itembelee sasa hivi kujiridhisha
Nashukuru kuwa umeacknowledge yote niliyosema, na kwamba mnaboresha ili at least Umbulu uondoke kwenye hiyo shule!...Otherwise majengo na hali ya mazingira ya shule ya Angeliko ni modern sana na panavutia sana kwa macho!
Hongera kwa nafasi yako hiyo Mkuu, nadhani nikibahatika kuzaa tena nitamleta hapo!
Vipi yule Sister alikuja kupatikana?
 
mleta mada rudi huku uje uhitimishe mada yako watu wameshakomenti vya kutosha.
 
Wana JF, natafuta shule nzuri ya English medium (Boarding school) zilizoko mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kwa ajili ya mtoto wangu wa kike mwenye umri wa miaka 3 na mwakani atatimiza miaka 4. Hivyo naomba msaada wenu ili niweze kupata shule hiyo kwa ajili ya mwanangu. Mwenye kujua shule nzuri (nasisitiza shule nzuri) hasa zilizoko mikoa ya Kilimanjaro na Arusha naomba anitajie ili niweze kumpeleka mwanangu. Asanteni sana.

Alafu watu wa kaskazini nimegundua ndo mnapenda sana kuwapeleka watoto wa dogo shule za boarding, kwanin lakini?
 
Mleta Mada .... Ukuta.

Mazuri ya JF ni kuweza kupata ushauri, tena wa maana bure kabisa! Utashangaa manufaa yake ukiusikiliza na kutekeleza. Naona wengi wanakushauri uachane na wazo la kumpeleka malaika huyo boarding.

Au ushauri wetu umegonga ukuta?
 
mtoto bado mdogo mkuu. Unamkosesha mapenzi ya wazaz wake. Dogo atakosa hata hug za mama yake na badala yake ataanza kujifunika mishuka. Kama kakuchosha mvumilie kidogo angalau akuekue ndo ukamuwekeze huko unapopaita boarding. (usimind kwa lugha ya kashfa. Najua unampenda mwanao.)
 
Mkuu,
Watu wengi tumeangalia implication ya mchakato mzima, sio swali lake, maana tunaishi katika jamii na tunajua kitakachofuata!...cha msingi hapa ni kudiscourage kabisa suala la kumpeleka mtoto kwenye shule za hivyo, na pia hatuko kwenye mtihani hapa!

Pili, suggestion yako kuhusu shule ya Fransiscan Sisters/Angelico Lipani, inaonyesha hujui kabisa kuhusu shule hiyo na wala hujaitembelea lkatika siku za karibuni!
Wanangu nilikuwa nimewapeleka shule hiyo lakini nilienda kuwahamisha wote baada ya sababu zifuatazo:

1. Darasa moja linakuwa na watoto 50, na ukitaka mwanao afuatiliwe ni lazima uongeze kitu kwa kila mwalimu wa somo, apart from ada!

2. Kama wewe kabila lako si MMBULU imekula kwako, maana asilimia 68 ya walimu wa pale ni Wambulu kutokana na fact kwamba Mwalimu Mkuu alikuwa Sista wa kabila hilo, na aliajiri walimu almost wote wa kabila lake!. Ukitaka mtoto wako afuatiliwe vema darasani lazima uongee kilugha na Mwalimu wake, tofauti utaishia kupoteza hela.

3. Huyo Sista wa Kimbulu aliivuruga shule kabisa mwaka jana baada ya kukomba 70m kwenye account ya shule na kutoroka na kijana mdogo wa kiume na kuelekea kusikojulikana!
Shule ilikosa mwelekea na harakaharaka Wajanja tukaondoa watoto wetu!

Narudia tena, Mleta mada tafadhali usithubutu kupeleka mtoto wako boarding kwa sababu yoyote ile!
Duuh afadhali nimesoma hii nilikuwa january nimpeleke mwanangu pale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana JF, natafuta shule nzuri ya English medium (Boarding school) zilizoko mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kwa ajili ya mtoto wangu wa kike mwenye umri wa miaka 3 na mwakani atatimiza miaka 4. Hivyo naomba msaada wenu ili niweze kupata shule hiyo kwa ajili ya mwanangu. Mwenye kujua shule nzuri (nasisitiza shule nzuri) hasa zilizoko mikoa ya Kilimanjaro na Arusha naomba anitajie ili niweze kumpeleka mwanangu. Asanteni sana.
Ndugu umechoka kukaa na mwanao? Kwa umri huo sikushauri upeleke mtoto huko, ndo baadaye unapata watoto mashoga/ anakuwa na tabia za ajabu unakuja tena kuomba ushauri. Mlee mwanao umfundishe tabia njema maadili yaliyotukuka utafurahi
 
Jamani msimlaumu mleta mada nafikiri yamemkuta kama mm, mfano mzuri ni mimi mwenyewe nina mtoto wa miaka 4 na kazi zangu ni za kusafiri kwenye ships ninaweza kukaa hata mwaka ndio nirudi Tz, mwaka jana nilimuachia mdogo wangu mtoto amlee ikiwemo ampeleke shule na pesa za matumizi ya mtoto nilimuachia 3million na kadi ya health insurance juu kwa matumizi ya mwaka mmoja
Sasa mdogo wangu huyu alichokifanya ni madudu pesa niliyomuachia kaenda kununulia kiwanja na mtoto hajampeleka shule, kula mtoto akila asubuhi mpk jioni kuumwa kila siku kwa ukosefu wa lishe, can u imagine vile mzazi ninavyojisikia inauma sana, baada ya kupata taarifa ya mazingira ya mwanangu ilinibidi nirudi bongo kumchukua na nilipomuona nililia kama nimefiwa na ss niko nae hapa but hasomi kutwa mama yake niko kwenye meli
Nafikiria hata mimi nimpeleke boarding school, kwa hiyo tusitoe maneno ya kumlaumu mleta mada hujui nini kimemsibu.
Huna wazazi wakamlea huyo mtoto? Usifikiri kuwa huko boarding kuna malezi mazuri tena walimu wenyewe ni vijana wadogo hawana hata huruma na mapenzi na watoto kuwa makini usije ukajuta
 
Back
Top Bottom