Shule Nzuri ya Boarding kwa mtoto wa miaka 3 - 4

Shule Nzuri ya Boarding kwa mtoto wa miaka 3 - 4

Wana JF, natafuta shule nzuri ya English medium (Boarding school) zilizoko mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kwa ajili ya mtoto wangu wa kike mwenye umri wa miaka 3 na mwakani atatimiza miaka 4. Hivyo naomba msaada wenu ili niweze kupata shule hiyo kwa ajili ya mwanangu. Mwenye kujua shule nzuri (nasisitiza shule nzuri) hasa zilizoko mikoa ya Kilimanjaro na Arusha naomba anitajie ili niweze kumpeleka mwanangu. Asanteni sana.
Nafkir hili linahitaji kabisa kutungiwa hata sheria
huyu mtoto bado ni mdogo sana kukaa boarding mlee mtoto angalau akue kue kidogo mkuuh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitasahau nilipompeleka mwanangu boarding akiwa darasa la tatu.Nilitafuta shule yenye gharama kubwa nikijua ndo huduma zitakua bora kumbe ilikuwa vise versa.One year later nilimtoa boarding nikamhamishia shule nyingine ya kutwa.Niliapa sitampeleka mwanangu yeyote boarding hadi amalize darasa la saba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom