YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,003
Kuna madai kuwa msomi anatakiwa awe anamudu kiingereza.Tanzania kuna waongea kiingereza vizuri ambao fani zao walizosomea hawazimudu ni mzigo na majipu yanayotakiwa kutumbuliwa.
Unaposoma somo lengo ni kulijua hilo somo sio Lugha ndio maana kuna makenika wazuri wa magari ambao wanajua kila chombo kilichomo kwenye gari kwa kiingereza lakini hawajui kuongea kiingereza fasaha.Ukitaka kujua kiingereza soma somo linaloitwa kiingereza hadi chuo kikuu.
Wako madaktari wazuri kibao wanajua aina za magonjwa na dawa zake lakini kiingereza hawajui kuongea kwa ufasaha.Lengo la kusoma fani fulani sio kujua lugha ni kuijua kwa undani fani husika .Ndio maana mtanzania akienda kusoma udaktari china aweza rudi anaujua vizuri udaktari lakini kichina hakijui kwa ufasaha.Taabu ya watanzania wanafikiri kusoma fani ni kusomea lugha!!!!!!!!!! Wanawaza ukiona injinia basi yeye kasomea lugha ya kiingereza.FANI ni zaidi ya Lugha!!!!
Shule na vyuo vyetu vijitahidi kufundisha fani watu watoke mahiri kwenye fani zao sio mahiri kwenye kiingereza!!!!!!
Tanzania ili iendelee inahitaji watu mahiri kwenye fani zao walizosomea sio waongea kiingereza kutwa.