Wakuu.. hope ni salama..
Nimejaribu kuangalia baadhi ya vyuo marekani kwa ajili ya kufanyia M.Sc. CS ambavyo vitakuwa affordable kwa ajili ya kujilipia mwenyewe, so far nimeona kimoja ambacho ni some how affordable kuwa admitted kwa sababu wanatoa loan. Kinaitwa Maharishi University of Management.
Utaratibu wao unatakiwa uwalipe ada kati ya dola 5000 - 7500 (ada yao full ni $37,339) kulingana na passmark zako za Java, mtihani unafanya online. Na wanataka uwe na dola 2200 za kutumia wewe pamoja na pesa yako ya ndege labda dola 1300. Kama ada let say utalipa dola 6000 na pesa ya matumizi na ndege jumla itakuwa dola 9500. ambayo ni kama mil. 20 za kibongo.
Then unakaa kampusi semista mbili, baada ya hapo wanakutafutia office unafaya internship for two years. Hapo ndo unakuwa unarudisha pesa waliyokukopesha.
Sasa mi nataka nichukue mkopo wa mshahara hiyo mil. 15 (5 ntaongezea) ilipwe kwa five years niache kazi nisepe US. makato yanaweza kuwa laki 3.3 a month, nilitaka wazoefu wanisaidie, je nitaweza kuafford kulipa kwa hiyo miezi tisa ya mwanzo, ambayo nitakuwa shule, nitaweza kupata kazi za boX na shule?
Na kama kuna muungwana anajua chuo chenye mpango bora nafuu zaidi anijulishe?
Usinishauri scholarship, nimevurugwa nataka by january intake nisepe.
With thanks