Shule binafsi Dodoma yawataka wazazi kuchangia ununuzi wa basi la shule

Tuti Tuti

Member
Apr 15, 2015
52
5
Ni ajabu na kweli kuna shule ya ST. Ignatius iliyopo hapa Dodoma imewataka wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wachangie ununuzi wa basi jipya kwa ajili ya kupeleka watoto shule pamoja na kuwa wamelipwa Ada na nauli ya kuwapeleka na kuwarudisha watoto shule. Hii shule ni ya Taasisi ya kidini lakini Ada zake na huduma zake hazifanani kabisa na huduma wanayotoa.

Pamoja na kuwa serikali imekataza Ada isipandishwe bado wenyewe wanasisitiza lazima wazazi walipe ada waliyopandisha ambayo ni Milioni moja na laki sita na nusu(1,650,000/=) kuanzia mwaka huu , aada iliyokuwepo hapo mwaka jana ni Milioni moja na laki tatu(1,300,000/=) kwa mwaka .Tunaiomba serikali iiangalie sana shule hii maana nayo ni jipu kama majipu mengine.
 
Siku hiyo hiyo nonayopata hiyo taarifa ningemtoa mwanangu.Ni dharau kubwa sana kuletewa taarifa kama hii na usiifanyie chochote
 
Ahaaa Elimu ni ghali au jaribu ujinga uone. Haku hakuna vya bure bure. Au mtoe Mtoto wako kaa naye nyumbani. vinginevyo changia hiyo "School Van" inunuliwe.
 
Huko ndo kwenye Division 1 mnataka nini zaidi? Mpeleke shule za kata ... Elimu bora ni gharama. Unalalamika huku wakati bodi ya shule ipo. Mnakera sana nyie watanzania.
 
utakuwa umemkomoa nani?
So uwekezaji wa shule yako uniambie mimi ndo nigharamikie?Kama umeona shule inahitaji kuwa na gari la kuwasafirisha wateja wako,inakubidi uifanye ww na sio nikuchangie mimi..Umeshawahi kuwachangia wamiliki wa daladala sh.ngapi katika kununua gari mpya?

Kwa swali lako,kuna shule nyingi tu zisizo na huo upuuzi,ataenda huko.
 
Ni ajabu na kweli kuna shule ya ST. Ignatius iliyopo hapa Dodoma imewataka wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wachangie ununuzi wa basi jipya kwa ajili ya kupeleka watoto shule pamoja na kuwa wamelipwa Ada na nauli ya kuwapeleka na kuwarudisha watoto shule. Hii shule ni ya Taasisi ya kidini lakini Ada zake na huduma zake hazifanani kabisa na huduma wanayotoa.

Pamoja na kuwa serikali imekataza Ada isipandishwe bado wenyewe wanasisitiza lazima wazazi walipe ada waliyopandisha ambayo ni Milioni moja na laki sita na nusu(1,650,000/=) kuanzia mwaka huu , aada iliyokuwepo hapo mwaka jana ni Milioni moja na laki tatu(1,300,000/=) kwa mwaka .Tunaiomba serikali iiangalie sana shule hii maana nayo ni jipu kama majipu mengine.
Mpeleke mwanao akasome makulu sekondary ni bure kabisa...hizo st.ni za kina watoto wa makufuli na wenzake huziwezi
 
Si shule hiyo peke yake. Zipo shule binafsi hapa Dar zimechangisha wazazi kujenga ukuta, kupanua au kuongeza madarasa n.k. Uzuri wazazi wa siku hizi si wanawapenda saana watoto wao wasipate taabu. Tunachanga! Lakini hii ni capital investment kwa mwenye shule. Ataongeza idadi ya wanafunzi, kipato kinaongezeka. Aliyefuatilia harusi ya mtoto wa mmiliki wa shule ya Tusiime anajua utamu na matunda ya uwekezaji huo.
 
Ni ajabu na kweli kuna shule ya ST. Ignatius iliyopo hapa Dodoma imewataka wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wachangie ununuzi wa basi jipya kwa ajili ya kupeleka watoto shule pamoja na kuwa wamelipwa Ada na nauli ya kuwapeleka na kuwarudisha watoto shule. Hii shule ni ya Taasisi ya kidini lakini Ada zake na huduma zake hazifanani kabisa na huduma wanayotoa.

Pamoja na kuwa serikali imekataza Ada isipandishwe bado wenyewe wanasisitiza lazima wazazi walipe ada waliyopandisha ambayo ni Milioni moja na laki sita na nusu(1,650,000/=) kuanzia mwaka huu , aada iliyokuwepo hapo mwaka jana ni Milioni moja na laki tatu(1,300,000/=) kwa mwaka .Tunaiomba serikali iiangalie sana shule hii maana nayo ni jipu kama majipu mengine.

Jamani kabla hujaamua kumpeleka mtoto shule ,ni vizuri ukatafuta historia yake kitaaluma.Vinginevyo unakuja kujutia gharama ulizoingia na mwisho wa siku performance ya mtoto na shule yenyewe ni Ziro.

Mfano mzuri ni hizi shule za Dodoma,nyingi ni majina makubwa yaliyokuzwa na uzuri wa majengo lakini ukiingia kwenye takwimu za ufaulu wa kitaifa,ni hovyo kabisa.

Ninachokiona wasomeshaji wengi wa mkoa huu ni wageni kwenye Elimu kiasi kuwa wakiona majengo mazuri wao hapo ndipo kwenye Elimu.

Natoa wito chunguzeni hizo shule kwa kutumia Data za kitaifa,na hapa Dom zipo shule ambazo huwezi kudhania,zina majengo ya kawaida,walimu simple ila wapo juu kuliko zenye majina.Si vizuri kuzitaja majina nisionekane nipo kwenye promo.
 
Ndio hvyo changieni mbona kwenye harusi mnachangia wakati ni uwekezaji wa kuhalalisha uzinzi wa watu wawili kwann kwenye elimu hamchangii wakati inaenda kunufaisha wengi badilikeni
 
Ni ajabu na kweli kuna shule ya ST. Ignatius iliyopo hapa Dodoma imewataka wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wachangie ununuzi wa basi jipya kwa ajili ya kupeleka watoto shule pamoja na kuwa wamelipwa Ada na nauli ya kuwapeleka na kuwarudisha watoto shule. Hii shule ni ya Taasisi ya kidini lakini Ada zake na huduma zake hazifanani kabisa na huduma wanayotoa.

Pamoja na kuwa serikali imekataza Ada isipandishwe bado wenyewe wanasisitiza lazima wazazi walipe ada waliyopandisha ambayo ni Milioni moja na laki sita na nusu(1,650,000/=) kuanzia mwaka huu , aada iliyokuwepo hapo mwaka jana ni Milioni moja na laki tatu(1,300,000/=) kwa mwaka .Tunaiomba serikali iiangalie sana shule hii maana nayo ni jipu kama majipu mengine.

Poleni sana,
Hili suala lipo sana katika hizi shule binafsi na hasa shule zinazojipambanua kama shule za dini. Kwenye mikutano na wazazi salamu za kidini zinatamalaki, kuwaaminisha wazazi kuwa wapo kwenye mkutano uliokatika context ya kiimani. Hii huwa ni hadaa, kwani mazingira halisi ya kibepari na kinyonyaji.
Inakuwaje shule inatoza ada ya shule, inatoza gharama ya usafiri lakini bado inaendelea kuitisha michango ya kununua bus kutoka kwa wazazi?. Je, ni nini matumizi ya pesa ya pesa inayolipwa kama gharama ya usafiri? je, walitumia vigezo gani kupanga hiyo gharama ya usafiri?. Hilo ni moja.

Pili kuhusu upandishwaji wa ada, kwakuwa hii shule ipo Tanzania, ni lazima utendaji kazi wake uzingatie matakwa na Taratibu za Serikali halali ya Tanzania kupitia wizara ya Elimu. Kukiuka na kudharau agizo halali la Waziri ni kosa linaloweza kupelekea Shule husika kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kwa mnaosema elimu ni gharama, hivyo kama hayupo tayari kulipa hicho kiasi basi amuhamishe mtoto kwenda shule nyingine. Ndugu yangu, bila shaka hujafikiria gharama inayoambatana na kumuhamisha mtoto shule interms of usumbufu kwa mtoto na implication yake kitaaluma. Na hiki ndicho wanachokitumia hawa wamiliki wa shule kuwa exploit wazazi, kwakuwa basi itakuwa ni kuhamisha watoto kila kukicha, leo unampeleka huku kesho kule kila ada inapopandishwa. Na hata wizara ilizingatia hilo mpaka kuja na pendekezo la ku regulate bei za ada ktk shule binafsi.
Hii ni kama vile EWURA wanavyo regulate bei za mafuta, kwanini wasiseme kama humudu gharama za kujaza gali mafuta basi tumia baiskeli, kwa nchi yoyote makini ni lazima kuwe na regulation ili kupunguza Unyonyaji baina ya Raia wake.

Ikumbukwe kiasi cha pesa alichokitaja huyu bwana kwamba kimeongezeka ni kikubwa mno, karibu asilimia 27. Na ninavyofahamu, wazazi wengi, kutokana na upendo kwa watoto wao, huwa wanaogopa kulalamika kwenye vikao wakihofia watoto wao kuwa mistreated. Hivyo wengi hukaa kimya, wakinung'unika na wakiendelea kuumia, na hii ndo maanz serikali imeingilia kati.

Ndugu wamiliki wa shule binafsi, zingatieni agizo la waziri kwani kipindi cha kuamua mambo kwa namna mnavyopenda wenyewe kimepita, huu ni wakati ambao masilahi ya Taifa yamewekwa mbele kisha masilahi yenu ya kibepari.
 
kama anawauzia hisa ni poa unakuta mtu kaanzisha shule halafu anawaambia wachangie majengo au madawati wakati zile ni investment zake binafsi
 
Ndio hvyo changieni mbona kwenye harusi mnachangia wakati ni uwekezaji wa kuhalalisha uzinzi wa watu wawili kwann kwenye elimu hamchangii wakati inaenda kunufaisha wengi badilikeni

Mchango wao wanautoa katika mfumo wa Ada na Malipo ya usafiri. Kuwachangisha kwa mara ya pili inakuwa ni kuwatwika mzigo wasioustahili.
 
Na kwenye harusi kuna malipo ya usafiri na vilevi na vingine vingi vya hovyo tena mnachangia harusi hadi kumi kwa mwaka kamchango ka shule moja tuu kelele hahahaha.....
 
Mchango wao wanautoa katika mfumo wa Ada na Malipo ya usafiri. Kuwachangisha kwa mara ya pili inakuwa ni kuwatwika mzigo wasioustahili.
Na kwenye harusi kuna malipo ya usafiri na vilevi na vingine vingi vya hovyo tena mnachangia harusi hadi kumi kwa mwaka kamchango ka shule moja tuu kelele hahahaha.....,
 
Ni ajabu na kweli kuna shule ya ST. Ignatius iliyopo hapa Dodoma imewataka wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wachangie ununuzi wa basi jipya kwa ajili ya kupeleka watoto shule pamoja na kuwa wamelipwa Ada na nauli ya kuwapeleka na kuwarudisha watoto shule. Hii shule ni ya Taasisi ya kidini lakini Ada zake na huduma zake hazifanani kabisa na huduma wanayotoa.

Pamoja na kuwa serikali imekataza Ada isipandishwe bado wenyewe wanasisitiza lazima wazazi walipe ada waliyopandisha ambayo ni Milioni moja na laki sita na nusu(1,650,000/=) kuanzia mwaka huu , aada iliyokuwepo hapo mwaka jana ni Milioni moja na laki tatu(1,300,000/=) kwa mwaka .Tunaiomba serikali iiangalie sana shule hii maana nayo ni jipu kama majipu mengine.

Hamisha mtoto mkuu, haina maana kuja kulalama humu wakati unaweza kumpeleka mwanano St Thome, ST Gaspar, Msalato DCT, Martin Luther and others. Be wise man
 
Na kwenye harusi kuna malipo ya usafiri na vilevi na vingine vingi vya hovyo tena mnachangia harusi hadi kumi kwa mwaka kamchango ka shule moja tuu kelele hahahaha.....,

Harusi huwa unachangia kwa kutoa kiasi kilichoandikwa kwenye kadi baasi. Ukifika ukumbini utakula, utakunywa, utasikiliza mziki nk.
Kwa kutumia hii analogy, ni sawa na kusema uchangie harusi kwa kutoa mchango uliopo kwenye kadi, halafu ukifika ukumbini utakiwe kulipia chakula utakachokula na kinywaji utakachokunywa. Swali ni, ule mchango tulioutoa umefanya nini?
 
Hamisha mtoto mkuu, haina maana kuja kulalama humu wakati unaweza kumpeleka mwanano St Thome, ST Gaspar, Msalato DCT, Martin Luther and others. Be wise man

Kwa nini umsumbue mtoto kwa kutokana na tamaa ya fedha na unyonyaji wa wamiliki wa shule?. Na hili likiachwa liendelee hivi, mtoto atahamishwa mara ngapi?
 
Back
Top Bottom