shule za kata zimekuja mambo yamekwishaharibika. Na kimkakati mtoto alitakiwa asome katika kata yake ambapo mwendo wa km 10 at most, Sisi pia tulipokuwa tukisoma kuna waliokuwa wakitoka mbali na shule japo si kigezo cha kutetea hoja. Elimu inakuwa na mwamko pale mwanafunzi anapoona waliotangulia wananufaikaje. Lilivyotekelezwa ni swala ambalo pengine limeleta janga. Kama tunavyoona shule za binafsi pia zina viwango, nyingine ya chini hata kuliko za serikali! Hivyo mikakati ya kuboresha elimu, hasa ya kata, iangaliwe upya ili pasiwe mahari pakupoteza muda.Kumbuka miaka ya nyuma hapakuwa na shule za kutwa, walimu walikuwa na wito. kipindi kile serikali ilikuwa inagharimia kila kitu kuanzia madaftari, vitabu na madawati. shule za msingi kulikuwa na bohari za vitabu shule zikifungiliwa vitabu vilikuwa vinasambzwa mashuleni, sekondari wanafunzi walikuwa wanasafirishwa. wanafunzi walikuwa wanakula vizuri. tulipoanzisha shule za kutwa na kata elimu ikaanza kushuka, fikiria una mtoto wa kike wengi wanamaliza darasa la saba wakiwa na umri wa kati ya miaka 13-15 hapo ndiyo foolish age, unampeleka shule ya kata km 50 akapange na kujitegemea, ajipangie ratiba ya kusoma, ratiba ya kupiga, ratiba ya kusali, ratiba ya kutembea na kujilinda na maadui watoto wa kiume, ataweza kuhimili haya yote pamoja na mabadiriko ndani ya mwili wake? basi ikiwa una kauwezom kidogo utajibana ili mtoto akasome hizo shule za binafsi hutaki subiri mjukuu. Hivyo serikali ina haja ya kuboresha elimu kwa shuke zake lkn pia kuthamini mchango wa hizi shule za binafsi lkn pia pia ada zisiwe juu sana zinajenga matabaka ndani ya jamii.
Pengine kubwa zaidi ni uwzo wa walimu, wengi wanachaguliwa au wanakubaliwa kuingia kufundisha wakiwa na passmark ndogo. Tuongeze kiwango cha entry grade ya kozi za ualimu si hii ya sasa. Pamoja na kuwa tutakuw na uhaba pengineni bora hili kama kiwango kitaongezeka. Kuna wasomi wengi wenye degree nzuri tu wamepunguzwa kazi wahamasishwe kujiunga kufundisha kwa kipindi maalumu kwa mishahara maalumu. Na visiongezwe muda, endapo atapenda kuendlea kufundisha basi aingie katika ajira ya kawaida ya ualimu.