Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Dancani, Jan 7, 2013.

 1. Dancani

  Dancani JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2013
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 800
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limetaja shule 24 za sekondari ambazo zitatoa wanafunzi 5,000 waliomaliza kidato cha sita watakaojiunga na jeshi hilo. Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Mahuga alisema katika taarifa yake jana kuwa wanafunzi hao watatakiwa kujiunga na jeshi hilo ifikapo Machi 2, mwaka huu.

  Shule hizo za sekondari ni Kibondo, Musoma, Kibaha, Ilboru, Bagamoyo, Jitegemee, Tabora Wavulana na Nganza.Shule nyingine ni Mtwara Wasichana, Ihungo, Kilakala, Benjamin Mkapa, Maswa Wasichana, Dodoma, Tumain-Singida na Galanos. Nyingine ni Ashira, Nangwa-Manyara, Iyunga, Mpanda, Lindi, Iringa Wasichana, Kawawa-Iringa na Ruhuwiko-Songea.

  Taarifa hiyo ilisema maofisa wa JKT watakwenda kwenye shule hizo kuanzia Januari 9, mwaka huu kwa ajili ya kutoa utaratibu wa mafunzo na kambi ambazo watakwenda."Mkuu wa JKT kwa mamlaka aliyopewa kisheria ya mwaka 1964 na kufanyiwa mapitio mwaka 2002, chini ya kifungu cha sheria namba 5," ilisema taarifa hiyo. Iliongeza kuwa "Anawaita vijana watakaohitimu kidato cha sita mwaka 2013 kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ifikapo terehe 2, Machi 2013." Utaratibu wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria ulisimamishwa tangu mwaka 1994.

  Akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Jeshi la Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Julai mwaka jana, Waziri wake, Shamshi Vuai Nahodha alisema kambi zilizopo za JKT zina uwezo wa kuchukua vijana 20,000 kwa wakati mmoja, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti mwaka huu wataanza kwa majaribio na vijana 5,000.


  Alisema wanafunzi 41,348 wanatarajiwa kuhitimu elimu ya kidato cha sita katika mwaka 2013 na kwamba vilikuwa vikiandaliwa vigezo ili kuwapata vijana 5,000 ili kujiunga na JKT.

  Kwa mujibu wa jarida la JKT, mafunzo hayo yatakuwa ya miezi sita katika Kambi za JKT Bulombora na Kanembwa mkoani Kigoma.
  Nyingine ni Mlale (Ruvuma), Mafinga (Iringa), Msange (Tabora) na Oljoro(Arusha).

  source Shule 24 kutoa wanafunzi kujiunga JKT mwaka huu - Kitaifa - mwananchi.co.tz

  Hoja: Kwanini huo mujibu wa sheria uwe kwa baadhi ya wanafunzi na kwanini wamelenga kuchukua wanafunzi kutoka shule nyingi za serikali kama sio zote na isiwe zile za watu binafsi?
   
 2. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2013
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii iko kwenye majaribio kwa mujibu wa taarifa uliyoleta, Labda tungoje maana idadi ya wahitimu 41,000 kuchukua hao 5,000 ni kidogo sana. Serikali inabidi kujipanga sana kwenye haya makambi maana ugonjwa wa UKIMWI na muenendo wa tekinolojia ya mawasiliano ni changamoto kubwa. Kila la kheri vijana maana naijua hali ya majaribio iko je!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2013
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,139
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  mbona wamechukua shule chqche sana?
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2013
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,731
  Likes Received: 1,296
  Trophy Points: 280
  Nahisi maafande watapata mlo wa watoto wetu,loo nahisi kutakuwa na visa vya mapenzi kwa sana
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2013
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,718
  Likes Received: 21,802
  Trophy Points: 280
  Kwani lazima?
   
 6. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2013
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,296
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Wangeanza na marian st francis aga khan mzizima st marys shaaban robert maria goreth academic loyola n the likes. Uko ndo watu wako kimayai mayai afu hakuna uzalendo. Wengi waliosoma shule za serikali uzalendo upo kwa kiasi fulani.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 7. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2013
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,911
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  Maoni yangu haya hayausiani na mtu wala kikundi cha watu

  Hapa kwenye JKT kwamba ndio inajenga uzalendo mi naona ni uongo mtupu yaania uongo ulio wazi
  kwani viongozi wetu wengi wamepitia huko na wengine ni wanajeshi wastaafu lakini mambo wanayoyafanya
  hayahusiani na uzalendi hata kidogo.
  Tuangalie kashfa nyingi zinazotokea kwa viongozi wetu je hawa hawajapitia JKT ?
  Jiulize kama hizi kambi hazitakua vyanzo vya kuambukizana HIV hawa wadogo zetu wnaenda kufanya nini
  huko kipya na je wameandaliwa mazingira gani madhubuti .kama kwenye vyuo vikuu kunaibuka akshfa za mabinti
  kujiuza je hili la JKT halitaongeza maambukizi ya HIV na mmomonyoko wa maaadili kwa hawa vijana.
  NI kwa nini serikali haiangalii jinsi ya kufufua viwanda ili hii nguvu kazi ikatumika hta kwa kujitolea kwenye
  hivyo viwanda kwa muda mfupi kabla ya kuanza maisha yao ya uraiani baada ya kutoka shuleni.
   
 8. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2013
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  ...kwa vision ile ile ya kurudisha na kujenga umoja wa kitaifa! Alafu utashangaa hizo zilizoachwa zitajengaje utaifa huo.
  Wengi hawapendi kuchanganya kingereza na Kiswahili lakini kwa kifupi ni kuwa "we are lost as a nation"!!
   
 9. Ze Heby

  Ze Heby JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2013
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 3,342
  Likes Received: 1,618
  Trophy Points: 280
  Hatuwezi kuwa wazalendo kwa namna hii.Mnawezaje kuona uhaini mioyoni mwetu ilihali hamuoni ufisadi wenu ulio wazi kabisa.Am telling you my dears,wazungu walifanya kosa kubwa kumuelimisha Mwl. Nyerere,na ndivyo mnavyoingia mkenge huo.
   
 10. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2013
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 28,607
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  hapa ni sawa, na ndo wakati wa serikali kutambua watu wake waliosoma st. nyerere kwa mwisho wa siku ndo watakaochaguliwa kwendaa vyuo vikuu vya serikali pia.
   
 11. I

  Izzo G JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2013
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 418
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  nimegundua kit watoto weng wa vigogo ndo hao wanaosoma marian galz,feza boyz, na hawaend huko ila wa maskn ndo chambo haya bhanaa
   
 12. w

  wa katikati Member

  #12
  Jan 7, 2013
  Joined: Oct 30, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  jangwani?, zanaki?, kisutu?- au makamanda hawataki kuburudika?.
   
 13. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2013
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,817
  Likes Received: 816
  Trophy Points: 280
  Mtoto wangu hatokanyaga huko JKT kamwe
   
 14. S

  SN.BARRY JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2013
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  wanaenda kuandaa makamanda wa chadema 2015, pia wasipojiangalia wanaenda kuzalisha majambazi, maana ajira hamna.
   
 15. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2013
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakuna nchi puuzi kama Tanzania chini ya huyu Kikwete. eti unlazimisha mtoto aende jeshini kwa mujibu wa sheria ya 1960s. Ni kwa nini vijana wasapply kwa hiari kama wanapenda kwenda? Kilichotekea miaka hiyo sio kinachotokea sasa. NYERERE alikuwa na upendo na uzalendo mkubwa kwa nchi yetu. Sasa huyu mnyany'anyi anakusanya watoto hawa kwa maadili gani aliyo nayo? Tusijidangane nchi hii imeoza kimaadili. Hawa watoto wataishia kufa ukimwi na sii zaidi. Angalieni the so called UDOM.
   
 16. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2013
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,859
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  bora special school zipo
   
 17. s

  structuralist JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2013
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,169
  Likes Received: 679
  Trophy Points: 280
  Kimsingi haya ni matokeo ya kukosa dira. uzalendo unaletwa na jkt? hii sio sawa; Haihitaji hata elimu ya darasa la saba (enz za mwl)kufahamu kuwa tuhuma zote kubwa za ufisadi nnchini,rushwa,dili za nyar za serikali na ishu nyingine zinawahusu watu ambao walipitia jkt. Inasikitisha kuona kama nnchi tunaacha kutatua matatizo ya msingi kama ya ajira tunakimbilia vitu ambavyo havina tija. Hivi tungeelekeza fedha hizi kila mwaka kwenye miradi mikubwa hasa ya viwanda tungesukuma uchumi huu kwa kiwango gani? Waliopo madarakani walipitia jkt mbona wanalipeleka taifa kusiko?mbona hawana uzalendo? au uzalendo wao ni kuuza ndege tatu kwa sh laki tano,chini ya bei ya king"amuzi? Au kuchukua nguzo iringa kuzipeleka mombasa then kuzidusha na kusema zimetoka south na kuuza nguzo moja milion?Au kukodishia aridhi sh 200 kwa heka kwa mwaka kwa wawekezaji? hata mimi nimekuwa na wasiwasi inawezekana kuna ajenda ya siri katika hili. Chondechonde kwa mtakao enda huko hasa MABINTI, angalieni mambo kwa jicho la tatu,hautafuti ajira jkt kwa hiyo incase kunamtu/watu wanakupresurize kwenye mambo yaleeee,kuwa na msimamo wa kweli na usiogope vinginevyo ndoto zako zakuwa.................baada ya 3 yrs zitayeyuka.INSHAALAH MUNGU ATAWALINDA
   
 18. mkandi

  mkandi JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2013
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapo makamanda wanaogopa moto!


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. Yusuph p. Kisunzu

  Yusuph p. Kisunzu Senior Member

  #19
  Jan 8, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari tuliomaliza f6 mwaka jana mtu hawezi kupelekwa?
   
 20. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #20
  Jan 8, 2013
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,097
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  acha hiyo kitu loyola kuna raia waliindaga zamaniii
   
Loading...