Shukrani ya malezi . . . . . !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shukrani ya malezi . . . . . !!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Aug 16, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,650
  Trophy Points: 280
  Najua jambo hili linaweza kuwa gumu kwa wengi,hii ni kutokana na mazoea.Hebu tutoke kwenye mazoea. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Ni jambo la kawaida kusikia kauli kama "hivi we mtoto nikikuambia unilipe kwa jinsi nilivyokulea utaweza" au "we mtoto huna shukrani,nimekulea vyema hivi" au "sijui nikulipe nini kwa malezi yako kwangu" n.k,kauli hizi mara nyingi hutolewa na wazazi au jamii inayotuzunguka au na watoto,kwanini uwaze kulipa mtu fadhila kwa kufanya kazi aliyojitakia mwenyewe tena kwa raha zake bila kukushirikisha?Ooo sijui nikulipe nini mama/baba kwa kunilea ili iweje?. . . . . . . . , . . . . . . , . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Hivi kulea mtoto ni sadaka?Au ni hisani?Wakati unamtafuta mtoto unajua kabisa atakachohitaji na yeye wakati huo hayupo na hachangii kwenye mjadala wenu,kwa kifupi hausiki na mipango ya kumleta duniani,iweje leo kumpa yaliyo HAKI yake ifananishwe na msaada?Mnawanyanyasa watoto kisa malez,kwa nini? . . . . . . . . , . . . . . . . . , . . Kumlea mtoto ni LAZIMA na mtoto asihusishwe na ujinga wa kumtisha kuhusu malezi.Najua hii ni ngumu kwa wengi,kwani ndivyo tumekaririshwa kutokujaji haya eti tutapata laana,ujinga tu.Usiogope malezi ni haki ya mtoto yoyote na hatakiwi kutishiwa nayo.Tuache kufikiri kimazoea ala!!!!
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,177
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Mhh Eiyer yamekukuta nini
  Ni kweli ni wajibu wao kuwalea wale waliowaleta duniani na mtu anayesema hayo hajui kuwa ni wajibu wake kumpa mtoto wake aliyemleta duniani malezi na elimu na kila hitaji lake mpaka atakapoweza kujitegemea au kufika ule umri ambao anaweza kujitegemea mwenyewe
  Ila wengi hawajui hilo wanaona malezi kama hisani ambayo inatakiwa kuja kulipiwa baadae
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,650
  Trophy Points: 280
  Mr Rocky hayajanikuta,ila nimeona watoto wengi sana wakinyanyaswa kwa kivuli cha malezi.Mtoto anatishiwa,eti"nikikuambia unilipe kwa jinsi nilivyokulea utaweza?" kauli hizi ni za kijinga sana!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,688
  Likes Received: 12,725
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu umenena vyema yatupasa kufurahia kuwalea watoto wetu kama tulivyo furahi kuwaleta duniani.a
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,650
  Trophy Points: 280
  Yes,tena bila kuwadai fidia!!!!
   
 6. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Cha ajabu wazazi wanaosemaga hizo kauli ni wale ambao hata malezi yao sio bora kiasi cha kuyapigia debe hivyo! Wazazi wanao walea watoto wao vyema kabisa hua hawana muda wa kauli kama hizo, wanajua fika kua ni wajibu na sio msaada..
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Baby braza, acha kum-mind mzazi bwana. Mrushie airtel money, wewe ndo pensheni yake mwenzio.
   
 8. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,943
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  most of time nnapozinguana na mshua, utasikia ivi wewe tungekuacha ulivyougua ulivokuwa mtoto ufe, au utasikia wewe unajua gharama tulizotumia kukusomesha? nguo tulizokununulia....nk. sasa uwa kila siku najiuliza ivi kweli iyo haikuwa haki yangu? maana ya kupata mtoto ni nini? nnachoamini ni kuwa mtoto uliyemzaa tena kwa raha zako ni wajibu wako kumpa mahitaji yote mpaka atakapofikia umri ambao ataweza kujimudu na ajitegemee
   
 9. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,650
  Trophy Points: 280
  Huwa napenda sana majibu yako,me love u sana dada!
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,650
  Trophy Points: 280
  Yaani wanakera sana hawa watu!
   
 11. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145

  Hili ni tatizo la baadhi ya wazazi kutokufahamu wajibu wao kama wazazi! Ni wazazi wasiojijuwa kama ni wazazi na hivyo kufikiria kuwa kumlea, kumtunza na kumsomesha mtoto ni kama msaada tu wanatoa! Kazi kweli kweli!
   
 12. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kwa upande mmoja ni sawa Mtoto kutonyanyaswa kwa sababu ya Malezi ya wazazi wake kwake..
  But lazima pia tufikirie kuwa hakuna HAKI bila Wajibu..Unao wajibu as mtoto unaotakiwa kuufanya kwa mzazi wako..
  Haijalishi ni malezi gani unapata lakini ni lazima ufikirie na wewe mtoto unao wajibu gani kwa mzazi wako?
  Mfano unakuta watoto wengine hawana adabu kabisa,wana dharau na pengine wanaanza kujifunza tabia mbaya kama wizi..
  Katika mazingira kama haya ni nadra kukuta mzazi anakuwa na mapenzi na mwanae na ndio hapo unaposikia..'ningekuwa najua hata mimba yako ningeitoa'..
   
 13. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ni kweli malezi ni wajibu wa mzazi lakini a small appreciation is nice, kumbuka mtoto anapaswa kumthamini/kuheshimu mzazi wake (4th commandment).
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,650
  Trophy Points: 280
  Tena kazi kubwa sana . . . . .
   
 15. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe SnowBall kuwa Mtoto ana wajibu kwa mzazi wake na pia anapaswa kuonyesha appreciation kwa upendo aliopata toka kwa wazazi. Lakini anachozungumzia mtoa mada siyo tatizo la mto kukosa kuwajibika au kuwa na tabia mbaya, nafikiri anamaanisha ile hali ya mzazi kutumia nafasi yake vibaya kumnyanyasa mwanae! Mathalani, baba yako mzazi kakupiga mzinga kuwa ana hali mbaya anaomba kiasi fulani cha fedha, kwa wakati huo na wewe huna hivyo unajitahidi na kumtumia nusu - Majibu anayokupa ndo kama hayo, wewe mtoto unanifanyia mambo kama vile sikukuzaa wala kukutunza, pesa gani unayonipa? Sasa wazazi wa staili hizi ndo tunaowazungumzia, wanatumia nafasi ya uzazi vibaya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...