MASHANJARA
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 379
- 500
Mheshimiwa Professor Anna Tibaijuka (Mama), Waziri na Mbunge, Mjumbe wa kamati kuu ya CCM naungana na waungwana wengine walionitangulia kukupa heko kwa ujasiri wako, umadhubuti wako, na misimamo yako katika kazi za umma.
Hata kukubali kujiunga hapa, tena kwa jina lako halisi ni ujasiri usio kifani nikijua wewe ni mama, mwanasiasa, msomi uliyebobea, mwanadiplomasia, mwanamageuzi ndani ya CCM na mwenye kuthubutu kwa kauli na matendo.
Naamini kuwapo kwako hapa kutatufundisha wengi na mengi, kutawasaidia kupevuka viongozi wengine ndani ya CCM na pengine kukiokoa chama chako na serikali yako, lakini zaidi na muhimu Tanzania yetu.
Karibu sana na huu ni mtihani pia kwako kwa namna nyingi. Binafsi, na kwa jina la Tanzania, nina imani na wewe. Karibu sana.