Shukrani kwa Rais Samia na Serikali yako tukufu

Sep 27, 2021
11
45
Tunashukuru Mh. Rais Samia na Serikali yako sasa tumeanza kuona ajira mpya. Ni jambo la kheri na inatia faraja kiasi.
Lakini pamoja na hayo yote mema na mazuri, Mheshimiwa tunaomba usawa katika nafasi hizi kama ikikupendeza nikiwa na maana hii:

1. Kuna baadhi ya kada hazipati fursa ya kutoa ajira nyingi pamoja na kwamba zina uhitaji. Kwa Mfano; kilimo na mifugo huwa zinatangazwa nafasi 3 au 4 kwa mwaka (hakuna uhalisia kwamba Tanzania nzima uhitaji wa watu watatu kwenye sekta hii Mheshimiwa).

2. Nafasi za walimu walau huwa zinatoka kwa maelfu na hii siyo mbaya sana japo haikidhi uhitaji.

3. Watu wa ulinzi hawa (jeshi, magereza n.k) tunashukuru tumeona nafasi zinatolewa japokua vigezo ni vikali sana (sio wote wenye astashahada , stashahada na shahada. Wenye vyeti vya JKT wapo na wana hamu ya kuomba nafasi hizi).

Haya machache yamebeba mengi kati ya yale tuliyo nayo sisi vijana wako wazalendo. Mungu aendelee kuibariki Tanzania.

Asante.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom