Shujaa wa Afrika

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,147
33,298
Shujaa na Bora ni yule anaesimamia kwa haki Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao,pamoja na kuhakikisha umoja wa taifa.
kama hawahakikishii Raia wake wote Ulinzi,Usalama na umoja wao huyo kwangu mimi sio Bora wala sio shujaa.

Bora na shujaa hutoa uhakika wa Usalama na Ulinzi hata kwa watu wawili tu katika nchi yake,ndio maana kuna nchi Raia hata watano tu wakifa kwa tukio ambalo sio la kawaida kiongozi wa nchi anaweza hata kukatisha Ziara yake na kurudi nyumbani kufuatila juu ya vifo vya Raia wake.

Kwangu mimi Naweza kusema,Shujaa na Bora yoyote ni kuhakikisha Raia wanakua huru, salama na wamoja katika nchi yao.

Ni yule anaeheshimu katiba,
anaeheshimu mihimili mingine ya dola kama Mahakama na Bunge, anaeheshimu Sheria,
anaeongoza watu wake kwa kufuata utawala wa sheria,
asiebagua watu wake kwa sababu zozote zile,ziwe za kibinafsi au za kisiasa,
hatakiwi kuwa na visasi,kwa sababu ana madaraka makubwa mno akiyatumia kufanya kisasi utakua ni uonevu mkubwa mno,
Hatakiwi kutoa lugha za vitisho,dharau au uongo.

anaeheshimu maoni ya watu wengine, kwa sababu binadamu tuna Mawazo tofauti na mitazamo tofauti,kwa hiyo kuheshimu Mawazo sio kukubali Mawazo,hivyo si vema kumchukia ama kumdhuru mtu mwenye Mawazo tofauti.

Ni yule anaeheshimu ushauri wa waliomtangulia,au wastaafu au wazee,

hatakiwi kuongoza nchi "kimafia".
au kuruhusu nchi yake kuwa na magenge ya mafia yanayoteka watu,kupiga watu,kupoteza watu,

ni yule Anaetakiwa kuhimiza uchunguzi wa watu wote waliopotezwa,walopigwa,waliouwawa na kuumizwa kwa namna yoyote ile hata kama watu hao hakua anawapenda,
anaesimamia haki hata za maadui zake.Huo ndo ushujaa.

Anatakiwa atumie vyombo vya dola,kuyapeleleza, kuyabaini magenge ya wasiojulikana yaliyohusika na kuteka,kupiga kupoteza na kuua watu na kisha kuyavunjilia mbali.

Ushujaa au ubora hauji kwa kujenga miundombinu,kwa sababu ujenzi wa miundombinu sio hisani wala fadhila,bali ni kazi ya moja kwa moja ya kila serikali katika nchi,na Duniani kote.
Ndio maana karibu kila serikali hapa nchini na kote ulimwenguni kuna wizara za ujenzi,
na ujenzi wote hufadhiliwa kwanza kabisa na kodi za wananchi wenyewe na mikopo,na sehemu kidogo ni misaada.
Kumbuka mikopo huja kulipwa baadae na kodi za wananchi.

chaguzi za kidemokrasia kwa mfano Uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi mkuu inaweza kumfanya asionekane ni bora au shujaa.

Kuteka na kunyang'anya fomu wapinzani wakati wa kurudisha fomu kwenye ofisi za Uchaguzi,

kukalia kimya wizi wa wazi wa kura wakati wa Uchaguzi inaweza kumfanya asionekane bora na shujaa.

kukalia kimya watu wenye mitazamo tofauti wakipigwa,wakitekwa,wakiharibiwa mali zao ,wakipotezwa au wakiuwawa bila kuhimiza haki zao zipatikane kama uchunguzi inaweza kufanya aisonekane bora ama shujaa.

kwa nchi inayoitwa nchi ya wakulima na wafanyakazi.
kuwanyima ongezeko la mishahara wafanyakazi kama ilivyoainishwa kisheria ya ajira na utumishi ni kuwaharibia Maisha wafanyakazi walio kwenye utumishi na hata watakapokuja kustaafu,

Ikumbukwe kuwa, kwa heshima kubwa wameitumikia nchi yao kwa weledi mkubwa Hadi wakafikia umri wa kustaafu bila kufukuzwa kazi.
kutokuwaongeza mishahara Hadi yeye binafsi apende kinyume na Sheria za ajira,ni kitendo kinachoweza kumfanya asionekane shujaa na Bora.

kutokuwatendea haki wakulima na hasa wa mazao ya biasharana chakula, mfano wakulima wa korosho ni kitendo kinachoweza kumfanya asionekane ni shujaa na Bora.

kuingilia akaunti za benki za watu,hasa wafanyabiashara wakubwa,kuzuia fedha zao,kuzichuku fedha zao na kuwasumbua ni mambo ambayo shujaa na Bora hatakiwi kuyafanya.

kuwasumbua wawekezaji kwa sababu zisizo na mashiko ni vitendo visivyo vya kishujaa.

kwa kifupi Ujenzi wa miundombinu kwa kutumia fedha za walipakodi sio Ushujaa wala kuwa wewe ni bora.
kwa sababu wote waliopita walijenga miundombinu na wote watakaokuja watajenga,kwa sababu hiyo ni kazi ya serikali.

shujaa na Bora ni yule anaehakikisha raia wote wanakua huru,wamoja,wenye Usalama wao na mali zao bila kujali waliomchagua na ambao hawakumchagua,anaowapenda na asiowapenda,wanaompiga kisiasa na wasiompinga kisiasa.

Shujaa ni yule asieruhusu chemo chale kitumiwe vibaya na walio chini yake au wateule wake.

Mfano mteule wake yoyote akituhumiwa tu kwa uhalifu au kukiuka maadili ya kazi,shujaa amwajibishe mapema.
 
Lengai ole Sabaya alikua ni kipenzi cha Mamlaka yake ya uteuzi.
Aliishi apendavyo na kutenda atakavyo.
Tujifunze jamani lolote linaweza kutokea.
Makonda hakujua iko siku atakuja kuwa hana madaraka yoyote na Lengai hakujua iko siku atakuja mfungwa.
 
Back
Top Bottom