Shujaa: Maj Gen Mwita Chacha Marwa "Kambale" Afariki

Mkuu tafuta mbona na waitara tuwajue pia hata mwamunyange


..Kikwete, Waitara, Mwamunyange,.. walikuwa maofisa wadogo mwaka 1978/79 wakati wa Vita vya Kagera.

..Waliopewa hayo majina walikuwa ni Wakuu wa brigedi na division zilizokwenda mstari wa mbele. Rank zao zilikuwa ni Brigadier(siku hizi brigadier general) na Major Generals. Nadhani alikuwepo Kanali mmoja kama sikosei jina lake ni Col.Tumbi.

..Kama taifa tunapaswa kuandika kumbukumbu ya vita vya Kagera. Makamanda karibu wote waliopiganisha vita ile wametangulia mbele za haki.
 

Msekwa ameingia UDSM wakati CCM hajazaliwa.
 
Je vijana wa leo mnaweza!!?? Kw ss hakuna uzalendo,vijana wamejazwa sumu na wanasiasa,leo ikipatikana vita tanzania,watanzania wengne watakuwa upande wa adui,Eti nao unaitwa ni uzalendo,R.I.P MARWA.NAKUMBUKA ULIVYOITEKA MTUKURA BAADA YA SIRAS MAYUNGA KUPAMBANA NA PARACOMANDOO YA JUVNALI HABYALIMANA.
 
Mashujaa wengi wamesahaulika. Hakuna maandishi ya yale waliyoyafanya. Tumebakia kuwasoma kina Napoleone, Douglas McArthur, Einsenhower etc
 
B

Hicho kibao kama sikosei kilipigwa na bendi ya Polisi (Kimulimuli) wakiwemo kina Zahir Ally Zorro na Mzee Kassim Mapili.
Kimulimuli ilkuwa bendi ya JKT Mafinga. Mwanzoni kulikuwa na JKT Kimbunga pale Mgulani halafu ikagawanya mara mbili na kuzaliwa Kimulimuli iliyopelekwa Mafinga.
 
Taifa ni lazima liwe na mashujaa wake, mashujaa ambao watakumbukwa na kuamsha mioyo ya mashujaa wengine. Taifa lisilotukuza na kuenzi mashujaa wake ni taifa linalojiumiza lenyewe kwani mwisho wa siku linakuwa taifa lisilo na mashujaa; taifa la watu wa kimchezomchezo. Nashukuru walioirudisha thread hii.
 
Nimekumbana na clip hii online ya brigadier Marwa (wakati huo) akiwa anateka vijiji vya Uganda kimoja kimoja. Watu wanadai hakuwa na elimu lakini unasikia kabisa kuwa anaongea kwa mantiki ya mtu aliyesoma vizuri. Alipata Comission yake ya kuwa 2nd Lt Uingereza nadhani Sandhurst ambako minimum entry wakati huo ilikuwa ni darasa la 12 la Cambridge (siyo form 4)!

 
RIP Kamanda, tutakukumbuka daima mwamba, hawa ndio walikuwa wazalendo wa kweli akiwa na akina Mayunga,Twalipo,Musuguli a.k.a mti mkavu nk.
Safiri salama mwamba.
 
Kama kuna mwenye pdf ya kitabu KUZAMA KWA NDULI IDD AMIN DADA kilichoandikwa na KPT Baldwin Mziray kama mpiga picha wakati wa vita ya Kagera atupie hapa tujikumbushe matendo ya kishujaa ya huyu Mwamba
 
Mungu ampuzishe salama...Wazalendo kama hawa nchi inawamisi sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…