Shujaa: Maj Gen Mwita Chacha Marwa "Kambale" Afariki

bin maryam comment yako inasikitisha sana sana..kwanza inabidi ufute kauli yako kuwa makamanda kama abdalah twalipo,david musuguri,silas mayunga,chacha marwa,walden,lupogo, imrani kombe,tumainieli kiwelu..ets kwa kuwa hawakuwa na elimu kubwa hwakuwa na mbinu...inaelekea hujui lolote kuhusu mfumo wa vita na wala hujui role ya mgambo,private hadi general/field marshall kwenye medani...kila mmoja ana kazi muhimu....

hawa makamanda ndio wapiganishaji wakuu..chini yao kwenye kamandi center wanakuwa na timu iliyotimia kabisa..na wao ndio hujenga hamasa na kuuongoza...kamanda akiwa mbovu basi hata kamandi yake yote inakuwa mbovu..

lingine lazima ujue kuwa hao makamanda unaosema ..elimu yao ni kubwa sana ...kwa kuwa vyeo hawapewi tu..na wala si kama wale wa joseph kony wanaopeana vyeo tu..hao wote walisoma elimu ya kivita canada Au sundhurst ,london....ma hiyo ni elimu inayojitegemea kabisa tofauti na uwanasheria au degree zingine.....askari kuwa na elimu nyingine hizi ni added advantage ...la muhimu ni awe na elimu ya kijeshi..lazima ujue kuwa elimu ya kijeshi nayo ni elimu!!

pia unatakiwa ujue kuwa jeshi linaenda kwa sucession ..kwa ngazi...hao unaosema walikuwa maafisa wa chini wapangaji wa vita ....nao ndio ambao unawaona wakiwa na vyeo vya juu sasa ..kipindi hicho wengi walikuwa mameja tu au makanali....hapo unawaongelea..kina...robert mboma.,meja gen msuya,waitara,gahhu,ets ..kwa kifupi wale wote unaowaona leo ni mabrigedia wengi wao wamefikia hapo kutokana na role yao vitani enzi hizo wakiwa na vyeo vya kati....

yule aliyejenga daraja ..rajabu ..alikufa akiwa brig...nani kakuambia hicho ni cheo kidogo...kumbuka brigedia anabakiza ngazi mbili tu kufikia general....na wengi huishia hapo..kwani kadiri cheo kinapokuwa kikubwa kinakuwa kinashikiliwa na watu wachache ..mfano kunakuwa na general active mmoja tu,luteni general mmoja tu,ma meja general hawazidi 8...na mabregadia hawazidi 15 kwenye service kwa kila wakati....ukiona wamechaguliwa wengine lazima kutakuwa na waliomaliza muda wao kwa sababu mbali mbali...

historia ya vita kwa maoni yangu ipo sawa kabisa.....

kuhusu wasomi kuwa suppressed hilo halina uhakika..lakini mnatakiwa kujua hivyo vyeo viwili vya juu ....rais anamuweka afisa wa juu anayemtaka..kwa mapendekezo maalum...ila hakuna njia ya kukwepa vitengo na idara chini ya hapo kuongozwa nawataalamu wasomi..ambao wengi huishia meja generals...lakini haiwezekani na wala wataalamu wakatengwa..kwani ukiangalia especially kwa sasa ngazi ya bregadia hadi meja general wa sasa wengi ni graduates na kuna hadi maprofesa,madaktari ,field engneers...ets..sasa mnapoongelea miaka ya 70 kupata magraduates jeshini ..hao wasomi walikuwa wapi..kwenye jeshi lililorithiwa mwaka 1964 kutoka kwa wakoloni...
Hivi mkuu kwenye hivyo vyeo ulivyovitaja hapo siyo kwamba akitoka meja general ndio anafata general? Hicho cheo cha luteni general mbona kama naisikia kwako mkuu?

Labda kwa kifupi kwa jinsi ninavyoelewa mimi nikutajie hizi rank za maofisa ni hivi.....

Luteni Usu > Luteni > Captain > Meja > Luteni canali > Canali > Brigedia Jenerali > Meja generali > Generali

Mkuu kama una la kusema hebu nikusikie mkuu. Ahsante
 
B
Kuna kile kibao cha "wazaaazi, wazazi wetu eeee, mashujaa waliorudi, walirudi kishujaaa..mashujaa waliokufa walikufa kishujaa, lengo na nia yetu ilikuwa mojaaaa" sijui alikipiga nani, kama mtu anacho tunaomba kirushwe hapa kumuenzi marehemu.
Hicho kibao kama sikosei kilipigwa na bendi ya Polisi (Kimulimuli) wakiwemo kina Zahir Ally Zorro na Mzee Kassim Mapili.
 
Hivi mkuu kwenye hivyo vyeo ulivyovitaja hapo siyo kwamba akitoka meja general ndio anafata general? Hicho cheo cha luteni general mbona kama naisikia kwako mkuu?

Labda kwa kifupi kwa jinsi ninavyoelewa mimi nikutajie hizi rank za maofisa ni hivi.....

Luteni Usu > Luteni > Captain > Meja > Luteni canali > Canali > Brigedia Jenerali > Meja generali > Generali

Mkuu kama una la kusema hebu nikusikie mkuu. Ahsante
Hapo kabla ya Generali kuna Luteni Generali.
 
Tuna kila sababu ya Kuwaenzi maKamanda wetu,Lakini Ndugu zangu pale kwenye Ukweli ni lazima Usemwe.Nakubaliana kabisa na Bin Maryam kuwa kulikuwa na Walakini kwenye Uwezo wa Kielimu wa Mzee Kiaro,Sina Uhakika na Mzee Msuguri,lakini kwa macho yangu nimeshuhudia Mzee Kiaro akishindwa kusema "Organization Of African UNITY".Jambo hili lilitokea Oljoro JKT wakati wa kumuaga Waziri Salim alipokuwa anakwenda kutumikia Ukatibu Mkuu wa Jumuiya hiyo.

Kwa kujua Uwezo wa Mkuu wa Majeshi,Kamanda Karubi(Mkuu wa kambi ya Oljoro kwa wakati huo)aliwaelekeza Vijana kupiga makofi na kushangilia pale Mzee Kiaro atakapokosea kiswahili au jambo lolote,Nina imani kuna vijana humu walikuwepo kwenye Shughuli hiyo na watakubaliana na hilo.

Kwa sababu nilizosema hapo awali ni kweli kwamba kuna baadhi ya Viongozi wakuu wa Jeshi walifikia vyeo walivyopata kwa ajili ya Utumishi ulotukuka na sio Elimu yao.

Pamoja na yote ni vyema tuutambue na Kuuheshimu Mchango Mkubwa ulotolewa na Makamanda wetu kuilinda Nchi dhidi ya Hujuma kutoka Nje.Mwenyezi mungu amlaze Mahali Pema Peponi Shujaa Mwita Marwa "Kambale"
Hii hoja yako nimeielewa vizuri sana
 
SHUJAA wa vita vya kagera ..maj general mwita chacha marwa amefariki dunia akiwa kwenye matibabu ...huko south afrika...kamanda huyu shupavu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingiza majeshi yetu entebbe..na kuukamata,baada ya mapambano makali...

amepata kuwa mkuu wa mkoa singida na mikoa mingine ,katibu wa chama,ets ,,pia kuna wakati alijiunga na CNADEMA kwa muda ..baada ya kuhisi kusahaaulika..kabla ya rais [nafikiri mkapa au mwinyi] kumuita ikulu na kumuuliza shida iliyopelekea kujiunga upinzani..baada ya hapo aliombwa ajitoe na mara moja tangu apo akarudishwa ikulu kama MSHAURI MAALUM WA RAIS...

HII ni thread ya kukumbuka legacy yake kama kamanda shupavu pamoja na vijana aliopigana nao bega kwa bega na wote wakiwemo makamanda ,maafisa na askari waliokomboa afrika ..kamamnavyojua role ya jeshi letu kivita angola,msumbiji,namibia,comoro ets...kwa waliopo na waliotangulia mbele za haki.....

Tupia kaphoto basi
 
..Twalipo -- " Chakaza "

..Mwita Marwa -- " Kambale "

..Silas Mayunga -- " Mti Mkavu"

..David Musuguri -- " Mutukula"

..John Walden -- " Black Mamba"

..Muhidin Kimario -- " Mbogo"

..Imran Kombe -- " Ngono ( ni kutokana Mto Ngono).

..

Hahahahahahaha safi sana duhh uko vizuri mkuu
 
Hahahahahahaha safi sana duhh uko vizuri mkuu

..nimewasahau wengine.

..Kulikuwa na " Kamanda radi "

..Kamanda "super sonic"

..Kamanda " one man one bomb"

..Kamanda " torpedo ".

..Wenye majina hayo wanaweza kuwa kati ya Majerali Wafuatao, Brigadier Hemedi Kitete, Col.Tumbi, Brigadier.Ramadhani Haji Faki, Maj.Gen.Rowland Makunda....

Cc Echolima
 
..Twalipo -- " Chakaza "

..Mwita Marwa -- " Kambale "

..Silas Mayunga -- " Mti Mkavu"

..David Musuguri -- " Mutukula"

..John Walden -- " Black Mamba"

..Muhidin Kimario -- " Mbogo"

..Imran Kombe -- " Ngono ( ni kutokana Mto Ngono).

..

Mkuu tafuta mbona na waitara tuwajue pia hata mwamunyange
 
Back
Top Bottom