Shujaa Bunge La Katiba ni Mwanasheria Mkuu Zanzibar

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,721
515
In simple terms hakukubaliana na rasimu ya katiba ya JMT inayokinzana na Katiba ya ZNZ! Achilia mbali kanga moko, viduku, vigodoro, vijembe, kejeli nk.
 
Huyo anajua, siku hizi nafasi ya AG Tanzania bara haina tofauti na nafasi ya mbunge wa kuteuliwa ccm. Ni miongoni mwa zile nafasi za wabunge wanaoteuliwa na raisi.
 
Mimi nilidhani kikundi kinachojiita UKAWA ambacho hakikupiga kura ndiyo mashujaa wa Bunge Maalum la Katiba!

Ushujaa wa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar ni upi hapo ukilinganisha na wale waliopiga kura ya HAPANA kwa Sura zote za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa hasa ikichukulia kuwa kuna Sura na Ibara ambazo Othman Masoud Othman alipiga NDIYO.

Ushujaa wake ni kurudi na kuanza kusema sura hii HAPANA, Sura hii NDIYO. Kama kweli angekuwa shujaa wa mapambano, kwa nini hakubakia ndani ya Bunge Maalum ili kutoa uchambuzi wake.

Shujaa ni yule anayepambana mpaka mwisho wa vita, siyo yule anayesubiri mapambano yanamalizika ndiyo anajitokeza na kuanza kurusha risasi.

Nadhani hufahamu hata maana ya neno shujaa katika muktadha wa mchakato wa Katiba.
 
Ukawa wanahusikaje na katiba @ Mwanadiwani ,Mwanasheria Mkuu wa Nchi ndio mpango mzima kwani Muungano wa Zanzibar na Tanzanyika inalalamikiwa kuwa hakukuwepo mwanasheria kutoka Zanzibar aliepitia kutoa maoni na kumshauri Karume ndio WaTanganyika wakatumia nafasi ya kuikandamiza Zanzibar hadi leo athari zake tunaziona.

Ila huyu ameonyesha uhuru wake na nafasi aliyonayo katika Taifa la Zanzibar hivyo hatakuwa na lawama hapo baadae iwapo kutazuka kero za Muungano.
 
mawazo mchundo kweli, hivi unadhani ukiteuliwa kuwa mwanasheria wa nchi wewe ndio umesoma sheria na kuzijua kuliko wengine?Haya mawazo ni pungufu hasa kwenye jukwaa la great thinkers. Hakuna dunia mpya tuliyopo ndio tunayoishi kwa kanuni zake, siku zote "mlipa mpiga zumari huchagua wimbo". huyu kanyea kitanda chake mwenyewe kwani huwezi kukataa kushiriki kuandika katiba nzuri, ukawaacha wenzio waandike then uje kusema kipengele hiki hapana, kwanini hukukaa nao mkakiandika vizuri?Kwamba yeye ndio ana akili kuliko wote waliokaa na kuandika, huu ni upuuzi wake na mawazo mgando!Huyu ni mchonganishi na haitakii mema nchi hii!Kumuunga mkono ni ufedhuli na haina tofauti na kuwa mhaini!Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom