ikizu
JF-Expert Member
- Oct 26, 2011
- 431
- 56
Ajali mbaya zimetokea mjini shinyanga na kuua watu zaidi ya watano hapohapo. Ajali hiyo imehusisha gari aina ya hiace iliyokuwa ikitokea Kahama kuelekea Shinyanga mjini na imetokea maeneo ya Ibinzamata karibu na Sido baada ya kuingia Mtaroni.
Wana jamvi nina rafiki yangu yuko mkoani Shinyanga ameniambia kuwa watu 7 wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka mkoani Shinyanga.
Ameripoti kuwa gari hilo aina ya Toyota Hiace lililokuwa linatokea katika Wilaya ya Kahama kuelekea mkoani Mwanza.
Aidha, amesema ameshuhudia majeruhi saba wakipelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa matibabu zaidi.
Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni mwendo kasi iliyomfanya dereva wa gari hilo kushindwa kulihimili na kupinduka.