Shuhudia ajali ya toyota hiace iliyouwa watu tisa na kujeruhi wengine tisa Shinyanga

ikizu

JF-Expert Member
Oct 26, 2011
431
0
Ajali mbaya zimetokea mjini shinyanga na kuua watu zaidi ya watano hapohapo. Ajali hiyo imehusisha gari aina ya hiace iliyokuwa ikitokea Kahama kuelekea Shinyanga mjini na imetokea maeneo ya Ibinzamata karibu na Sido baada ya kuingia Mtaroni.

Wana jamvi nina rafiki yangu yuko mkoani Shinyanga ameniambia kuwa watu 7 wamenusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka mkoani Shinyanga.

Ameripoti kuwa gari hilo aina ya Toyota Hiace lililokuwa linatokea katika Wilaya ya Kahama kuelekea mkoani Mwanza.

Aidha, amesema ameshuhudia majeruhi saba wakipelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Shinyanga kwa matibabu zaidi.

Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni mwendo kasi iliyomfanya dereva wa gari hilo kushindwa kulihimili na kupinduka.

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232

ruanganyi

Senior Member
Aug 19, 2014
115
0

[FONT=Georgia, Times New Roman, serif]
[/FONT]

[FONT=Georgia, Times New Roman, serif]Toyota haice yenye namba za usajili T761 CKD iliyokuwa ikitoka wilayani Kahama kuelekea mjni Shinyanga ikiwa imepinduka katika eneo la Buhangija manispaa ya Shinyanga na kuuwa watu tisa na kujeruhi wengine tisa,baada ya kupinduka mara tatu baada ya kuvuka tuta kisha kugonga daraja na kuangukia mtaroni,chanzo chake ni mwendo kasi ambapo dereva wa gari hilo Anwar Awadhi mkazi wa Lubaga Shinyanga aliruka na kukimbia.
[HR][/HR][/FONT]

Wananchi wakishuhudia ajali hiyo.
PICHA ZAIDI>>>
 
andishile

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
1,430
1,225
poleni sana wafiwa,na majeruhi ugueni pole!ajali zitatumaliza jamani! inasikitisha sana
 
Manosa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
4,513
2,000
Aise kama ni hii hiace ninayoijua siwezi shangaa, nilipanda tokea kagongwa-shy mbona nilisali na ilikua usiku,mwendo 160km/h ikabidi niseme maana ngosha walikua wanaona sawa, poleni sana wafiwa,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom