Shughuli za Kilimo kwa Tanzania ya sasa

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wote tunajua shughuli kuu za kiuchumi Kama Kanda ya Ziwa ni Uvuvi, kilimo, ufugaji, madini.

Kanda ya Kaskazini Kuna Kahawa, Mahindi, Migomba

Kanda ya Kati Wanalima Zaidi Alizeti, Karanga, Zabibu na Mahindi pia

Mbeya Wanalima Zaidi mpunga, Mahindi pia nk.

Wakuu Case Study ya Mada Hii ni Mkoa Wa Mara

Aslimia kubwa ya wananchi wa Mkoa Wa Mara ni wakulima na zao kuu ni muhogo kwa ajili ya kinga ya njaa na Biashara kidogo.

Na pia Zao kuu la Biashara ni Pamba lakini uzalishaji wake umepungua sana kutokana na kushuka kwa bei na gharama kubwa za madawa.

Alizeti Kwa Mkoa Wa Mara inalimwa kidogo lakini kuna changamoto ya mbegu na madawa.

Natambua juhudi za mhe. Mbunge Muhongo Mbunge Wa Musoma Vijijini kuwaunganisha wavuvi ili wafuge samaki kwenye vizimba.

Humu kuna wenyeji Wa Mkoa Wa Mara na watalaamu wenye uzoefu kwenye angle ya Kilimo

Naomba tusaidiane je tunaweza kuanzisha kilimo cha zao gani litakalo weza kuwaongezea kipato wananchi wanaoishi Mkoa Wa Mara asa Halmashauri ya Musona Vijijini?

Asanteni

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Katani inafanya vizuri sana sokoni haitaji madawa wala umwagailiaji unavuna mara mbili kwa mwaka. Eka tano ukosi ukosi milioni 40.

Wanunuzi wakubwa Chinese people.
 
Katani inafanya vizuri sana sokoni haitaji madawa wala umwagailiaji unavuna mara mbili kwa mwaka. Eka tano ukosi ukosi milioni 40.
Wanunuzi wakubwa Chinese people.
Mkuu Kalunya.

Tunaweza kuanzisha zao la mkonge na kuboresha zao la Mhogo kwa kuongeza nguvu kubwa kwenye upatikanaji mbegu kinzani za Mhogo.
.
Naana asilimia kubwa za mbegu ya Mhogo wetu zinaumwa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Kalunya.
Tunaweza kuanzisha zao la mkonge na kuboresha zao la Mhogo kwa kuongeza nguvu kubwa kwenye upatikanaji mbegu kinzani za Mhogo...
Unga wa muhogo ni biashara nzuri Sana soko kubwa Sana kanda ya ziwa pia Burundi ukifika nao tu unagombewa.

Pia unaweza ukazalisha starch ukauza nje soko ni kubwa,au unaweza ukalima muhogo kwa ajili ya kuzalisha ethanol soko ni kubwa sana popote nchini hasa kwa kupanda kwa bei hizi za petrol,so ethanol ni mbadala na production cost yake ipo chini per lita so utauza cheap kwenye market.
 
Unga wa muhogo ni biashara nzuri Sana soko kubwa Sana kanda ya ziwa pia Burundi ukifika nao tu unagombewa...
Mkuu Duniani Kote AGRI-BUSINESS Ni nguzo muhimu Sana ya kuleta maendeleo chanya na ambayo inakuza uchumi wa eneo kwa haraka na kufanya sekta zingine zikue.
.
Lakini ili tufikie malengo ya kukuza AGRI-BUSINESS ni lazima Kuna vigezo vingi vya kuangalia.
.
Mosi; Nature ya ardhi kwa Musoma DC Ni Kama imegawanyika karibu maeneo matatu kwa mazao tofauti tofauti Kama Pamba, Alizeti na mihogo.
.
Na Pili; Uwajibikaji wa serikali ngazi ya Halmashauri ktk kusaidia wadau.
.
Tatu- Uwajibikaji wa wataalamu wa sekta za kilimo, uvuvi, mifugo ngazi za kata na vijiji una shaka kubwa beyond no doubt kwa wadau.
.
Leo Mkulima, mfugaji na mvuvi kukosa ushauri wa Mara kwa Mara Ni kumuua kisaikolojia hivyo kufanya shughuli zao kuwa in harvazad condition.
.
Hivyo ili kufanikisha adhima ya hoja nashauri integration ya hoja kuu Serikali iwape Watu Elimu pia.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom