figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Shughuli za Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki zimesimama kwa muda usiojulikana kutokana na nchi mbili za Kenya na Sudani Kusini kushindwa kukamilisha mchakato wa kuwachagua wabunge watakaoziwakilisha kwenye bunge hilo.
Afisa Habari wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw Bobi Odiko amesema wakati kenya ikiwa bado inakabiliwa na changamoto za kuwapata wabunge wawakilishi wao kutoka kwenye vyama vya siasa,baadhi ya wananchi wa Sudani Kusini wamewasilishan rasmi pingamizi la kusimamisha kuapishwa kwa wabunge wa bunge hilo kwa madai kuwa wabunge waliochaguliwa kutoka nchi hiyo hawakupatikana kihalali.
Bw Odiko amesema hatua hiyo itaathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za bunge hilo la nne ambapo kwa mujibu wa sheria na taratibu kwa sasa shughuli zote zitalazimika kusimama ikiwemo ya kuwapisha wabunge wapya,kuchagua spika na kuunda kamati haziwezi kufanyika hadi mchakato wa kuwapata wabunge kutoka nchi zote wanachama utakapokamilika.
Alipolipokuwa anafunga Bunge la tatu la Jumuiya hiyo Spika wa Bunge hilo anayemaliza muda wake Mh Daniel Kidega alisema kuwa walishatoa taarifa ya kuitaka nchi ya Kenya kukamilisha haraka mchakato wa kuwapata wabunge wao ili kuepuka kukwamisha utendaji kazi wa bunge hilo.
Hadi sasa nchi tano wanachama ikiwemo Tanzania,Uganda,Rwanda,Burundi na Sudani Kusini zimeshawasilisha majina ya wabunge wanaoziwakilisha japo majina ya wabunge wa nchi ya Sudani Kusini wamewekewa pingamizi.
Chanzo: ITV