Unazungumziaje ubora wa katiba ya Kenya katika kuwawajibisha kwa haki wanasiasa?Ungetamani Tanzania Tufike walipo Kenya?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,088
4,887
Makamu wa Rais wa Kenya ameondolewa madarakani bila nguvu ya polisi kuonekana. Ameondolewa madarakani kwa kura za wazi na akipewa nafasi yakujtete bila TV kuzimwa.

Ameondolewa adharani kwa mfumo wa wazi bila kuwepo kwa maneno kwamba kuna watu wanahatarisha amani ya nchi. Ameondolewa katika mazingira ambayo kila aliyeshuhudia mchakato ameridhika kwa ni muda sasa wa yeye kukaa pembeni na kujipanga upya kisiasa.

Kilichomondoa ofisini ni KATIBA imara ambayo imetenganisha Bunge, Serikali na Mahakama. Tumeona serikali imefanya yake, Bunge limefanya yake na Mahakama imefanya yake kwa haki. Amekataliwa na wabunge means amekataliwa na umma uliowateua wabunge.

Je, bado Tanzania Tunaamini ipo siku mfumo wetu wa siasa utaruhusu maendeleo haya makubwa ya fikra? Ipo siku mfumo wetu utaondoa Chawa na kuwaruhusu wasomi na wabunge kujadili adharani? Ipo siku mfumo wetu utaruhusu viongozi wasiowajibika kuchukuliwa hatua?

Naamini Kenya wataendelea kupiga hatua za maendeleo kwa sababu wameruhusu akili kufanya kazi. Huku Tanzania akili zipo ila hazina uhuru

PIA SOMA
- Katiba ya Tanzania ni bora zaidi ya Katiba ya Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla
 
Back
Top Bottom