Shtuka..! Unaibiwa

Utakuwa ulikuwa unamtaka Brenda jamaa kakuzidi kete πŸ˜€.
 
Mimi hapo kuna kitu sijakielewa maana hilo jina karijuaje kuwa ni brenda kama yeye hajanyimwa namba kaamua kuharibu kwa njia hii
 
Tatizo ni mwanamke. Kutongozwa ni kawaida, sio lazima akubali. Japo kuna ndugu m1 alilalamika kuwa kuna wanaume wanajua kuimbisha ni hatari. Safari ya Mwanza to Dom waweza jikuta unateremka Singida (kwa mwanaume), ila ni hoja dhaifu
Hahaaa. Naona unawakingia kifua wanaume Shooo. Hivyo na wao kutongoza ni kawaida. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Kikubwa wanawake tusiwape nafasi wanaume za huko kuimbishwa maana eti mtu anashuka njiani kisa mtu ambaye hata nauli hajamlipia. Duuuh.

Maajabu hayo kwani wanashikiwa fimbo? πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Parapanda italiaa parapanda
 
Unajua wanaume kutongoza ni kawaida sana sababu ya tamaa na kibaolojia, lakini pamoja na hayo huwa tunarequest sasa mwanamke ndio mwenye mamlaka ya kuapprove.
Hahahaaa. Nimecheka sana kwa ulichokiandika ila sijuagi kwa nini huwa mnaisingizia hiyo sijui baiolojia.

Jitahidini kuizuia hiyo tamaa sababu si wanawake wote wanajuaga kukataa. Mnawapa shida tu wanawake wa watu.

Jirani sumbai nimeona lile neno lako pendwa hapa. Hahaaaa.
 
Ukhty wataka anzisha uzi ndani ya uzi?


Mungu anakuonaa
 
Aisee! Basi mi ni tatizo, unaweza kaa na Mimi siti moja hata safari iwe ya Massa kumi no story, yaani kuna kipindi huwa najishangaa, yaani hata ukinisemesha nitaona kama unanikera tu, huwa sipendi story sijui kwa nini...! Na nikikaa na Mwanamke ndo kabisaa... Afadhari mwanaume mwenzangu tunaweza ongea mawili matatu, lakini mwanamke huwa sitaki mazoea nao niwapo safarini, waifu mwenyewe kuna kipindi akiwa ananisemesha huwa namuweka wazi tu, "naomba uniache". Ye ataenda kuendelea na shughuli zake mi ananiacha ndani
 
Siwakingii kifua. Ila hatuwezi kataa wala kupinga kuwa mitongozo tunaipata sana. Iwe ni wakati wa kwenda vigengeni au masafa ya mbali. Mwanamke ndo anatakiwa ajitambue na kujithamini. Vinginevyo... Ni hasara kwa mume/mchumba. Kushuka njiani huu ni ujinga uliotukuka
 
Kuna tofauti Kati ya Whatsoop na JF
 
Updates:

Sasa hivi namuona Brenda amesinzia, shingo ameilazia kwenye bega la jamaa

Jamaa akilala na yeye lazima niwapige picha kabisa

Roho inaniuma sana kuona kijana mwenzangu anaibiwa hivi hivi na usikute nauli katoa jamaa ya kumsafirisha demu wake.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…