Shost wangu wa kwanza

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,776
Nilipomaliza shule basi ile ninaaply chuo nilijaribu tu chuo kimoja kilikuwa nchi flani hivi, majibu yamekurudi nimekubaliwa, basi nikaanza maandalizi ya safari.

Nilipofika kule nilipokelewa na mama mmoja ambae ni family friend, aunt, nilikaa kwa aunt kwa raha zote, lakini mama ambae ndiye shost wa aunt hakupenda nikae pale muda mrefu. Nilianza kujichanganya mtaani basi haikuchukua muda mrefu nilipata nyumba ya kushare na wengine.

Nilipata shost humu ndani alinifahamisha anaitwa Alex, nilipata na kibarua katika mgahawa mmoja mjini, ninafanya siku tatu kwa wiki, J1, J2 na J5 asubuhi mpaka saa tisa mchana. Kwakweli nilikuwa busy, siku nyingine nilikuwa chuoni.

Alex alikuwa raia wa nchi ile, lakini alitokea huko mikoani, hakuwa na vitu vingi zaidi ya sanduku lake. Nikirudi tu kutoka either kazini au chuoni Alex alikuja chumbani kwangu kwakuw nilikuwa na TV basi tuliangalia wote mwisho nilikwenda jikoni kupika chakula na tunakula wote. Kasheshe ilianza nikitoka kuoga aliniambia anapenda manyonyo yangu.

Jamani nilisoma boarding mbona hakuna mwanamke/msichana aliyewahi kuniambia haya? Haya ya nchi za watu haya. Kuna tamthiliya moja Alex aliipenda sana kwenye TV na mimi pia niliipenda tamthilia ile, aliniambia kwakua hana pesa ya kunipa na anakula na mimi karibu kila siku, anaomba awe analeta chocolate wakati tunaangalia tamthilia ile.

Nyumba ya pili kutoka nyumba yetu ilikuwa bar, siku moja Alex ananiambia nilikuwa ninapita pale bar nimemuona mwanaume mzuri lazima nirudi, mmh, mambo ya nchi za watu haya nilijisemea moyoni, kule kwetu mwanamke anatongozwa.

Siku moja vijana tuliokuwa tunakaa nyumba moja walinipa kwa kirefu habari za shost yangu Alex, Alex ni mwanaume ambae ameamua kuwa shoga, anatumia dawa za hormones ili ndevu zisiote. Alex alikwenda na mtu kutoka ile bar ya jirani kufika nyumbani ndiyo jamaa anastuka mwanamke aliyekuwa nae na ndimu mbili na bamia.

Yule mwanaume kwa mshtuko ndiyo aliwahadithia wale vijana tunaoishi nao nyumba moja, jamani nguvu ziliniishia, kumbe shost ana ndimu mbili na bamia.
 
Sijui ni sababu nina mind chafu au lah!

Nilichoelewa hapa ni kwamba ulinusurika kugogwa na shoga siyo?:D:D:D:D:D
 
Sijui ni sababu nina mind chafu au lah!

Nilichoelewa hapa ni kwamba ulinusurika kugogwa na shoga siyo?:D:D:D:D:D
Wala hakuwa tena anatamani wanawake, yeye alikuwa anawinda wanauma, tatizo ni kuwa nilijua na yeye ni Khadija kama mimi kumbe mwenzangu ana ndimu mbili na bamia.
 
Wala hakuwa tena anatamani wanawake, yeye alikuwa anawinda wanauma, tatizo ni kuwa nilijua na yeye ni Khadija kama mimi kumbe mwenzangu ana ndimu mbili na bamia.
Pole sana........kuna msela'ngu aliwahi kunisimulia kisa kama ulichoeleza.......Huku duniani kuna mambo ya ajabu na magumu kuyaamini kama hukuwahi kushuhudia.
 
Back
Top Bottom