Short Story: Matabaka

Ramsy Dalai Lama

Senior Member
Apr 5, 2021
147
540
Siku moja, Mungu alinyang'anya kila mtu mali yake. Watu wote waliachwa bila chakula na walikuwa na njaa siku nzima. Siku ya pili yake jioni, Mungu alimpa kila mtu kuku.

Kundi la kwanza lilifurahi sana kupewa kuku hao na hawakufikiria chochote zaidi yakuchinja na kula kuku wao. walikula na kusaza huku wakiwa na furaha. Baadhi kati yao hawakufanya uamuzi mwanzoni, lakini walipoona maneno ya kufurahisha ya wale waliokula na kusaza, hawakuweza kujizuia zaidi na wao wakachinja kuku wao na kupika kisha wakala.

Kundi la pili nao walikuwa na njaa kali, lakini baadhi yao waliona wamepata kuku wa mayai, walivumilia njaa kwa siku tatu na wakamlea kuku, ambaye kila siku alitaga yai, wakawa wanakula hayo mayai ingawa haya wakuwashibisha sana, lakini at least waliweza pata mlo kila siku. wale wenye wajogoo wakasema watawatumia kuwaamsha asubuhi ili kuweza kulisha kuku wao wa mayai.

Kundi la mwisho hawa wakakaa wakafikia wakaona kwamba kuna wenye majogoo na wenye kuku wa mayai. wakakubaliana kwamba kuku wamayai wapandane na majogoo kisha wazalishe vifaranga. Baada ya vifaranga kukua watatenga majogoo pembeni na wa kike pembeni na wale wanaotumika kwa ajili ya mayai pembeni kisha wataendelea na program yao ya ufugaji. lakini pia wakawaza vip wata survive mpaka kuku kukua wakaona kwamba wachukue wale wamayai watage yai wapate kula. lakini pia watakula kwa zamu leo akila huyu kesho yule mpaka hapo wale vifaranga wakue. kweli wakakubaliana japo hawakuweza kushiba lakini waliona wateseke kwasasa kwa ajili ya faida ya baadae.

Baada ya muda kweli wakafanikisha malengo yao wakawa na kuku wengi wakawafuata kundi la pili wakawaomba wawape kuku wao wamayai na majogoo kisha wao watakua wakiwapa yai moja kila siku na baada ya muda watawapa mayai mawili kwa kila mtu. Kundi la pili walifikiria wakaona hawana chochote cha kupoteza hata hivyo, na pia watapata mayai wawili kuliko hapo mwanzo, kwa hivyo walikubali.

Na kweli baada ya muda wakaanza kupata wayai mawili mawili kila mtu.lakin pia huku nako kundi la kwanza la watu walikuwa na njaa, wengine walikonda sana wengine walikufa kwa njaa. Na walikuwa wakikaa chini wakilalamika kwa nini Mungu ameacha kuwapa kuku.

Kundi la pili lilikula mayai yao, huku wakapata yai lingine kutoka kwa kundi la tatu, na waliishi maisha japo si ya kuridhisha lakini at least hawakua na njaa. Kundi la tatu lilivuna vifaranga wengi sana na wakawa na kuku wengi sana wakiwemo wa mayai, wanyama, na majogoo yakutosha. kwa kweli waliweza kuishi kwa furaha sana wakijua wana chakula chakutosha. Na mwishowe wakaona watafute watu wawe wakiwafanyia kazi yaufugaji wa kuku wao. Kwa hiyo wakawaendea kundi la kwanza na kuwauliza ikiwa wangewafanyia kazi ya ufugaji basi wangeweza kupata yai na kipande cha nyama ya kuku kwa ajili ya kazi hiyo. kweli wakakubali na wakaanza kuwafanyia kazi ya ufugaji na baadhi ya kundi la pili nao wakajiunga kufanya kibarua endapo siku walijisikia wale nyama ya kuku kwasababu walichoka mda mwingine kula mayai.

Mwisho wake ikawa jamii iliyokua na usawa na kuku mmoja kwa kila mtu mwanzoni, lakini baadae ikawa na matabaka, yan kukawa na tabaka la masikini, tabaka la kati na tabaka la matajiri.

Nadhani hadithi hii inaonyesha ukweli ambao upo kwenye jamii zetu hivi leo. lakini yote haya inatokana na baadhi ya maamuzi yetu sisi wenyewe ndo itaamua wewe utaishia tabaka gani. So tujifunze kupamba kwa kila hali tutoke tulipo kwasababu lolote linawezekana ikiwa utafanya maamuzi sahihi katika muda sahihi na sehemu sahihi.

asante kwa kusoma
 
Sasa Mkuu kama watu hao walipewa kuku waliwalisha nini?
Maana kama ingekuwa pumba basi watu hao wangekula mahindi na mtu hawezi kufa njaa ikiwa anaona wadudu kama siafu au chavuchavi

UONGO HUU NIUONGOOOO UONGOOO

Labda useme ni paukapakawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom