Shonza na Mwampamba ndani ya New Habari

Shonza na Mwampamba ndani ya New Habari

Juliana na Mwampamba.

hawa vijana toka waondoke CDM basi wanapendana sana, yaani kama kulwa na doto hawaachani -- upendo wao huu ni wa ajabu na tunaomba na udumu. maana kila sehemu wako wawili hata wakienda kutoa matamko ni wawili hivyo hivyo.

Inatia moyo mno, hongereni vijana huu ndiyo upendo ambo mwenyezi mungu alisema Tupendane kama alivyoagiza yeye.
 
Juliana na Mwampamba.

hawa vijana toka waondoke CDM basi wanapendana sana, yaani kama kulwa na doto hawaachani -- upendo wao huu ni wa ajabu na tunaomba na udumu. maana kila sehemu wako wawili hata wakienda kutoa matamko ni wawili hivyo hivyo.

Inatia moyo mno, hongereni vijana huu ndiyo upendo ambo mwenyezi mungu alisema Tupendane kama alivyoagiza yeye.

Hujamalizia mkuu, wakienda kulala ....
 
Nimewasoma;wanasema walimbaba Saanane nne smu ya kumuua Zitto,katumwa na Slaa na Mbowe,kumuua Zitto kwa sababu Zitto amewalipa watu hela kumtukna Mbowe katika mtandao,katika Forums za mtandao. Sasa Shonza na mwenzake wamesahau kusema kama hizo fears za Mbowe zilikuwa justified,kwa sababu kama haya mabo kweli Zitto alifanya,what is the complaint,kwamba Mbowe anatetea reputation yake?
Pia Shonza kama amehama Chadema,lazima azungumzie Chama chake kipya cha CCM. Never mind about what sins someone else is committing. It is only your sins which should concern you,Juliana.
Kwanza aseme Zitto hakumajiri mtu yoyote kuandika mabaya kuhusu Mbowe,halafu ndio aishambulie Chadema. Otherwise this is interference katika mambo ya ndani ya Chama kingine.
 
Nimepitia maelezo ya akina Shonza na Mwampamba kwenye gazeti la mtanzania la tarehe 27 March na April 3, 2015 wakieneza propaganda zinazohusu siri ya mpango wa kumuua Zitto, lakini kwa kukosa umakini na labda kwa kuchanganyikiwa wamejikuta wakitoa maelezo tofauti kuhusu mpango huo.

Katika gazeti la Mtanzania March 27.

" Shonza alidai kuwa siku ya tukio, yeye na Zitto walikuwa wamekaa meza moja na Saanane ambaye mkono wake wa kushoto ulikuwa umefungwa bandeji aliyowaeleza kuwa aliifunga kutokana na maumivu ya mkono.

Alisema wakiwa katika maongezi, huku Saanane akionyesha kuzidiwa na kilevi alichokuwa amekunywa, alitoa bahasha ya kaki yenye fedha ili alipie gharama za vinywaji vya wote ambayo ilidondoka na ndani yake ikatoka karatasi ndogo ya nailoni ikiwa na unga mwekundu."

Wiki iliyofuata kwenye gazeti hilo hilo la Mtanzania lakini la April 3, 2013, bibie akaanza kujichanganya,
Anadai siku ya tukio zitto hakutokea. Nanukuu ya gazeti hii hapa chini.

"Kama nilivyosema awali, tulikutana na Saanane nikiwa na Mwampamba lakini Zitto hakutokea na siku hiyo ndiyo tulimkamata akiwa na ile sumu."

Tulikuwa tunazungumza huku tunakunywa vinywaji tukimsubiri Zitto na muda ulipotutupa mkono huku tukiamini kuwa hawezi kufika, Ben alitoa bahasha kwa ajili ya kulipia gharama za vinywaji ndipo kile kifuko kilichokuwa na sumu kilipondoka, tukakiona wote, akanyang’anya na hakupewa mpaka alipokiri ukweli kuwa alipewa na Dk. Slaa ili ammalize Zitto

Alisema, sumu ingewekwa kwenye kinywaji cha Zitto akiwa katika kikao hicho, lakini hatua yake ya kutohudhuria ndiyo iliyomuokoa.

Uongo mwingine ni huu, gazeti la tarehe 27 March anadai alikuwa amekaa meza moja yeye (shonza), Zitto na saanane lakini gazeti la tarehe 3 April anadai Ben Saanane na Zitto hawajawahi kukutana.

Anasema (Shonza) "Lakini ni kweli kwamba Zitto hamfahamu Ben Saanane na kwa ninavyojua mimi hawajawahi kukutana kwa sababu siku zote Saanane amekuwa akisisitiza tumkutanishe na Zitto kwa vile sisi ndiyo tulikuwa na uwezo wa kuonana naye".

Maswali yangu kwa Shonza na Mwampamba.
1. Ben alipotaka kumuwekea Zitto sumu, zitto alikuwepo hotelini au alikuwa Marekani na hakuhudhuria?
2. Na je ni kweli Ben na Zitto hawajawahi kukutana?
3. Kwa nini mlimsubiri Zitto arudi Marekani ndipo mumuulize kama muende polisi au la badala ya kwenda na huo ushahidi mkononi? Mkiambiwa kwamba nanyi mlishiriki kwenye njama za kumuua Zitto mtakataa?
4. Ben alipodondosha hiyo sumu nani aliiokota? Na kwa nini mumng'ang'anize Ben akiri kwamba ule unga ulikuwa sumu na si kilevi chake kama alivyojibu mwanzo.(kama ni kweli alidondosha kifuko cha unga mwekundu)
5. Na kama Ben alikuwa amelewa chakari hamuoni kwamba majibu yake yalikuwa ya mlevi?
6. Na kwa maoni yenu Ben angewezaje kumwekea zitto Unga mwekundu (sumu) kwenye kinywaji chake mkiwa mmekaa meza moja? is Ben Stupid?

Ninamuomba Nape na Nchemba wawaangalie hawa vijana kwa jicho la tatu kwani badala ya kuijenga CCM wanazidi kuibomoa. Hapa ni dhahiri kwamba Shonza na Mwampamba wanadhihirisha jinsi wanavyotumiwa na CCM kutaka kuiua chadema kabla ya 2015, lakini kwa uongo huu CCM itatangulia kaburini.
 
Tatizo mkuu kuna watu wanafikiri CHADEMA ina watu wajinga na kwamba CDM ni zito, Slaa na Mbowe peke yao. chadema ni taasisi yenye multiple professions. Watu kama akina Kigaila ninamwamini tangu alipokuwa na misimamo yake pale alipokuwa Rais wa DARUSO mwaka 1997 na kufuatiwa na Kitila Mkumbo. hawa tunawashukuru sana kuweza kuzuia third face Ya cost sharing . sisi watoto wa masikini tuliweza kusoma na kumaliza salama. Waliweza ku control migomo sana. Mimi niko CCM ila mbinu hizi zitatuchafulia chama. Yaani hainingii akilini yaani uwe na sumu halafu sijui umelewa halafu... Hajaja .... Kwa hili inabidi hizi story waandikiwe wanaokunywa matatapu sio wasoma magazeti.
 
Back
Top Bottom