Shonda ya mama hii

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,778
Yaliyotokea huku kwetu Kwamtogole weekend iliyopita ni haya. Shost Clara alipoona umri unakwenda hajavaa a while dress aliamua kujisogeza kanisani kwenye maombi. Kule alikutana na Joshua ambae na yeye umri umesogea kidogo. Joshua alikwenda South Africa kubangaiza na baadae Botswana amerudi amepata ajira na pale kanisani ndiyo 'church's choir master'.
Walielewana na Clara ambae ana kazi yake na mipango ya harusi ilianza. Clara alitualika harusi wote tulishangaa member mwenzetu wa Balimi anaolewa harusi ya kilokole lakini watu hubadilika basi tulifurahi.

Baada ya ndoa Clara alibahatika kupata mtoto. Kumbe alimiss beer kupita kiasi tatizo watu wote wanajua sasa sister Clara mlokole mambo ya kwenda bar ni big NO. Clara alianza kipita supermarket anachukua beer zake anaweka kwenye handbag huyo home. Akifika nyumbani anamlia timing mume wake akiwa kwenye mazoezi ya kwaya na yeye anapiga bia zake mbili analala, wakati huo ameacha kunyonyesha. Mtoto akawa anamuona mama anapiga maji ya dhahabu na yeye anayatamani,mama alimjibu hii ni soda ya mama si kwa watoto.

Brother Joshua kufikiria wema aliyotendewa na mchungaji tangia wamefahamiana hasa msaada katiaka maandalizi ya harusi, alumshauri mkewe wamkaribishe mchungaji na mkewe dinner.

Siku iliwadia namaandalizi yalifanyika, ilikuwa ni mwendo wa soda na juice za Azam, Clara aliamua kunywa maji tu, wanywaji wengi sukari sukari hazipandi. Katikati ya mlo ndipo mtoto alipozama chumbani na kuibuka na kopo la Heineken na kumwbia mama yake 'mama shoda yako hii'. Brother Joshua haamini macho yake uzuri mchungaji aliua soo haraka kwa kulikemea pepo la ulevi.
 
Haha nakemea mapepo ya aina yoyote yatambaao na yarukayo. Niseme tu kwa jina la yesu shosti mchungaji akimshindwa nitamwombea.

Nipo hapa jirani yenu
Shost analipia gharama za kutafuta a white dress
 
Mwambie amantain sasa akae nayo hadi kifo kitakapowatenganisha hapo anaharibu.
Mkuu ukiwa addicted ni kama mtu akwambie kuanzia Leo wewe si Daby si rahisi kuacha mazoea
 
Back
Top Bottom