Shoga yako anatembea na mumeo!

Mwanamke anayeipenda ndoa yake na kuthamini aibu ya mumewe hawezi kutoa mambo ya chumbani au nyumbani kwake na kuhadithia mashoga.
Matatizo yangu nitalia na mungu wangu na yakinishinda nitachagua yanayoongeleka nitaongea na mama yangu mzazi period.
 
Matatizo na raha zako tatua au share na mwenzako, na hii ni kwa wanawake na wanaume. Kwa upande mmoja, kumbuka kuwa kama utamweleza rafiki au shoga yako matatizo ya mwenzako, yeye anaweza kukuona wa ovyo, hujui kuhandle mambo na yeye kujiona staring, akafanya lile linalokushinda.

Kwa upande mwengine, kumweleza shoga yako (mara nyengine hata baadhi ya wanaume kwa marafiki zao) uzuri na utundu wa mwenzako kwenye 6x6 ndio kabisa unampa mwanya wa kwenda kujionea mwenyewe.

All in all, kama raha faidi na usimwambie mtu, kama matatizo yatatueni baina yenu au shirikisheni wazazi/walezi wenu but never to outsider hata iwe kwa sheikh au mchungaji.
 
Hebu fikiria kwamba, umebaini kuwa shoga yako wa karibu kabisa, ndiye ambaye amekuwa akitembea na mumeo au mpenzi wako. Umekuwa ukimsimulia shida zako na matatizo yako yatokanayo na ndoa yako au uhusiano wenu, yaani mume wako au huyo mpenzi wako kutotulia, ukijua unamsimulia shost wako, wakati ndiye chanzo cha madhila uliyo nayo.

Katika kumsimulia amekuwa akikupa moyo na kukuambia wanaume ndivyo walivyo na wakati mwingine amekuwa akikwambia kwamba, ukiona vipi ni bora uachane naye. Hivi sasa unagundua kwa maumivu kwamba, yeye ndiye ambaye amekuwa akikusababishia maumivu yote. Hebu sema ungefanyaje?

1. Kizuri kula na nduguyo, kibaya mtupie mbwa.
2. The only person you can trust about your wife/husband is yourself...Hata mchugaji wako usimwamni kabisa katika hilo, ije kuwa rafiki?
 
ukisimulia/ukitoa yaliyo moyoni yanayokuumiza unakuwa kama umetua mzigo hivi. But katika maisha ya sasa, simwambii mtu l.o.l awe shoga, mzazi wala nani... Binadamu wengi wanafurahi wenzao wakiwa katika matatizo. au ndo anakuzunguka. Hakuna haja ya kumwambia mtu... nitamweleza Mungu.. au ntakuja kufunguka MMU l.o.l. HAKI YA NANI VILE trust NO BODY !!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hivi kweli mnaweza kukaa kimya au mnadanganya tu humu MMU? Swala la wanawake kuwasimulia mashoga zao juu ya mahusiano yao na wenza wao au wapenzi wao ni jambo ambalo wanawake wengi hufanya sana. Ni wanawake wachache sana wanaweza kuwa hawafanyi hivyo, lakini, hata hivyo kuna baadhi ya siri zao watazivujisha tu kwa mashoga zao aidha kwa bahati mbaya au kwa kukusudia pale wanapohitaji kusifiwa japo kidogo au kuwakoga wenzie kuwa wanacho cha kujivunia................ kuweni wakweli kwa nafsi zenu, msibishe kishabiki.............!

just a salutation for you! wanawake hawa wanaofikia hata kuazimana nguo xao za ndani.........hawa wanawake wa kibongo..........thubutu. hawa wanaongela mahusiano yao ndani ya daladala aaaah wapi. kama kuna wanawake wafyatukaji wa mambo yao ya ndani basi ni hawa wa kibongo!
 
ukisimulia/ukitoa yaliyo moyoni yanayokuumiza unakuwa kama umetua mzigo hivi. But katika maisha ya sasa, simwambii mtu l.o.l awe shoga, mzazi wala nani... Binadamu wengi wanafurahi wenzao wakiwa katika matatizo. au ndo anakuzunguka. Hakuna haja ya kumwambia mtu... nitamweleza Mungu.. au ntakuja kufunguka MMU l.o.l. HAKI YA NANI VILE trust NO BODY !!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Aisee jimbo lako liko 'wazi' nije kugombea?
 
Kwanza ni kosa kumueleza shoga mambo yako yote kama unamueleza basi mpe utandu ukoko uweke mwenyewe manake mashoga wazuri hakuna tena kumebaki mafisadi, nikigundua kama ndio mkwe mwenza nikumshukuru kwa uungwana wake na kufunga njuga kumuweka mumeo atulie ili huyu shostito akijue cheo chake juu yakua inauma sanaaaaaaaaa lakini nikiwa kama mwanamke ntakikisha mume wangu nikonae nimemthibiti....

Kwenye red: Si rahisi kihivyo. Ni wako akiwa kwako, akitoka nje si wako.
Hapo ni kuvunja ukimya tu, kwa msaada wa watu wa Marekani.
 
Hahahaa mkuu umenikumbusha kipindi nasoma TIA, demu alkuwa anamsifia mpenzi wake kwa rum, shosti mmoja akajitosa, duh ilikuwa noma kinyama ndo mpaka sasa anajilia nyama yake.nikta
 
Ngumu kusema ntafanyaje hadi itokee, lakini sina tabia ya ku-share info zangu za ndani na marafiki zangu wa karibu. Yaani ni bora nimhadithie mtu wa mbaliiiiiiii kama nimezidiwa kabisa.
 
kwangu mie siwezi sema mpaka limetokea lakutokea so far i trust men kuliko hao so called shoga sijui nini kumueleza mambo yangu ........................
nimekudondokea gafla... Aisee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom