figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,654
- 59,077
Msanii mashuhuri kutoka Afrika Kusini, Sho Madjozi, ametoa ujumbe mzito kupitia ukurasa wake wa Instagram akielezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu marafiki na Watanzania kwa ujumla, kufuatia kile kinachoendelea nchini Tanzania baada ya maandamano na machafuko yaliyosababisha vifo, majeraha na kukatika kwa mawasiliano ya simu na intaneti.
Sho Madjozi amesema kuwa ameshindwa kuwasiliana na marafiki zake waliopo Tanzania na hivyo anajisikia kuhuzunishwa na hali hiyo.
Kupitia ujumbe wake, aliandika: “Tangu jana siwezi kupata marafiki zangu Tanzania kwenye simu. Niko worried sana.
Ninachokijua ni kwamba naipenda sana Tanzania. Ninaamini kuwa Watanzania, kama watu wote, wana haki ya kuchagua waongozi wao, na haki pia ya kuandamana kwa amani bila hofu au vurugu.”Ameongeza kuwa Watanzania ni watu wapole, na kwamba kwao kufikia hatua ya kupambana ni ishara kwamba “kuna jambo kubwa sana limefikia kikomo. ”Sho Madjozi pia ametuma ujumbe kwa viongozi wa Tanzania, akisema:“Kwa walio madarakani: dunia inatazama.
Mnaweza kuzima mtandao, lakini hamwezi kuzima tamaa ya kuona mabadiliko. Maombi ya watu yanapaswa kujibiwa kwa mabadiliko, siyo kwa ukandamizaji. "Akiendelea kuzungumzia maandamano yanayoendelea nchini humo, msanii huyo amewataka wananchi kuwa watulivu na kuepuka vurugu, akisisitiza kuwa:“Vurugu ni silaha yao, siyo yetu.
Tafadhali muwe salama. Tanzania daima.”Sho Madjozi ni miongoni mwa wasanii wachache wa kimataifa waliotumia majukwaa yao kuonyesha uungaji mkono kwa amani na demokrasia Tanzania, jambo lililopokelewa kwa hisia kali mitandaoni.#ForThePeople #ToThePeople #WananchiForum #Demokrasia #HakiZaKiraia #Maandamano