Shirika la ndege la Qatar kuanza safari nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shirika la ndege la Qatar kuanza safari nchini

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BabuK, Mar 14, 2012.

 1. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  MILANGO ya wawekezaji na utalii kutoka Mashariki ya Kati, India na China, inatarajiwa kufunguka zaidi baada ya Shirika la Ndege la Qatar, kuanza kutua nchini.

  Hatua ya kuanza kwa safari hiyo inayotarajiwa kuanza Julai baada ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) kukarabatiwa kwa dola za Marekani 35 milioni.

  Mradi huo ulioanza tangu Januari 2012 na utajumuisha marekebisho ya njia za ndege mpya ili kuuongezea uwezo uwanja huo na upanuzi wa majengo kwenye uwanja huo. Akizungumzia taarifa ya safari za Qatar jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kia Marco van de Kreeke alisema mpango huo utafungua milango kwa wawekezaji kutoka kwenye maeneo hayo.

  Alisema huduma mpya za kila siku kupitia Doha zitasaidia kukuza uchumi wa Taifa na kutangaza vivutio vilivyopo Kaskazini mwa Tanzania. “Uongozi wa uwanja una furaha kubwa kutokana na uamuzi uliofikiwa na Shirika la Ndege la Qatar kutumia Uwanja wa Kilimanjaro. Ushirikiano huu na Qatar Airways kupitia Doha utawarahisishia watu kutoka Mashariki ya Kati, India, China na nchi nyingine za Bara la Asia kutembelea Tanzania,” alisema.

  Alisema kituo cha Doha kinatoa fursa nyingi za kuunganisha nchi nyingine barani Ulaya ikiwamo Mji wa London ambao ni soko kubwa la vivutio vilivyoko Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Dk Aloyce Nzuki akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa safari hiyo katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini alisema kuwa mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani ikiwamo Tanga, Arusha na Manyara itafaidika kupitia vivutio vya kitalii na baadaye kukuza sekta ya utalii nchini.

  “Safari hii itakuwa na manufaa makubwa katika kukuza sekta ya Utalii wa Taifa letu. Shirika la Qatar limepata sifa mbalimbali kutokana na huduma safi wanazozitoa. Tunaamini tutafaidika sana baada ya safari hii kuanza” alisema.

  Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Akbar Al Baker alitangaza taarifa hiyo wakati wa maonyesho makubwa ya wakala wa usafirishaji wa anga na utalii maarufu kama ITB Berlin, yaliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita jijini Berlin.

  Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo jana ilisema kuwa Qatar Airways itatoa huduma za anga katika uwanja wa KIA kwa kutumia ndege aina ya Airbus A320 kupitia jiji la Nairobi.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Habari imeandikwa kana kwamba Qatar Aiways ndo inaanza kutoa huduma nchini, wakati ni kuwa itaanza pia kutoa huduma kutokea KIA. Quatar Airways imekuwa ikifanya safari zake kutoka Tanzania kupitia Dar-es-Salaam. Hivyo kinachofanyika ni kuongeza safari zaidi kwa kutumia kiwanja kingine cha KIA.
   
Loading...