Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
Aibu gani?
Amkeni.
Nyerere alishakufa.
Wamebaki wezi tu.
Watu wanatoka Pwani na India kuja kuchota madini kwenu. Munaachiwa mashimo na vumbi.
Mumelala.
Wenzenu Mwanza kula mapanki tu wameona ni upumbavu. Wamewamwaga walafi CCM.
Mkoa wenu uko full madini. Lakini ndiyo mkoa unaoongoza kwa vifo vinavyosababishwa na njaa. Aibu gani?
Nyie mnakubali mtu anashinda kwa kura moja?
Kwani mte na masala?
Acheni kutuaibisha bana.
Tz kama kawa ni shamba la bibi nasikia kule Madaba watu wanachimba Uranium kinyemela wakati wengi wetu twajua officially ni Namtumbo.
Naona yakibaki mashimo ndo tutathmini hayo mashimo
Usiwakatishe tamaa watu wa shinyanga na harakati zao za kujinasua mikononi mwa CCM shinyanga ina majimbo 5 chini ya upinzani ( Maswa 2 meatu 1 bukombe1 na Bariadi 1) na tena wa vyama viwili chadema na UDP.Kwa taarifa yako shinyanga ndiyo inaongoza kwa wingi wa majimbo ya mengi ya upinzani T-Bara na ndiyo mkoa wenye majimbo mengi ya CHADEMA.Matarajio ya wanashinyanga ni kuondokana na CCM 2015 na ukumbuke nguvu kubwa imetumika kupokonywa jimbo la shy-town na kuna kesi mahakama kuu.Ukandamizaji wa CCM upo pote TZ kinachotakiwa wote tuhamasishane kuunga mkono kuwa na tume huru na kuandikwa kwa katiba ndiyo ukombozi pekee, vinginevyo hata huko kwenu usitegemee mabadiliko.
Tafadhali watendee haki wanashinyanga usije hapa kuwavuruga
Usitumike kuwakatisha tamaa kama umetumwa sema
Nimelizaliwa Kishapu baba.
Kwa Mpendazoe.
Mimi ni shabiki wa Simba lakini nimekula yanga. Unaifahamu yanga wewe?
Siwakatishi tamaa.
Ninachowauliza ni kwamba uko wapi ujasiri wao?
Nitawauliza na tena na tena na tena.
Kwa nini waliacha mtu akashinda kwa kura 1?
Kwa nini usiulize JK kuingizwa madarakani na wapiga kura millioni 5 wakati waliojiandikisha ni millioni 20 ? nakuona unafikiria taratibu kwani hata ubabe wa CCM huna taarifa nao.Kwa taarifa yako hata kwako kishapu upinzani ulipita. je unatushawishi tushangae kwa vipi Nchambi mjukuu ni mbunge wako??
Tafakari kabla hujafungua jamiiforum kuwajuza watu.
Wewe una matatizo.
Au umetumwa.
Tena wewe si msukuma.
Sisi huwa hatujui kubambeleza.
Kwa kuwa hatujui kubembeleza ndo maana nawauliza tena Wanashinyanga, ilikuwaje kuwaje wakaruhusu CCM kushinda kwa kura 1?
Hoja yangu ni clear: 2015 sitaki kusikia Shinyanga kuna jimbo linaongozwa na CCM.
Siwezi kusubiri 2014 au 2015 kupaza sauti yangu.
Hapa tunajadili maswala ya nchi si ya wasukuma.Wasukuma hawana ubaguzi kama wewe ni wastaarabu sana lakini wewe unazidi kuwaudhi, haufanani na wasukuma, wewe si msukuma.shinyanga ni ya watanzania si wasukuma
hapo kwenye red: wewe ni juha.
kama ni ya Watanzania kwa nini viongozi wa Tanzania wanaipuuza?
Hauna tofauti na JK anayetangaza udini kila kukicha.
Naamini wasukuma wahako upande wako, wao ni watanzania
usijipendekeze kwa wasukuma bwana weeeeeee!!
Usituletee ubaguzi wako na JK, wasukuma ni WATANZANIA na ndiyo maana wanapokelewa kila wanapohamia na mifugo yao na kufanya kilimo.Wasukuma wapo Mpanda , Mbalali, ifakara, kilosa na kwa sasa wanaingia Lindi.Hii ni kwa sababu hawajitambulishi kwa usukuma wao kama navyo-advocate wewe mbaguzi,
wao wanajitambulisha kwa Utanzania wao.
ELIMIKA NDUGU ACHA UBAGUZI KAMA JK
Mabadiliko si siku moja ni mchakato, hivyo usije ukadhani hawa watu wamelala, Kimya kingi ......Aibu gani?
Amkeni.
Nyerere alishakufa.
Wamebaki wezi tu.
Watu wanatoka Pwani na India kuja kuchota madini kwenu. Munaachiwa mashimo na vumbi.
Mumelala.
Wenzenu Mwanza kula mapanki tu wameona ni upumbavu. Wamewamwaga walafi CCM.
Mkoa wenu uko full madini. Lakini ndiyo mkoa unaoongoza kwa vifo vinavyosababishwa na njaa. Aibu gani?
Nyie mnakubali mtu anashinda kwa kura moja?
Kwani mte na masala?
Acheni kutuaibisha bana.