Almasi na ukakasi Katika aridhi ya Tanzania

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
ALMASI, KITU KIDOGO KILIVYO WEZA KULETA UKAKASI KATIKA ARIDHI YA TANZANIA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Tuesday -1/02/2022
Iringa Tanzania

Kuna Kisa cha kiarabu huko Iran cha miaka 2400 iliyopita inayoelezea kuwa chanzo cha almasi ni kutoka huko Uajemi, kwenye moja ya miliki ya mfalme Cyrus l, inaeleza kuwa mfalme alitumia Almasi kama mapambo yake.

Hakuna ushahidi wa hili kwenye masalia ya vitu kale vya hekaru la mfalme huyo kuthibitisha hilo, japo Kisa hiki kimebaki maarufu sana Bara Arab.

Ila...........

Habari za kwanza za uhakika kuhusu almasi ilianza kujulikana miaka 2327 iliyopita, huko India.

Hii ni kwamba madini ya almasi kwa mara ya kwanza yaligunduliwa huko nchini INDIA na mfalme Alexander the great wa Macedonia, huyu ndio mtu wa kwanza duniani katika historia iliyoandikwa alietoa madini India na kupeleka barani ulaya mnamo mwaka 327 B.C.

Hii Inamaana kwamba kabla ya Alexander mkuu hakuna kitu kilichoitwa almasi kilikuwepo ulaya wala wazungu hawakujua kitu chochote kuhusu almasi.

Basi bwana......

Mwaka 1725 wachimbaji wa dhahabu ya sesa nchini BRAZIL waliokota jiwe ambalo wao kama wao hawakuweza kulitambua kama ni jiwe gani ila baada ya jiwe hilo kuchukuliwa na kwenda kufanyiwa vipimo ilionekana kuwa ni jiwe la almasi.

Mwaka 1859 madini ya almasi yaligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini ambayo yalikuwa yanapatikana katika mgodi wa kwanza wa MWAMBA mwaka 1868.

Kufatia hilo hatmaye mgodi wa madini ya almasi ulifunguliwa rasmi nchini Afrika kusini tokea muda huo nchi ya Afrika kusini mpaka leo hii migodi hiyo bado inaendelea kuchimbwa madini ya almasi na haujawahi kukata almasi mpaka leo.

Mpaka muda huu madini ya almasi yanapatikana kwa wingi katika nchi zifuatazo, Russia, Australia, South Africa, Botswana, Zimbabwe, Angola, Namibia na DRC Congo.

Sasa basi........

Madini ya almasi ndio JIWE GUMU kuliko mawe yote yaliyopo katika dunia hii, au ndio madini magumu kuliko madini yote, kwa ugumu huu almasi huwa inamatumizi mbalimbali kama kukatia vioo, kutobolea miamba n.k

Madini ya almasi ndio madini magumu kuliko madini yote kama nilivyosema hapo juu, madini ya almasi ndio madini yenye thamani kubwa kuliko madini yote duniani, madini ya almasi ndio madini yenye uwezo mkubwa wa kutawanya mwanga kukiko madini yote, madini ya almasi ndio MFALME wa madini ya vito, nadhani sasa unanielewa.

Hii ni kwamba madini ya almasi huwa yapo ya rangi zote unazoziona kwenye Upinde wa mvua kwani almasi ipo ya rangi Nyeupe, Nyekundu, Blue,njano, Pink, Nyeusi, Ndigo na kadharika.

Pamoja na yote hayo katika rangi za madini ya almasi, rangi ya almasi ambayo ina thamani kubwa kule almasi ya aina yeyote ni almasi ya rangi nyekundu, na hii ina thamani kubwa sokoni kwa kuwa ndio rangi Adimu zaidi kupatikana kuliko almasi za rangi nyingine hivyo kwa kuwa haipatikani kirahisi basi jiwe lake sokoni bei yake sio ya kitoto.

Mnunuzi na mzalishaji mkubwa wa madini ya almasi duniani ni kampuni iitwayo "DE BEERS GROUP".

Hapa sasa ndio nataka kueleza......

Lengo la makala hii nikueleza kuhusu hawa wamiliki wa madini ya almasi duniani, kwanini ni wao? Na historia ya madini ya almasi nchini Tanzania na namna Almasi ilivyosababisha UKAKASI ndani ya uso wa Tanzania

Kwanza kabisa.....

Hawa DE BEERS GROUP ndio kampuni mama inayo miliki zaidi ya asilimia 90 ya stock ya madini ya almasi duniani kote, kampuni hili ndio inapanga bei ya almasi katika soko la dunia, kwa lugha nyepesi ndio muuamuzi wa mwisho wa soko la almasi katika soko la dunia.

Kiasili hawa "DE BEERS GROUP" ni Makaburi wa kiyahudi wa Afrika kusini, ambao uzao wao unatokana na visalia vya Wayunani wenye asili ya Ujerumani, hili ntalieleza hapo baadae kidogo.

Hii familia ndio imekuwa na umiliki wa madini ya almasi dunia nzima kwa zaidi ya miaka 150 sasa wao ndio "A Strange Mining Story wealthy reading" duniani kote.

Kimsingi biashara ya madini Duniani, imekamatwa na familia mbili tu za Kiyahudi, Moja ikijielekeza kwenye madini ya dhahabu (na jamii zake) ambao ndio hapo wakina BARRICK na moja katika madini ya almasi ambao ndio DE BEERS, Hawa ndio "wamiliki" wa madini yote ya dunia, bila kujali mipaka ya nchi walipo na kule yalipo madini.

Ni kwamba.......

Familia ya Kiyahudi ya Oppenheimer (waliohamia Afrika kusini ndio wenye kampuni ya "De Beers Group of Co.", ndiyo "imejimilikisha" madini yote ya almasi yaliyopo katika dunia hii baada ya "kumpoka kwa nguvu" umiliki wa kampuni Cecil Rhodes.

Kuanzia madini ya India, Brazil, Afrika Kusini, Angola, Siera Leone na Botswana mpaka Mwadui, Shinyanga nchini Tanzania hadi Siberia ni "mali" ya De Beers.

Hapa kwa Mwadui Shinyanga, ntaeleza kidogo......

Mji wa Mwadui upo katika mkoa wa Shinyanga upo kilomita 23 (14 mile) kutoka Shinyanga mjini, ni moja ya Miji maarufu sana duniani kutoka na kuwepo machimbo ya Almasi, mji huo pia hufahamika kama mji wa Mgodi wa Almasi wa Williamson.

Mwadui ipo kaskazini mashariki mwa Shinyanga nchini Tanzania, mji huu ulijulikana sana kama mgodi wa kwanza Afrika wa almasi nje ya Afrika Kusini, Mgodi huu ulianzishwa mwaka wa 1940 na Dk John Williamson, mwanajiolojia wa kutokea Canada.

Na umekuwa ukifanya kazi mfululizo tangu wakati huo, na kuufanya kuwa mojawapo ya migodi mikongwe zaidi inayoendelea kuendesha migodi ya almasi duniani, Katika maisha yake yote mgodi huu wa Mwadui umezalisha zaidi ya karati milioni 19 (kilo 3,800 ) za almasi.

Ripoti ya 2020 iliyotolewa na "The Guardian" ilisema kwamba almasi ya ubora wa juu ya waridi kutoka mgodi wa Mwadui inaweza kuwa na thamani ya hadi dola $700,000.

Sasa basi..........

Mwaka 1940, Dr John Williamson alifungua mgodi wa almasi Mwadui, nje kidogo ya mji wa Shinyanga, Mwadui ilikuwa na mkanda wa "kimberlait" wenye hifadhi nyingi ya almasi, Dr Williamson raia wa Canada, akautengeneza mji mdogo wa Mwadui na kuwa moja kati ya miji bora sana kusini mwa jangwa la Sahara (Mwadui Township).

Kufikia mwaka 1947, Dr Williamson alikuwa amejenga nyumba bora za wafanyakazi, hospital ya kisasa, shule za msingi tatu, mbili za wafanyakazi wa kiafrika na moja ya wafanyakazi wa kizungu ambayo ndio ilikuwa moja ya "English Medium School" ya kwanza Tanganyika.

Akajenga chuo cha Ufundi wa aina zote ndani ya mgodi kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi, chuo cha kilimo na shule ya upili yani sekondari, Huko kwao waliita "School Near The Equator" Ilikuwa shule bora na ya kisasa.
.
Dr Williamson akajenga uwanja wa ndege wa kisasa ndani ya mgodi mwaka 1940's, akanunua ndege mbili za mwanzo aina ya Dakota DC 3 na Cessna 180 wakati huo hata serikali ya Kikoloni ya Muingereza ikiwa haina wazo la ndege, wakati serikali ya Tanganyika ikiwa haina uhakika wa uwanja wa ndege kupokea ndege kubwa aina ya Dakota DC4.

Dr Williamson alikuwa tayari na uwanja huo, ambapo wageni toka London Uingereza, ndege zilitua Malta, Khartoum Sudani na baadae Nairobi (Wakati huo ukiitwa Embakasi Airport), na baadae kuchukuliwa na ndege moja kwa moja mpaka Mwadui Shinyanga, ambapo Serikali ya Kikoloni ilikuwa na afisa mmoja wa uhamiaji.

Dr Williamson alijenga kanisa na msikiti bora na wa kisasa kwa ajili ya wafanyakazi wake.

Wakati huo, usafiri pekee wa watumishi wa serikali ya Kikoloni ilikuwa ni meli maarufu ya "The Braimer Castro" iliyokuwa inatoka Ulaya mpaka Mombasa, Yeye Dr Williamson na wafanyakazi alioajili walikuwa wanapanda ndege kupitia Embakasi na baadae Mwadui.

Williamson akajenga "Power House" yenye uwezo wa kuzalisha 900kw kwa mitambo ya diesel na 750kw kwa Gas Turbine na hivyo kuwa na umeme wa uhakika kuliko hata jiji la Dar es Salaam achilia mbali mkoa wa Shinyanga.

Wakati huo umeme wa Dsm ulikuwa unategemea ule mtambo ulioweka pale makao makuu ya Wizara ya Nishati kama makumbusho kwa sasa.

Ndani ya mgodi wa Mwadui, Dr Williamson alijenga "Sailing Club", yaani Club inayoelea katika bwawa alilichimba eneo la Songwa, hii ndio ilikuwa Club pekee inayoelea Afrika na Kusini mwa Jangwa la Sahara.

May 2,1952, Gazeti Kongwe la "The Cairns Post" (Est.1882) liliandika juu ya uwepo wa bwawa la Songwa, Mwadui Shinyanga, Tanganyika, Gazeti hilo la Australia lilielezea bwawa la Songwa kama moja kati ya "Artificial dam" kubwa zaidi duniani, lenye uwezo wa kuchukua "two thousands million gallons of water", Mradi ambao hata serikali ya mkoloni iliushangaa.

Mwadui kulikuwa na mfumo wa maji safi na maji taka yaliyotibiwa na wataalamu waliosomeshwa na mgodi, Huduma ya elimu ya watu wazima na elimu ya uchumi wa nyumbani "home economics" kwa wamama waliokuwa nyumbani ilikuwepo.

Kufikia mwaka 1970, karibu 97% ya wakazi wa mgodi huo ambao walifikia 60,000 walikuwa wanajua kusoma na kuandika, na wamama wakiwa na ujuzi wa ushonaji, upishi nk.

Dr Williamson aliajiri mpishi maarufu toka Ufaransa, ambaye alikuwa akipika na kuandaa chakula katika "mesi" kubwa ndani ya mgodi wa Mwadui, Mfaransa huyo alifundisha wapishi wengi wa Kiafrika na alikuwa kama "chuo" cha wapishi wengi wa maafisa wa serikali ya kikoloni, na hata wapishi wa mwanzo wa Ikulu ya Dsm baada ya Uhuru, walipita katika mafunzo ya "mesi" ya Mwadui.

Kufikia mwaka 1950,Tanganyika ilikuwa na vyumba viwili tu vyenye hadhi ya kulala familia ya kifalme ya Uingereza, chumba kimoja katika Ikulu ya sasa ya Dsm na kingine kwenye "rest house" ndani ya mgodi wa Mwadui.

Mgodi wa Mwadui chini ya Dr Williamson, uliweza kujenga kiwanja cha golf chenye mashimo tisa, ambacho kilikuwa ni moja ya viwanja vikubwa na vya kisasa Afrika nzima wakati huo.

Mwaka 1952, Dr alishawishi mpaka mashindano makubwa ya kombe la Malikia la Golf nchini Canada yafanyike Mwadui, kila kitu kilikubalika isipokuwa hali ya uwanja wa Embakasi Kenya haukuwa sawa sababu ya vuguvugu la vita vya Maumau lililotishia usalama wa kiwanja, hivyo mashindano yakashindikana kufanyika Mwadui, Swimming Pool za viwango vya Olympic tatu ndani ya mgodi zilijengwa.

Viwanja vya tennis, pamoja na viwanja vitatu bora vya mpira wa miguu vilivyokuwa na viwango vya kimataifa vilijengwa ndani ya mgodi wa Williamson, Timu ya mpira ya Mwadui Mining ilishiriki mashindano ya kitaifa kwa ubora mkubwa.

Waamuzi wakongwe wa viwango vya kimataifa kama Mshangama na Mashishanga (RC wa zamani) ni matunda ya Dr Williamson, kama Ulikuwa ufahamu hilo.

Ustawi wa maisha ya mgodi na kushamiri kwa faida ya Dr Williamson kuliwauzi "wamiliki" wakubwa wa biashara ya madini ya almasi ambao ni De Beers Group of Co.

Hapa sasa ndio vita ikaanza......

Almasi ya Mwadui iliingia kwa kasi sana katika soko la dunia jijini London, De Beers wakashindwa kumdhibiti Dr Williamson na almasi yake, mpaka ikapelekea almasi ya Afrika Kusini kushuka thamani katika soko la dunia, njia pekee iliyobaki kwa De Beers ilikuwa kumtaka Dr Willy aungane nao katika biashara.

Dr Willy alikataa, akataka kuupeleka mgodi kwa namna yake, hakutaka kuwanyonya Waafrika na wafanyakazi wake, ndoto zake ilikuwa ni kuijenga "Quebec ndogo ndani ya Tanganyika", alitaka kuonyesha tofauti ya thamani ya madini na maisha ya wazawa kwa kuutumia mgodi wa Mwadui.

Aliiishi Afrika Kusini na kuona jinsi wazawa wa kando ya migodi na wafanyakazi wasivyofaidika na madini katika ardhi yao, Dr Willy hakutaka hali hiyo itokee.

Mkoloni na De Beers walichukia uamuzi wa Dr Williamson kuufanya mgodi wa Mwadui kama "Ulaya ya Afrika", Walim-fustrate kwa kukataa kuipokea almasi yake katika viwanda vya wachonga almasi kule London (diamond Cutting).

Mwaka 1950, Serikali ya kikoloni kwa Shinikizo la familia ya Oppenheimer wakataka kuutaifisha mgodi wa Mwadui ili uwe mali ya serikali ya mkoloni na si mtu binafsi.

Hali hii ilichanganya sana Dr Williamson,akawa mlevi wa kupindukia wa whisky ya Scotland,akawa "chain Smoker" na kwa sababu alikuwa "bachelor" hakuwa na mtu wa kumtuliza mawazo.

Mwaka 1952, mwezi Machi, kampuni ya De Beers ilimtuma mtoto wa kwanza wa mmiliki wa kampuni, Herry Oppenheimer kuongea na Dr Williamson namna ya kuuza sehemu ya hisa kwa De Beers ili aweze kuwa "salama", Dr Williamson alisitasita sana, akawaza jinsi wafanyakazi wake wa kiafrika na wale aliowaleta toka Ulaya watakavyonyanyasika, akawaza jinsi ndoto yake ya kujenga "Mji wa Quebec wa Afrika" inavyopotea.

Mwaka 1956...Princess Margareth akiambatana na Gavana wa Tanganyika na ujumbe wake walitembelea mgodi wa Mwadui wakiwa ndani ya ndege aina ya Dakota DC4 mali ya Dr Williamson walishangaa sana kuona maendeleo ndani ya Mwadui.

Ikumbukwe kuwa ziara hii ya mwanamfalme Margareth ilikuwa ni mbinu ya ushawishi kumfanya Dr aachie sehemu ya hisa za mgodi

Kwa shingo upande akatoa 50% yake kwa kuwauzia De Beers kwa £4 milioni, miaka michache baadae akagundulika kuwa na saratani ya koo, ugonjwa uliochukua maisha yake miaka michache baadae (japo ilisemekana ulipandikizwa ili kumuondoa).

Dr Williamson aliomba kuwa akifa mwili wake uzikwe ndani ya eneo la Mwadui kwani kwake Mwadui ndio ilikuwa nyumbani.

Mwaka 1958, Herry Oppenheimer ndio akawa mwenyekiti wa Mgodi wa Mwadui, sehemu ya hisa za Dr Williamson aliachiwa dada yake, na kwa sababu hakuwa na uzoefu wa mambo ya madini, De Beers wakamshauri aziuze.

De Beers na serikali ya kikoloni wakawa na 50/50 ya umiliki wa mgodi na almasi yote ya Mwadui, mdoto na mipango ya De Beers na familia ya Oppenheimer ikawa imetimia, nayo ni "KUMILIKI MADINI YOTE YA ALMASI CHINI YA ARDHI YA DUNIA.

Mchezo ukaishia hapo......

Kabla De Beers awajafaidi matunda ya mgodi wa Mwadui, Tanganyika ikapata uhuru, Mwl Julius Nyerere alipochukua nchi 1961, baadae aliamua kutaifisha mali zote, akaunda Stamico isimamie sekta ya madini.

De Beers iliwauma sana kufurushwa na Nyerere, hawa Waisrael wakaunda team ya namna ya kumkomesha Julius Nyerere, kwanza waliweka fitna katika soko la almasi pale London, wakazishawishi "Diamond Cutting and Polishing Companies" kule London ziisusie almasi ya Mwadui, Mwalimu akawa mbishi na kuimarisha "TunCut Diamond Co" pale Iringa.

De Beers akazidi kuweka fitna kwenye viwanda vinavyotengeneza vipuri vya mitambo iliyopo Mwadui, Kuanzia mitambo ya kuchimba, kusafisha na kuchambua almasi.

Mwishowe vifaa vikachakaa bila kuwa na ukarabati, uzalishaji ukapungua na almasi ya Mwadui ikapotea katika soko la dunia.

Wataalamu toka nje waliokuwa katika mgodi wa Mwadui wakaondoka, Ikawa ni hasara juu ya hasara.

Mwaka 1993, De Beers kupitia Herry Oppenheimer yuleyule wa enzi za Dr Williamson walirudi Tanzania kupitia mtoto wao Nicolaus Oppenheimer, wakaishawishi serikali ya Tanzania, na hatimaye De Beers Group of Co wakauziwa 75% ya hisa za mgodi wa Mwadui, Hatimaye ile ndoto yao ya kumiliki madini yote ya almasi ya dunia ikaendelea kutimia.

Hawa ndio De Beers, familia ya Kiyahudi ya Oppenheimer, Wanaosadiki kuwa almasi yote inayopatikana katika uso wa dunia hii ni mali yao.

Walimsurubu Dr John T. Williamson, mzungu-msukuma aliyetaka mali ya ardhi ya Mwadui ilete thamani kwa Waafrika na Tanganyika.

Hawa ndio De Beers waliomtikisa Mwalimu Nyerere, hawa ndio familia ya almasi duniani, wanaochochea yale ya Angola ya Savimbi, Siere Leone ya Foudah Sankho na Almasi ya damu "blood diamond" na DR Congo ya M23 ili waendelee kuchota utajili wa Afrika.

Wayahudi ndio wanaomiliki benki kuu za duniani kupitia kwa familia ya Rothschild wa Marekani ambao wanamiliki asilimia 80 ya uchumi wa dunia nzima.

Jambo zuri ni kwamba Wayahudi huwa wanamiliki na kuendesha biashara zao na uchumi wao kifamilia na kiukoo ndiyo maana wamekuwa na nguvu kubwa kiuchumi duniani.

Kumbukumbu kubwa inayobakia mpaka sasa kuhusu mgodi wa Mwadui ni kuhusu Almasi ya kuvutia zaidi iliyo chimbwa kwenye mgodi huo ni pamoja na almasi ya waridi yenye karati 54 ambayo ilitolewa kwa Princess Elizabeth na Prince Philip wakati wa harusi yao mwaka wa 1947, kama zawadi.

Na pia almasi ya karati 388 iliyopatikana mwaka wa 1990, ambayo ndio Almasi ya pink kubwa zaidi duniani, hata hivyo Mgodi wa Mwadui unaendelea kuwa chanzo cha almasi adimu ya pink ulimwenguni.

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
Written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.
FB_IMG_1644401517961.jpg
 
Hongera sana kwa historia nzuri ya mgodi wa Williamson Diamonds. Bila shaka huyu Mzungu angekuwa ni Binadamu wa kwanza, miongoni mwa Wazungu, mwenye uchungu wa kuwatakia na kuwaletea maendeleo Waafrika! RIP Dr. Williamson.
 
We jamaa umeongia mzima mzima hivi unajua kwamba madini inayojua dunia yako Tanzania ni asilimia 20 tu.mfano umesema almasi ndio madin ghal pole mkuu unajua bei ya longido ruby? Unajua bei ya alexandrite ya songea .unaijua bei ya trsovarite garnet ya mto mbwa.kifupi almas haipo top 10 ya madini ghal tanzania.
 
hivo vijimadini vyako ni vya humu humu Tanzania. Duniani hazipo miongoni mwa madini ghali na uapatikanaji wake hautabiriki tofauti na Almasi na Dhahabu.
We jamaa umeongia mzima mzima hivi unajua kwamba madini inayojua dunia yako Tanzania ni asilimia 20 tu.mfano umesema almasi ndio madin ghal pole mkuu unajua bei ya longido ruby? Unajua bei ya alexandrite ya songea .unaijua bei ya trsovarite garnet ya mto mbwa.kifupi almas haipo top 10 ya madini ghal tanzania.
 
hivo vijimadini vyako ni vya humu humu Tanzania. Duniani hazipo miongoni mwa madini ghali na uapatikanaji wake hautabiriki tofauti na Almasi na Dhahabu.
Madini pekee ambayo unaweza ya ita ya humu ndani ni tanzanite .mengine yako masoko yote ya kimataifa.afu dhahabu kuwa uhakika kupata nakubari .ila kuhusu almas kaka ni mziki mwingine
 
We jamaa umeongia mzima mzima hivi unajua kwamba madini inayojua dunia yako Tanzania ni asilimia 20 tu.mfano umesema almasi ndio madin ghal pole mkuu unajua bei ya longido ruby? Unajua bei ya alexandrite ya songea .unaijua bei ya trsovarite garnet ya mto mbwa.kifupi almas haipo top 10 ya madini ghal tanzania.
Tuwekee bei zake ktk soko la dunia
 
Madini pekee ambayo unaweza ya ita ya humu ndani ni tanzanite .mengine yako masoko yote ya kimataifa.afu dhahabu kuwa uhakika kupata nakubari .ila kuhusu almas kaka ni mziki mwingine
Naomba bei za hayo madini toka mto mbwa bei zake ktk masoko ya duniani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom