Shinyanga: Mwanamke amchinja mume wake kisa wivu wa mapenzi

View attachment 593098

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 2;30 usiku wakati mwanamke huyo akiwa na mumewake nyumbani kwao, gafla simu ya mwanaume iliita ndipo mkewe akaichukua na kupokea,... akasikia sauti ya Mwanamke, na kupeleka hisia huenda ni mume wake anamsaliti, ndipo ugomvi ukazuka hadi kusababisha mauaji.

Akitoa taarifa ya tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Simoni Haule, alisema baada ya ugomvi huo kuzuka ndipo mwanamke alipochukua kitu chenye ncha kali, na kumchinja shingo mume wake na kusababisha mauaji papo hapo, ambapo mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa huo.

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi ambapo mwanamke mara baada ya kuita simu ya mumewe aliikimbilia kuipokea, na aliposikia sauti ya mwanamke tayari akajua ni hawala wa mmewake, ndipo wakaanza kupigana hadi kusababisha mauaji,”alisema Haule

Hata hivyo Kamanda Haule alisema Jeshi hilo linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi, na uchungunzi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji linalo mkabili, iliapate kuchukuliwa hatua kali zaidi za kisheria.

CHANZO: Nipashe

 
Matokeo ya semina elekezi za kina mama kuhusu kupinga mfumo dume ndiyo hizi sasa - Mwenyezi Mungu aliwapa uwezo huo walionao, sasa sisi kwa ujuzi ujuzi wetu tunaanza kuwafundisha mambo mengi ambayo hawakupewa na Muumba wa mbingu na nchi.

Sasa wanaume tujiunge kupingania haki zetu tulizopewa na Mwenyezi Mungu wakati wa uumbaji. - tukicheza hawa akina EVA hawa ni hatari sana wanaweza kutupoka zote.

Sasa ona, wengine nasikia wanapangiwa hata siku za kupata unyumba wenye ndoa, sasa ole wako ujaribu kugusa gusa siku ambayo siyo ya ratiba uone kitakachokukuta - haya wengine nao huo unyumba hawapati kabisa - tunakokwenda siko, lets go back to the root....
 
Jamani,huu ndo uzezeta wa mapenzi,mme unae then simu tu ya mtu ambae hujui hata alipo unasababisha mauaji.Ndo ukaozee pale Mhumbu sasa.Stupid wife.
 
Mapenzi kwa kweli yanapaswa kuingizwa kati ya vitu vinavyohatarisha uhai wa binadamu

Ikiwezekana kuwe na bima ya mapenzi.
 
so sad RIP,

kanipa funzo ni mwendo wa kublock michepuko yote nikiwa home...!!
Unajuaje kama aliyepiga alikuwa mchepuko?
hawezi kuwa relative?
work mate?
business call?
ordinary friends call?

Anyway, kama mkeo ni wa design hiyo iko siku yatakupata Ya kukupata(God forbid )
 
Back
Top Bottom