Shinyanga: Mwanamke amchinja mume wake kisa wivu wa mapenzi

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
kisu.jpg


Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 2;30 usiku wakati mwanamke huyo akiwa na mumewake nyumbani kwao, gafla simu ya mwanaume iliita ndipo mkewe akaichukua na kupokea,... akasikia sauti ya Mwanamke, na kupeleka hisia huenda ni mume wake anamsaliti, ndipo ugomvi ukazuka hadi kusababisha mauaji.

Akitoa taarifa ya tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Simoni Haule, alisema baada ya ugomvi huo kuzuka ndipo mwanamke alipochukua kitu chenye ncha kali, na kumchinja shingo mume wake na kusababisha mauaji papo hapo, ambapo mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali ya mkoa huo.

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi ambapo mwanamke mara baada ya kuita simu ya mumewe aliikimbilia kuipokea, na aliposikia sauti ya mwanamke tayari akajua ni hawala wa mmewake, ndipo wakaanza kupigana hadi kusababisha mauaji,”alisema Haule

Hata hivyo Kamanda Haule alisema Jeshi hilo linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi, na uchungunzi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji linalo mkabili, iliapate kuchukuliwa hatua kali zaidi za kisheria.

CHANZO: Nipashe

 
Hasira za kuiga kwenye movie za kizungu sasa zimemtokea puan
 
Back
Top Bottom