Shinyanga: Mwanamke amchinja mume wake kisa wivu wa mapenzi

Hii nayo imenishangaza, mwanamke apitishe kisu kwenye koromeo langu tens tukiwa katika mapambano, huu uzembe wa mwanamme, labda kama alikuwa amelala
Mkuu wewe wa vimbaumbau eh?hujakutana na mshine jike zilizoshiba eh? Kuna mijike zaidi ya ngumi ya kichwa au ndosi moja maridhawa huna cha kumfanya sijui ulete mieleka mieleka au kukabanakabana atakutoa nnya hivi hivi unajiona kilo mia plus za kimazoezi zikukalie halafu zimeshika kisu ukitilia maanani una mfadhaiko wa kufumaniwa ,hutaki kumpa upercut au cross punch za uso kuhofia kumuumiza na hapo ndipo tunapochemka maana mwanamke huwezi kumnyuka jumla jumla kama mwanaume mwezako ni grapling na vibao vya hapa na pale!.
Inshort utachinjika tu!
 
Matokeo ya semina elekezi za kina mama kuhusu kupinga mfumo dume ndiyo hizi sasa - Mwenyezi Mungu aliwapa uwezo huo walionao, sasa sisi kwa ujuzi ujuzi wetu tunaanza kuwafundisha mambo mengi ambayo hawakupewa na Muumba wa mbingu na nchi.

Sasa wanaume tujiunge kupingania haki zetu tulizopewa na Mwenyezi Mungu wakati wa uumbaji. - tukicheza hawa akina EVA hawa ni hatari sana wanaweza kutupoka zote.

Sasa ona, wengine nasikia wanapangiwa hata siku za kupata unyumba wenye ndoa, sasa ole wako ujaribu kugusa gusa siku ambayo siyo ya ratiba uone kitakachokukuta - haya wengine nao huo unyumba hawapati kabisa - tunakokwenda siko, lets go back to the root....
Siku hizi kesi za kunyimwa unyumba zimekwisha !shikamoo michepuko
 
wanaume wa mikoani wameanza kuiga ulegelege wa wanaume wa mkoa wa bashite. mwanamke anakuchinjaje labda kama alihisi mahaba niue
 
Aione zarina hassan..........mondi akija kwako toa kichwaa mazima hawezi kukuletea upupu. ......huyo ndo mwanamke jasiri sasa sio kutwa kulialia tu .....unatoa kichwa unaenda kula ugali wa bure uko gerezani fullstop
 
Hii nayo imenishangaza, mwanamke apitishe kisu kwenye koromeo langu tens tukiwa katika mapambano, huu uzembe wa mwanamme, labda kama alikuwa amelala
Unayafahamu ma mwanamke ya Kikurya wewe? Yameenda hewani halafu yamejazia, sasa wewe kimwili kama cha Humphrey Polepole utaweza wapi kulikabili?
 
MKAZI wa Kata ya Tinde katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Zena Mohamedi (28) anashikiliwa na Polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumuua mumewe, Bakari Salehe (35) kwa kumchinja shingo kwa madai ya wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Simon Haule alisema tukio hilo limetokea juzi saa 2.30 usiku wakati mwanamke huyo akiwa na mume wake nyumbani kwao, simu ya mwanamume iliita ndipo akaichukua mkewe huyo na alipoipokea akasikia sauti ya mwanamke, na ndipo ugomvi na majibizano yalipoanzia.


Kamanda Haule alisema baada ya ugomvi huo kuzuka, ndipo mwanamke alipochukua kitu chenye ncha kali na kumchinja shingo mume wake na kusababisha kupoteza maisha, na mwili wake tayari umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.


“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi ambapo mwanamke mara baada ya kuita simu ya mumewe aliikimbilia kuipokea, na aliposikia sauti ya mwanamke mwingine kwa hisia zake akaona tayari ni hawara wa mume wake, ndipo wakaanza kupigana hadi kusababisha kifo,” alisema Haule.


Hata hivyo, Kamanda Haule alisema jeshi hilo linamshikilia mwanamke huyo kwa mahojiano zaidi na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji lililotokea na kutumia kitu chenye ncha kali. Aidha, kamanda alitoa mwito kwa wananchi kuacha tabia za ugomvi wakutumia vitu vyenye ncha kali.

Chanzo: Habari Leo
 
Aisee!!! Mauaji ya wivu wa kimapenzi yameshika kasi sana cjui tatizo nn!! Kama umeoa au kuolewa kwann usitulie!?
 
Back
Top Bottom