Shinyanga: Kelele hizi za muziki usiku mbona zimeachwa tu?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Nasikitika sana tangu saa tisa nimeshindwa kulala kutokana na muziki mzito sana ninaosikia nikiwa maeneo ya Lubaga Inn.

Muziki huu ni wa kwaya na sielewi ni kwa nini wameweka sauti nzito sana ya base kiasi kwamba inatikisa hadi kichwa juu ya mto nilioegemeza.

Hivi hata kama mnafariji watu msibani hamjui kuwa wanahitaji kupumzika pia?

Tafadhali naomba mamlaka za Shinyanga mliangalie hili maana sio mara ya kwanza.

Kumbukeni tuna majukumu mengine asubuhi hii pamoja na kuwa tulichelewa kulala tukiangalia match za UEFA.

Bahati mbaya saa tisa naamshwa tena na muziki mzito.

Kama mna nia ya ujumbe kufika punguzeni uzito wa base tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Brother unafeli. Ikiwa tu sauti ya muziki ni kubwa, fundi mitambo atapataje notification (kama umethibitisha yuko jf) ilhali simu yake ame_mute? Amka taratibu nenda eneo la tukio waeleze wahusika. Vinginevyo ujumbe wataupata asubuhi wakati ushaenda job
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom