Shindano la tuzo ya ushairi Tanzania limefunguliwa,washairi kazi kwenu.

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,856
2,000Shindano la tuzo ya Ushairi ya Ebrahim Hussein limefunguliwa rasmi. Ewe mshairi uliopo Tanzania wasilisha tungo yako kabla ya tarehe 31/07/2018. Hakikisha unazingatia vigezo na masharti!
MASHARTI
• Hili ni shindano la utunzi wa ushairi katika lugha ya Kiswahili tu.
• Kwa mwaka huu, tungo zitakazoshindan
ishwa ni za aina mbili tu: mashairi na nyimbo. Tenzi/Tendi na kazi za kinathari, kama riwaya au tamthilia, hazitahusika.
• Kila mshiriki awasilishe tungo moja tu.
• Tungo iwe ni ya mtunzi mwenyewe.
• Tungo iwe mpya kabisa. Yaani, isiwe imepata kuchapishwa au kutiwa katika CD au kanda; kuchezwa jukwaani, redioni au katika televisheni, au kusambazwa katika mitandao.
• Bahari zitakazoshindanishwa ni: Kundi A: Mashairi (ya kimapokeo au huru/
masivina); Kundi B Nyimbo: za kimapokeo, k.m. bongo fleva.
• Kila utungo wa kimapokeo uzingatie kanuni za kijadi za utunzi, na usipungue beti 7 au kuzidi beti 8.
• Utungo huru usipungue mishohoro (mistari) 3 wala kuzidi mishohoro 50.
• Kila mshiriki awasilishe tungo moja ikiwa aidha ni shairi la kimapokeo, huru-masivina au nyimbo ya bongo fleva.
• Mtunzi atachagua mwenyewe mada na maudhui ya utungo wake.
• Tungo iheshimu miiko ya kijamii na kimaadili.


MAELEKEZO ZAIDI
Kila mshiriki aambatanishe ukurasa wenye maelezo mafupi yenye kuzingatia yafuatayo:
•Jina lake kamili, wasifu na sifa zake kwa ufupi (umri, jinsia, kazi, utunzi wake).
•Anwani ya posta/makazi, anwani-pepe, na namba ya simu ya mkononi.
•Maelezo kuwa mswada ni kwa ajili ya shindano la Ushairi la Ebrahim Hussein.
•Tungo zichapwe kwa kompyuta, upande mmoja wa karatasi, kwa kutumia herufi za ukubwa wa pointi 12, na kuacha nafasi moja na nusu baina ya mistari.
•Tarehe ya mwisho ya kupokea tungo ni tarehe 31/07/2018.
•Tungo ziwasilishwe kwa kutumia barua pepe tunzoushairi@gmail.com
 

FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,366
2,000
Hii ni habari nzuri.

Ila hujsema mshindi anazawadiwa nini? kikombe/fedha/cheti n.k.

Pia nina wasiwasi na baadhi ya maneno kama yanafahamika vema na kila mtu, kwa mfano neno mishohoro....hakuna ufafanuzi zaidi wa neno hilo?
 

Thad

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
12,732
2,000
Hii ni habari njema, ngoja nikae na majagina wangu tujinyakulie tunzo hiyo
 

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,856
2,000
Hii ni habari nzuri.

Ila hujsema mshindi anazawadiwa nini? kikombe/fedha/cheti n.k.

Pia nina wasiwasi na baadhi ya maneno kama yanafahamika vema na kila mtu, kwa mfani neno mishohoro....hakuna ufafanuzi zaidi wa neno hilo?
inaonyesha hapo katika posters na neno mshororo linaleweka kwa watunzi wa mashairi kuwa ni nini.
ila kwa msaada tu ni MSTARI ULIOPO KATIKA KILA UBETI WA SHAIRI.
karibu sana.
 

FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,366
2,000
inaonyesha hapo katika posters na neno mshororo linaleweka kwa watunzi wa mashairi kuwa ni nini.
ila kwa msaada tu ni MSTARI ULIOPO KATIKA KILA UBETI WA SHAIRI.
karibu sana.
Swadakta.

Natumai na ukomo wa umri kwa Washiriki hakuna.
 

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
16,304
2,000
Hii ni habari nzuri.

Ila hujsema mshindi anazawadiwa nini? kikombe/fedha/cheti n.k.

Pia nina wasiwasi na baadhi ya maneno kama yanafahamika vema na kila mtu, kwa mfano neno mishohoro....hakuna ufafanuzi zaidi wa neno hilo?
WATUNZI WA MASHAIRI WANALIELEWA!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom