Shilingi

Red Scorpion

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,736
4,252
1452163453906.jpg
 
Huko nyuma hasa wakati wa utawala wa mkweree watu walizoea kutokulipa kodi na yeye mwenyewe aliamini kuwa maendeleo ya nchi yataletwa kwa kuomba omba toka kwa wafadhili hivyo mapesa yakawa mengi yanazunguka nchini bila kuongeza uzalishaji na mfumuko wa bei ukawa juu!! Sasa Magufuli amekuja na " HAPA NI KAZI TU" mimi kwa tafsiri yangu ni kwamba hataki wala haamini kuwa maendeleo yetu yatakuja kwa kuwategemea watu wa nje iwe kwa kuomba au kukopa bali maendeleo yetu yatakuja kwa kufanya kazi sisi wenyewe kwa kutumia rasilimali zetu kwa ufanisi na tija katika uchumi wetu; hivyo ndio tunaweza kupata sustainable development!!

Wale waliozoea mission town ndio sasa wanalalamika kuwa shilingi haionekani lakini kwa wale waliozoea kuchacharika shilingi itaonekana tena ikiwa na thamani ya juu!! Tukaze buti tu kwani mambo mazuri yanahitaji subira.
 
Back
Top Bottom