Shilingi Bilioni 15 Kusaidia Uhifadhi Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa na Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess, wameshuhudia kusainiwa kwa Mkataba wa Utekelezaji wa Mradi wa Bilioni 15 (Euro milioni 6), Kusaidia Tanzania Kupambana na Wanyama Waharibifu katika maeneo ya Kusini mwa Tanzania.
1f744d3e-6aa0-481f-b9eb-5da1b83db9f0.jpg

c7532592-eb13-46e3-8d4a-8b8ba58840d9.jpg

Mkataba huo umetiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi na Dkt. Mike Falke, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Ujerumani nchini (GIZ), Aprili 20, 2023.

“Kusainiwa kwa mkataba huu ni ishara kuwa Serikali imeanza na itaendelea kulipa uzito suala la uhufadhi na hasa kupunguza athari za wanyama waharibifu kama tembo kwa kushirikiana na wadau kama mnavyoona hapa leo,” alisema Waziri Mchengerwa.
dc052169-1eeb-45a9-8b4f-49b894d69b36.jpg

8b0c93bc-1b7c-427b-892a-0375cc67aeb5.jpg
 
Back
Top Bottom